2023
Ninawezaje Kuamini pasipo Kuona?
Julai 2023


“Ninawezaje Kuamini pasipo Kuona?,” Liahona, Julai 2023.

Njoo, Unifuate

Yohana 20

Ninawezaje Kuamini pasipo Kuona?

Picha
Yesu akiwatokea wale Thenashara baada ya Ufufuko Wake

Maelezo kutoka Yesu Akiwatokea wale Thenashara baada ya Ufufuko, na Scott Snow

Mmoja kati ya Mitume wa Yesu Kristo, Tomaso, hangeamini kama Kristo angefufuka mpaka alipomwona katika mwili (ona Yohana 20:25). Na hatimaye Tomaso alipomwona Mwokozi aliyefufuka, Mwokozi alimwambia, “Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki” (Yohana 20:29).

Ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mwaliko wa Yesu wa “wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye”? (Yohana 20:27).

Njia za Kuimarisha Imani na Ushuhuda

Jifunze maandiko. “Imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” (Warumi 10:17).

Ishi injili. “Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kama mimi nanena kwa nafsi yangu tu” (Yohana 7:17).

Tafuta ufunuo kutoka kwa Roho Mtakatifu. “Ukweli wa msingi sana unadhihirishwa tu kwa ufunuo kutoka kwa Mungu. Sababu zetu za kibinadamu na utumiaji wetu wa fikra za kimwili havitatosha.” (Henry B. Eyring, “Roho Mtakatifu kama Mwenza Wako,” Liahona, Nov. 2015, 104).