2023
Safari Yangu kwenye njia ya agano
Septemba 2023


Makala

Safari Yangu kwenye njia ya agano

Nilipofikisha miaka 18, umri wa kwenda misheni, mimi na baba yangu tuliweka mpango wa fedha ili kuniruhusu niweke akiba ili niweze kujitayarisha kutumikia misheni. Kimsingi, baba yangu aliniamini kwa usimamizi wa moja ya biashara zake, kwa masharti mawili. Nilipaswa kulinda uwekezaji wake katika biashara na kutumia faida kuchangia kwa ajili ya misheni yangu.

Kufuatia hali ngumu ya uchumi kutokana na vurugu za kisiasa za wakati huo, sikuweza kutengeneza faida kubwa kama nilivyokuwa nimepanga. Ilikuwa ngumu kwangu kulinda uwekezaji na kufilisika kulianza kutishia kwenye upeo wa macho.

Ili kuanzisha biashara yenye mafanikio, ni muhimu kuwa na msingi imara kifedha.

Kama ilivyo kwa biashara yoyote yenye faida, fedha za kutosha ni muhimu na ni msingi kwa ajili ya uendeshaji wenye tija. Ikilinganishwa na vipengele muhimu kwa ajili ya uanzishaji wa biashara, sisi pia tunahitaji kuwa na mahala pa kuanzia au msingi kote katika safari yetu kwenye njia ya agano.

Msingi Wetu Ni Upi?

Tukirejelea biashara ya baba yangu, tunaweza kujiuliza: ni yapi mambo muhimu au misingi ya maisha? Je, tunayo hata moja? Ikiwa ndivyo, yamejikita juu ya nini? Ni juu ya nini tumeyakita maisha yetu, maamuzi yetu na wakati wetu ujao?

  • Je, tunayakita maisha yetu juu ya kile kinachoweza kufilisika kwa sababu ya mdororo wa kiuchumi au vurugu za kisiasa?

  • Au badala yake je, tunayakita maisha yetu kwenye idadi ya “likes” tunazopata kwenye mitandao ya kijamii?

  • Na vipi kuhusu miito yetu ya Kanisa?

Je, hii inatoa mtazamo kamili wa maisha yetu na kile tunachokifanya?

Ikiwa tutarudi nyuma kwenye ushauri wa baba yangu, ambao ulikuwa kulinda kampuni yake kutokana na ushawishi iliyokuwa nao juu yangu, je, hii si ya kulinganishwa na maisha yetu?

Katika Kitabu cha Mormoni, ushuhuda mwingine wa Yesu Kristo, nabii Helamani aliwafundisha wana wake kile wanachopaswa kuyakita maisha yao juu yake na sababu ya kufanya hilo:

“Na sasa, wana wangu, kumbukeni, kumbukeni kwamba ni juu ya mwamba wa Mkombozi wetu, ambaye ni Kristo, Mwana wa Mungu, kwamba lazima mjenge msingi wenu; kwamba ibilisi atakapotuma mbele pepo zake kali, ndio, mishale yake kimbungani, wakati mvua yake ya mawe na dhoruba kali itapiga juu yenu, havitakuwa na uwezo juu yenu kuwavuta chini kwenye shimo la taabu na msiba usioisha, kwa sababu ya mwamba ambako kwake mmejengwa, ambao ni msingi imara, msingi ambako watu wote wakijenga hawataanguka.” (Helamani 5:12)

Hatupaswi kuyakita maisha yetu kwenye maoni ya watu wengine, kipi wanachofikiria, kipi vyombo vya habari husema kuhusu sisi, umaarufu wetu kupimwa kwenye mitandao ya kijamii au chochote chenye umaarufu sana leo. Lakini, katika siku ya magumu yetu, je, tunalinda uwekezaji ndani yetu? Yesu Kristo, kwa upande mwingine, daima atakuwepo pale. Yeye atatusaidia. Atatusaidia tufanye chaguzi sahihi. Kama Yeye mwenyewe alivyoahidi katika M&M 50:44 “Kwa hivyo, Mimi nipo katikati yenu, na mimi ni mchungaji mwema, na jiwe la Israeli. Yule ajengaye juu ya, mwamba huu hataanguka kamwe.”

Wakati wa safari yangu kwenye njia ya agano, nimejifunza kwamba Bwana hafanyi lolote bila kuwafunulia watumishi wake manabii, siri yake. Kwa baraka ya Nabii wa kipindi chetu cha maongozi ya Mungu, katika ujumbe wake wa kwanza kama Rais wa Kanisa, Rais Russell M. Nelson alisema:

“Msimamo wako wa kumfuata Bwana na kufanya na kutii maagano Naye utafungua mlango wa baraka na fursa zote za kiroho zilizopo kwa wanaume, wanawake na watoto kila mahali. […]; ibada za hekaluni na maagano unayoyafanya huko ni msingi wa kuimarisha ndoa yako, familia yako na uwezo wako wa kuhimili mashambulio ya adui. Kuabudu na huduma hekaluni hapo kwa ajili ya mababu zako kutakuletea ongezeko la ufunuo na amani na kuimarisha msimamo wako wa kubaki kwenye njia ya [agano].”1

Hekalu ni mahala pekee ambapo tunaweza kuimarisha misingi yetu na kuwa salama kipindi cha nyakati za kushindwa ambazo zitatikisa maisha yetu kwenye njia ya agano.

Tanbihi

  1. Russell M. Nelson, “Tunaposonga Mbele Pamoja,” Liahona, Apr. 2018, 7.