2023
Kanisa Linaunga Mkono Juhudi za Serikali ya Uganda za Kuboresha Afya ya Wasichana na Mahudhurio Shuleni
Septemba 2023


Habari za Kibinadamu

Kanisa Linaunga Mkono Juhudi za Serikali ya Uganda za Kuboresha Afya ya Wasichana na Mahudhurio Shuleni

Msaada umewezekana kwa dhabihu za waumini waaminifu wa Kanisa kote ulimwenguni.

Watawala wa Jimbo la manispaa ya Makindye Ssaabagabo nchini Uganda waligundua kwamba wasichana wadogo wanaohudhuria shule za wilaya mara nyingi hawakufika madarasani kwa sababu familia zao hazikumudu kuwanunulia taulo za kike wakati wa mizunguko yao ya hedhi.

Viongozi hawa wa umma waliwageukia wamisionari wa huduma za kibinadamu wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kwa ajili ya kusaidiwa. Kwa kutumia fedha za Kanisa zilizotolewa kama msaada, wamisionari walinunua taulo za kike 1500 zinazoweza kufuliwa na kutumika tena kutoka kwa kampuni iliyo nchini Uganda na kuziwasilisha kwa viongozi wa Jimbo la manispaa ya Makindye Ssaabagabo mnamo Januari 23, 2023.

Visanduku hivi vitasambazwa kwa wasichana wanaotoka katika familia zenye kipato cha chini wanaohudhuria shule 15 zinazosaidiwa na serikali kote katika manispaa kwa miezi ijayo. Viongozi wa serikali watasimamia usambazaji na kufuatilia kwa viongozi wa shule kuona kwamba uhudhuriaji shuleni unaimarika.

Viongozi kadhaa wa serikali wa eneo husika walihudhuria hafla ya makabidhiano. Hawa ni pamoja na Mheshimiwa Dkt. Ssonko Shafiq, Mwenyekiti, Mheshimiwa Nakilambi Deborah, Mwenyekiti Msaidizi, Lwanga Ronald, Mkaguzi wa Mashule, Prossy Kizza, Mweka hazina, Jumba Ahmed, Mkaguzi Msaidizi wa Afya na Aide Kalibbala Katerega, Mwenyekiti wa Uzalishaji, Jimbo la Ndejje.

Kanisa liliwakilishwa na John Katerega, mshiriki wa uaskofu wa Kata ya Kabowa, Patricia Ekeesit, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kigingi cha Kampala Uganda South na wamisionari wa Kanisa wa huduma za kibinadamu Mzee na Dada Bird.

Dkt. Ssonko Shafiq, wa uongozi wa jimbo, alielezea shukrani kwa kazi ya Kanisa katika eneo na kusema manispaa inatazamia kushirikiana zaidi na Kanisa. Wasichana wengi wana mahudhurio yasiyoridhisha darasani kwa sababu wazazi hawawezi kumudu kununua taulo za kike kwa ajili ya wanafunzi wa kike na hilo huwasababisha wabaki nyumbani wakati wa mzunguko wao wa hedhi.

Kaka Katerega alifafanua kwamba msaada huu uliwezekana kwa dhabihu za waumini waaminifu wa Kanisa, ambao hujinyima chakula siku moja kila mwezi na kutoa pesa ambayo wangeitumia kwa Kanisa kwa ajili ya miradi ya kibinadamu kama huu. Alitoa ushuhuda wake wa Injili ya urejesho ya Yesu Kristo na kuwaalika hadhira kuhudhuria mikusanyiko iliyoko kwenye maeneo yao ili wajifunze zaidi.

Maelezo ya Picha: Hayfield ya ugawaji wa taulo za kike huko Makindye Ssaabagabo, Uganda mnamo Januari 23, 2023. Mstari wa mbele: Wasswa Godfrey, Karani Mkuu Msaidizi wa Mji, Mary Nakilambi, kaimu mwenyekiti wa jimbo na Afisa Elimu Wilaya, pamoja na Kaka na Dada Katerega. Mstari wa nyuma: Patricia Ekeesit, Dada na Mzee Bird, Dkt. Ssonko Shafiq na Mhazini Prossy Kissa.