2010–2019
Kukaribia Kiti cha Enzi cha Mungu kwa Imani
Oktoba 2014


Kukaribia Kiti cha Enzi cha Mungu kwa Imani

Kwa kutumia Upatanisho wa Yesu Kristo unaweza kuanza kuongezea imani yako ya kiroho leo kama utakuwa tayari kusikiliza na kutenda.

Katika mizani ya 1 hadi 10, unaweza kupima vipi uhakika wako wa kiroho mbele ya Mungu? Je! Una ushahidi wa kibinafsi kwamba kujitolea kwako kwa sasa kama Mtakatifu wa Siku za Mwisho kunatosha kuridhi uzima wa milele? Unaweza kusema kwamba Baba wa Mbinguni anafurahishwa nawe? Ni mawazo gani yanayokujia akilini kama ungekuwa na mahojiano na Mwokozi wako katika dakika moja kutoka sasa? Je! Dhambi, majuto, na mapungufu yangezidi vile unavyojiona, au utapata tu matarajio ya furaha? Je! Utatazama au utakwepa uso Wake? Je! Utasita mlangoni au utatembea hadi Kwake kwa uhakika?

Kila wakati adui anaposhindwa kuwashawishi Watakatifu wasio kamili wanaojitahidi kama wewe kuacha imani yako katika Mungu binafsi na mwenye upendo, yeye hutumia njama kali kuweka umbali mkubwa iwezekanavyo kati yako na Mungu. Adui anajua kwamba imani katika Kristo---aina ya imani ambayo huzaa mtiririko thabiti wa rehema nyororo na hata miujiza mikubwa----huambatana na uhakika wa kibinafsi kwamba unajitahidi kuchagua kilicho sahihi. Kwa sababu hiyo atatafuta kila njia kuingia ndani ya moyo wako kukuambia uongo---uongo kwamba Baba wa Mbinguni hafurahishwi nawe, kwamba Upatanisho u mbali sana nawe, kwamba hakuna hata haja ya kujaribu, kwamba kila mtu mwingine ni bora kuliko wewe, kwamba wewe hustahili, na mbinu elfu za mpango huu mwovu.

Almradi unaruhusu sauti hizi zichonge kwenye nafsi yako, huwezi kujongelea kiti cha enzi cha Mungu kwa kujiamini kweli. Chochote unachofanya, chochote unachoombea, chochote unachotumainia muujiza unaweza kukipata, daima kutakuwa na shaka ya kutojiamini ikichubuachubua imani yako---si imani yako katika Mungu tu, bali pia kujiamini kwako binafsi. Kuishi injili katika njia hii si rahisi, wala si vyema. Juu ya yote, haifai kabisa! Uamuzi wa kubadilika ni wako, na wako peke yako.

Ningependa kushiriki mapendekezo sita ambayo, kama yatafuatwa, yataondosha hizi sauti ovu na kurejesha kwako aina ya uhakikisho wa amani na imani ya kiroho ambayo ni yako kama tu unaitaka. Bila kujali unavyojipima mwenyewe katika mizani ya 1 hadi 10, kwa kutumia Upatanisho wa Yesu Kristo unaweza kuanza kuongezea imani yako ya kiroho leo kama utakuwa tayari kusikiliza na kutenda. Mimi nitanena kwa ujasiri, nikitumaini kukuelimisha na si kukuhudhi.

1. Chukua jukumu la hali yako njema ya kiroho yako mwenyewe. Koma kuwalaumu wengine au hali zako, koma kujitetea, na ukome kutoa vijisababu kwa nini hujitahidi kuwa mtiifu. Kubali kwamba wewe una “uhuru kulingana uanadamu” na “haki kuchgua uhuru na uzima wa milele” (2 Nefi 2:27). Bwana anajua hali zako vyema, lakini pia anajua vyema kama tu unachagua kutoishi injili kikamilifu. Kama hivi ndivyo ilivyo, kuwa mwaminifu ya kutosha kukiri. Na ujitahidi kuwa mkamilifu katika mazingira yako ya hali. Uhakika wa kiroho huongezeka unapochukua jukumu la hali yako ya kiroho mwenyewe kwa kutumia Upatanisho wa Yesu Kristo kila siku.

2. Chukua jukumu la hali njema yako ya kimwili mwenyewe. Nafsi yako inajumuisha mwili wako na roho yako (ona M&M 88:15). Kulisha nafsi hali unatelekeza mwili, ambao ni hekalu, kwa kawaida hupelekea kwenye ukinzani wa kiroho na kulegea katika kujistahi. Ikiwa hauko sawa kimazoezi, ikiwa hujisikii vizuri na mwili wako mwenyewe na unaweza kufanya kitu juu yake,basi kifanye! Mzee Russell  M. Nelson amefunza kwamba tunafaa “kuchukulia mwili wetu kama hekalu letu wenyewe” na kwamba tunapaswa “kuthibiti lishe yetu na mazoezi ya kimwili” (“We Are Children of God,”Ensign, Nov. 1998, 87;Liahona, Jan. 1999, 103).

Rais Boyd  K. Packer amefunza kwamba “roho na mwili wetu imeunganishwa katika njia kwamba mwili huwa chombo cha akili yetu na msingi wa silka yetu.” (“The Instrument of Your Mind and the Foundation of Your Character” [Church Educational System fireside, Feb. 2, 2003], 2; speeches.byu.edu). Kwa hivyo, tafadhali tumia hukumu nzuri katika kile utakachokula na hasa kiasi utakachokula na kupatia mwili wako mazoezi unaohitaji na yanayoufaa. Kama unajiweza kimwili, amua leo kuwa bwana wa mwili wako mwenyewe na uanze mpango wa kila mara na kuendelea wa mazoezi, unaofaa uwezo wako, ukijumlishwa na lishe bora.Kujiamini kwa kiroho huongezeka roho yako, kwa msaada wa Mwokozi, kikweli ndiye anayesimamia mtu au mwanamke wa kawaida wako.

3. Kubali kabisa kwa hiari, moyo mkujufu utiifu kama sehemu ya maisha yako.Tambua kwamba huwezi kumpenda Mungu bila pia kuzipenda amri Zake. Viwango vya Mwokozi ni wazi na rahisi: “Mkinipenda, mtazishika amri zangu” ” (Yohana 14:15). Utiifu wa kuchaguachagua huleta baraka za kuchaguachagua, na kuchagua kitu kibaya badala ya kitu kibaya sana bado ni kuchagua kosa. Huwezi kutazama sinema baya na utarajie kujisikia mwema kwa sababu hukutazama sinema bayasana. Uzingativu wa uaminifu wa baadhi ya amri hautetei kutekeleza zingine. Abraham Lincoln alisema vyema: “Ninapofanya vyema, najisikia vyema. Ninapofanya vibaya, nasijikia vibaya” (Katika William  H Herndon na Jesse William Weik, Herndon’s Lincoln, “The True Story of a Great Life,vols. [1880], 3:439;.

Pia, fanya mambo sahihi kwa sababu sahihi. Bwana, ambaye “anahitaji moyo na akili yenye kukubali” (M&M 64:34) na ambaye “ni mtambuzi wa mawazo na makusudi ya moyo” (M&M 33:1), anajua kwa nini unaenda kanisani, kama wewe upo hako katika mwili pekee au kikweli kuabudu. Hauwezi kuimba Jumapili, “Ee, Babeli, Ee, Babel [mimi] nakupigia kwaheri” na kisha utafute na kukubali uenzi wake tena dakika chache badaye (“Ye Elders of Israel,” Hymns, no. 319). Kumbuka kwamba uholelaholela katika mambo ya kiroho kamwe si furaha. Lifanye Kanisa na injili ya urejesho kuwa maisha yako yote, si tu sehemu ya maisha yako ya nje au kijamii. Kuchagua siku hii nani ambaye utamtumikia ni jambo la mdomo mpaka tu pale utaishi kihalisi vile ikupasavyo (ona Yoshua 24:15). Kujiamini kwa kiroho huongezeka unapokuwa unajitahidi kikweli, kwa sababu zilizo sahihi, na kuishi maisha yaliyowekwa wakfu, licha ya mapungufu yako!

4. Kuwa mwepesi, mwepesi kabisa katika kutubu kabisa na haraka.Kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo ni halisi sana, unapaswa kuutumia kwa wingi kwa masaa 24/7, kwa vile kamwe haukauki. Kubali kabisa Upatanisho wa Yesu Kristo na toba kama vitu ambavyo vinafaa kukaribishwa na kutumika kila siku kulingana maagizo ya Tabibu Mkuu. Anzisha mtazamo wa kuendelea, wa furaha, toba ya shangwe kwa kuifanya kuwa namna ya maisha yako kwa uchaguzi. Kwa kufanya hivyo, jihadhari na majaribu ya kuahirisha, na usitarajie ulimwengu kukushangilia, Lenga macho yako kwa Mwokozi, jali zaidi kuhusu kile Yeye anachofikiria juu yako, na uyaache matokeo yafuate. Kujiamini kwa kiroho huongezeka unapotubu dhambi zote ndogo na kubwa kwa hiari na kwa furaha wakati huo huo kwa kutumia Upatanisho wa Yesu Kristo.

5. Kuwa mwepesi, mwepesi kabisa wa kusamehe. “Mimi, Bwana, nitamsamehe yule nitakaye kumsamehe, lakini ninyi mnatakiwa kuwasamehe watu wote” (M&M 64:10). Msamehe kila mtu, kila kitu, wakati wote, au angalau jitahidi kufanya hivyo, basi kuruhusu msamaha katika maisha yako mwenyewe. Usiweke kinyongo, usiudhike haraka, samehe na samehe haraka, na kamwe usifikirie kwamba umeachiliwa kutoka kwa amri hii. Kujiamini kwa kiroho huongezeka tunapojua kwamba Bwana anajua kwamba hauna hisia mbaya kwa mtu mwingine.

6. Kubali majaribio, vipingamizi, na “mastaajabu” kama sehemu ya uzoefu wetu wa maisha ya muda. Kumbuka kwamba uko hapa kuthibitishwa na kutahiniwa, ili kuona kama [wewe] utafanya mambo yote yale ambayo Bwana Mungu [wako] atawaamuru” (Ibrahimu 3:25)—na acha niongeze, “katika hali zote.” Mamilioni ya kina ndugu na kina dada wamesha au wanatahiniwa, sasa kwa nini wewe uachiliwe? Majaribio mengine huja kupitia kutotii kwako au kupuuza. Majaribio mengine huja kwa sababu ya kutekeleza wengine au tu kwa sababu huu ni ulimwengu ulioanguka. Majaribio yanapokuja wafuasi wa adui wanaanza kutangaza kwamba umefanya kitu makosa, kwamba hii ni adhabu, ishara ambayo Baba wa Mbinguni hakupendi. Puuza hayo! Badala yake, jaribu kulazimisha tabasamu, tazama mbinguni, na useme, “Mimi naelewa, Bwana. Mimi najua hiki ni nini. Ni wakati wa kujithibitisha, ama siyo?” Kisha ungana Naye kuvumilia vyema hadi mwisho. Kujiamini kwa kiroho huongezeka unapokubali kwamba “kila mara majaribio na taabu zinaruhusiwa kuja katika [maisha yako] kwa sababu ya kile [wewe] unachofanya sahihi”(Glenn L. Pace, “Crying with the Saints” [Brigham Young University devotional, Dec. 13, 1987], 2; speeches.byu.edu).

Nikiwa ninasimamia Misheni ya Ukraine Kyiv, wakati mmoja nilimuuliza mojawapo wa kina dada waaminifu kwa nini yeye daima alikuwa anajihukumu sana, kwa nini yeye daima alikuwa anasononeka kwa ajili ya mambo madogo. Jibu lake lilikuwa asili sana la mtu anayesikiliza sauti isiyo sahihi alipokuwa anajibu, “Ili mtu yeyote asinishinde mimi katika hilo.”

Kina ndugu na kina dada, ushauri wangu kwa dada huyu mmisionari ni ushauri wangu kwenu: tambua na mkabiliane na udhaifu wenu, lakini msilemazwe nao, kwa sababu baadhi yake itakuwa ni wenzi wenu mpaka mtakapoondoka kutoka kwa maisha ya duniani. Bila kujali hali yenu ya sasa ni nini, ile dakika wewe utachagua kwa uaminifu, furaha, toba ya kila siku kwa kujitahidi kufanya hivyo na kuwa bora zaidi, Upatanisho, hukufikia na hukufuata popote uendapo. Ukiishi kwa njia hii, kwa kweli unaweza “daima kuhifadhi msamaha wa dhambi zenu” (Mosia 4:12) kila saa la kila siku, kila sekunde ya kila dakika, na basi kuwa msafi kabisa na kukubalika mbele za Mbungu wakati wote

Nafasi ni yenu, kama mkiitaka, njoo mjijulie wenyewe, leo au karibuni, kwamba mnampendeza Mungu licha ya mapungufu yenu. Nashuhudia juu ya Mwokozi mwenye upendo ambaye anatutarajia tuishi amri. Nashuhudia juu ya Mwokozi mwenye upendo ambaye ana hamu sana ya kutoa neema na rehema Zake. Nashuhudia juu ya Mwokozi mwenye upendo ambaye hufurahia tunapotumia Upatanisho Wake kila siku kwa uhakikisho tulio nao wa furaha kwamba sisi tunatazama mwelekeo sahihi. Nashuhudia juu ya Mwokozi mwenye upendo ambaye ana hamu ya kujiamini kwenu kuongezeke nguvu katika uwepo wa Mungu (ona (M&M 121:45). Katika jina la Yesu Kristo, amina.