2010–2019
Ukuhani wa Matayarisho
Oktoba 2014


Ukuhani wa Matayarisho

Katika matayarisho ya ukuhani, “nionyeshe” ni muhimu kuliko “niambie”

Nina shukrani kukusanyika na ukuhani wa Mungu, ambao umesambaa duniani kote. Nashukuru kwa imani yenu, huduma yenu, na maombi yenu.

Ujumbe wangu jioni hii ni kuhusu ukuhani wa Haruni. Ni kwetu sote pia ambao tunasaidia katika kupatikana kwa ahadi za Bwana kwa wale wenye kile kinachoelezewa kwenye maandiko kama “ukuhani mdogo.”1 Vile vile unajulikana kama ukuhani wa “matayarisho.” Ni kwa maandalizi hayo matukufu ambayo nitayazungumzia jioni hii.

Mpango wa Bwana kwa ajili ya kazi Yake umejawa na maandalizi. Aliiandaa dunia kwa ajili yetu kupata ujuzi wa majaribio na fursa za maisha ya hapa duniani. Tunapokuwa hapa, tunakuwa katika kile maandiko yanakiita “hali ya maandalizi”2

Nabii Alma alielezea umuhimu mkubwa wa maandalizi hayo kwa ajili ya uzima wa milele, ambapo tutaishi milele katika familia na Mungu Baba na Yesu Kristo.

Alielezea haja ya maandalizi kwa njia hii: “Na tunaona kwamba mauti yanampata binadamu, ndio, mauti ambayo yamezungumziwa na Amuleki, ambayo ni mauti ya muda; walakini mwanadamu alipewa nafasi ya kutubu; kwa hivyo maisha haya yakawa ya hali ya kujaribiwa wakati wa kujitayarisha kukutana na Mungu; wakati wa kujitayarisha kwa ile hali isiyo na mwisho ambayo imezungumzwa nasi, ambayo ni baada ya ufufuo wa wafu”3

Kama vile muda tuliopewa kuishi katika maisha ya duniani ni kujiandaa kukutana na Mungu, muda tuliopewa kuhudumu katika Ukuhani wa Haruni ni fursa ya kujiandaa kujifunza jinsi ya kutoa msaada muhimu kwa wengine. Kama vile Bwana atoavyo msaada tunaouhitaji ili kufaulu mtihani wa maisha ya duniani, vile vile anatutumia msaada katika maandalizi ya ukuhani.

Ujumbe wangu ni kwa wale ambao Bwana huwatuma kusaidia kuandaa kama ilivyo kwa wale Wenye Ukuhani wa Haruni. Nazungumzia akina baba. Nazungumza kwa maaskofu. Na nazungumza kwa wale wa Ukuhani wa Melkizedeki ambao wameaminiwa kuwa wenza wa vijana ambao wako kwenye maandalizi ya ukuhani.

Nazungumza katika kutukuza na katika shukrani kwa wengi wenu duniani kote na kwa wakati wote.

Sitakuwa naonyesha shukrani kama sitanena kuhusu rais wa tawi na askofu wa ujanani mwangu. Nilikuwa shemasi nikiwa na miaka 12 katika tawi dogo sehemu ya mashariki ya Marekani. Tawi lilikuwa dogo sana kiasi kwamba kaka yangu mkubwa na mimi tulikuwa pekee wenye ukuhani wa Haruni mpaka baba yangu, ambaye alikuwa rais wa tawi, alipomwaalika mtu wa makamo kujiunga na Kanisa.

Mwongofu mpya alipokea ukuhani wa Haruni na pamoja na hiyo aliitwa kuulinda ukuhani wa Haruni. Bado nakumbuka kama vile ilikuwa ni jana. Ninaweza kukumbuka matawi mazuri katika msimu wa kipupwe wakati mwongofu huyu mpya alipoambatana na kaka yangu na mimi kufanya kitu kwa ajili ya mjane. Sikumbuki mradi ulikuwa ni nini, lakini ninakumbuka hisia ambazo zilitusaidia kukifanya kitu nilichojifunza baadaye kwamba Bwana alikuwa amekisema kwamba lazima sote tufanye ili tusamehewe na hivyo tuwe tayari kumwona.

Hivi sasa nikikumbuka tukio hilo hapo nyuma, ninahisi shukrani kwa rais wa tawi ambaye alimwita mwongofu mpya kumsaidia Bwana kuandaa vijana wawili ambao baadaye wangekuwa maaskofu wenye majukumu kuwasaidia maskini na wenye mahitaji na pia kusimamia ukuhani andalizi.

Nilikuwa bado ni shemasi wakati familia yangu ilipohamia kwenye kata kubwa katika Utah. Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza nilipohisi nguvu ya jamii kamili katika Ukuhani wa Haruni. Kwa kweli, ilikuwa mara ya kwanza kuona moja. Na baadaye ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuhisi nguvu na baraka za askofu msimamizi katika jamii ya makuhani.

Askofu aliniita kuwa msaidizi wake wa kwanza katika jamii ya makuhani. Nakumbuka kwamba alifundisha kwenye jamii yeye mwenyewe—jinsi alivyokuwa na kazi nyingi na kuwa na wanaume wengi wenye vipaji ambao angeweza kuwaita kutufunza. Alikuwa na viti darasani vilivyopangwa kwenye mduara. Aliniomba nikae kwenye kiti karibu yake upande wake wa kulia.

Niliweza kumwangalia kupitia bega lake alipofundisha. Aliangalia chini mara kadhaa kwenye muhtasari aliouchapa kwa uangalifu katika faili dogo kwenye mapaja yake na katika maandiko yaliyokuwa yamealamishwa na kuchakaa kwa sababu ya kutumika ambayo alikuwa ameyaweka kwenye goti lingine. Ninaweza kukumbuka msisimko aliouweka alipohadithia hadithi za ujasiri kutoka kwa kitabu cha Daniel na ushuhuda wake wa Mwokozi Bwana Yesu Kristo.

Nitakumbuka daima jinsi Bwana huwaita wenza waliochaguliwa kwa makini kwa ajili ya wenye ukuhani wake katika maandalizi.

Askofu wangu alikuwa na washauri mahiri, na kwa sababu ambayo sikuelewa wakati huo, zaidi ya mara moja aliniita kwa simu nyumbani na kusema, “Hal, nakuitaji twende nawe kama mwenza wangu kufanya matembezi kadha.” Wakati mmoja, ilikuwa ni kwenda pamoja naye kwenye nyumba ya mjane aliyekuwa anaishi peke yake na hakuwa na chakula katika nyumba. Tulipokuwa njiani kurudi alisimamisha gari, akafungua maandiko yake, na akanieleza ni kwa nini alimfanya yule mjane kama kwamba alikuwa na nguvu siyo ya kujisaidia tu awezavyo, bali pia wakati fulani katika siku za usoni angekuwa na uwezo wa kuwasaidia wengine.

Tembezi lingine lilikuwa ni kwa mwanaume ambaye alikosa kuhudhuria Kanisa kwa muda mrefu. Askofu wangu alimwalika kurudi na kuwa na watakatifu. Nilihisi upendo wa askofu wangu kwa mtu aliyeonekana kwangu kuwa asiyependeka na adui mkaidi.

Mbali na hapo kwa wakati tofauti tulitembelea nyumba ambapo wasichana wawili wadogo walitumwa kutulaki mlangoni na wazazi wao walevi. Wasichana hao wadogo walizungumza kupitia mlango wa wavu kwamba baba na mama yao walikuwa wamelala. Askofu aliendelea kuongea nao, akitabasamu na kuusifia wema wao, na ujasiri wao, kwa kile kilichoonekana kwangu kama dakika 10 na zaidi. Nilipoondoka naye nikitembea katika upande wake, alisema taratibu, “Hili lilikuwa ni tembezi zuri. Hawa watoto hawatasahau kuwa tulikuja.”

Baraka mbili ambazo mwenza wangu mkubwa anaweza kutoa ni uaminifu na mfano wa kujali. Nililiona hilo wakati mwanangu alipopewa mwenza ambaye alikuwa na ujuzi mkubwa wa kikuhani kumshinda. Mwenza mkuu wake alikuwa rais wa misheni mara mbili na alikuwa amehudumu katika sehemu mbalimbali za uongozi.

Kabla ya kuitembelea familia waliyopangiwa, kiongozi huyo wa ukuhani mwenye uzoefu aliomba kumtembelea mwanangu nyumbani kwetu kabla ya kuondoka. Wakanirusu kusikiliza. Yule mwenza mkubwa alifungua kwa sala, akiomba msaada. Baadaye alisema kitu kama hiki kwa mwanangu: “Nafikiri tufundishe somo ambalo litaweza kusikika kwa familia hii kama mwito wa toba. Nafikiri hawatauchukulia vyema kutoka kwangu. Nafikiria watachukulia ujumbe vyema zaidi kutoka kwako. Je unaonaje kuhusu hilo?

Nakumbuka hofu katika macho ya mwana wangu. Bado ninaweza kuhisi upendo wa wakati ule wakati mwanangu alivyopokea wajibu huo.

Haikuwa kwa bahati kwamba askofu aliweka ule uenzi pamoja. Ilikuwa kwa maandalizi ya makini ambayo mwenzi mkuu alikuwa amejifunza kuhusu hisia za familia hiyo ambayo wangefundisha. Ulikuwa ni mwongozo wa kiroho ambao ulimfanya arudi nyuma, kumwamini kijana asiye na uzoefu kuwaita watoto wazee wa Mungu kwenye toba na kwenye usalama.

Sikujua matokeo ya matembezi yao, lakini ninachojua ni kwamba askofu, Mwenye Ukuhani wa Melkizedeki, na Bwana, walikuwa wanamwandaa huyu kijana kuwa mwanamume wa ukuhani na siku moja askofu mwenyewe.

Sasa, hadithi kama hizi za mafanikio katika maandalizi ya ukuhani zinajulikana kwenu kwa kile mlichokiona na kile mlichopata uzoefu nacho katika maisha yenu. Mmejua na mmekuwa Maaskofu, wenza, na wazazi. Mmeuona mkono wa Bwana katika maandalizi yenu kwa ajili ya kazi za ukuhani ambazo alijua ziko mbele yenu.

Sisi sote katika ukuhani tuna jukumu la kumsaidia Bwana kuwaandaa wengine. Kuna baadhi ya vitu tunavyoweza kufanya ambavyo vinaweza kuwa na umuhimu sana. Hata vyenye nguvu zaidi ya kutumia maneno katika mafundisho ya mafunzo ambayo ni mifano yetu ya kuishi mafundisho haya.

Cha umuhimu kabisa katika huduma ya ukuhani wetu ni kuwaalika watu kuja kwa Kristo kwa imani, toba, ubatizo, na kupokea Roho Mtakatifu. Rais Thomas S. Monson, kwa mfano, ametoa mafundisho za kuchochea moyo katika mafundisho haya. Lakini ninachojua kuhusu alichowafanyia watu na wamisionari na marafiki alipokuwa akisimamia misheni ya Toronto kinanichochea kutenda

Katika maandalizi ya ukuhani, “nioneshe” ina maana kuliko“niambie”

Ndio maana maandiko ni muhimu sana katika kutuandaa katika ukuhani. Yamejaa mifano. Nahisi kama ninaweza kumwona Alma akifuata amri za malaika na baadaye akiharakisha kuzifundisha kwa waovu pale Amoniha ambao walikuwa wamemkataa.4 Ninaweza kuhisi baridi kwenye gereza wakati nabii Joseph alipoambiwa na Mungu kuwa jasiri kwamba alikuwa analindwa.5 Kwa taswira la maandiko hayo akilini tunaweza kujiandaa kuvumilia katika huduma zetu wakati zinapoonekana kuwa ngumu.

Baba au askofu au mwenza mkubwa wa mafundisho ya nyumbani anayeonyesha kwamba anamwamini kijana mdogo mwenye ukuhani inaweza kubadilisha maisha yake. Baba yangu aliwahi kuulizwa na mshiriki wa Jamii ya Wale Mitume Kumi na Wawili kuandika makala mafupi kuhusu sayansi na dini. Baba yangu alikuwa mwanasayansi mashuhuri na mwenye ukuhani mwaminifu. Lakini bado naweza kukumbuka wakati aliponipa karatasi aliyokuwa ameandika na kuniambia, “Hii hapa, kabla sijaituma kwa wale Kumi na Wawili, nataka uisome. Utajua kama iko sahihi.” Alikuwa amenizidi miaka 32, mwenye busara na akili nyingi kunizidi kwa umbali mkubwa.

Bado naimarishwa na imani hiyo kwangu kutoka kwa baba mwema na mtu wa ukuhani. Nilijua kwamba siyo kwamba imani yake haikuwa kwangu lakini kwamba Mungu angeweza na angeniambia kitu gani kilichokuwa ni cha kweli. Ninyi wenza wenye tajiriba mnaweza kuwabariki vijana wadogo wenye ukuhani katika maandalizi pale mnapowaonyesha aina hiyo ya kuwaamini. Itawasaidia kuamini hisia nzuri za kuwainua wao wenyewe wakati zinapokuja ambapo pale ataweka mikono yake kufunga baraka za kuponya mtoto ambaye madaktari wamesema atakufa. Imani hii imenisaidia zaidi ya mara moja.

Mafanikio yetu katika kuwaandaa wengine katika ukuhani yatakuja kulingana na jinsi gani tunavyowapenda. Hii itakuwa kweli hasa pale ambapo itatulazimu kuwarekebisha. Fikiria kwa dakika ambapo mwenye Ukuhani wa Haruni, labda kwenye meza ya sakramenti, anapofanya makosa katika kufanya ibada. Hili ni jambo muhimu sana. Wakati mwingine kosa linahitaji kurekebishwa mbele za watu kukiwa na uwezekano wa kusita, hisia za kushushwa hadhi na hata kukataliwa.

Utakumbuka shauri la Bwana: “Kukemea kwa ukali kwa wakati wake, utakapokuwa umeongozwa na Roho Mtakatifu; na halafu baadaye kuonyesha ongezeko la upendo kwa yule uliyemkemea, asije akakudhania wewe kuwa ni adui yake.”6

Neno ongezeko lina maana muhimu katika kuwaandaa wenye ukuhani wanapohitaji kurekebishwa. Neno linapendekeza ongezeko la upendo ambao tayari ulikuwepo. “Kuonyesha” kunahusu ongezeko. Wengine wenu ambao mnaowaandaa makuhani mtapata, kuwaona wakifanya makosa. Kabla ya yao kupokea ukosoaji wako, ni lazima walikuwa wamehisi upendo wako mapema na kwa uthabiti. Ni sharti walihisi kusifu kwako kikweli na kwa dhati kabla ya kukubali kukosolewa nawe.

Bwana Wenyewe amewachukua wale wenye ukuhani mdogo kwa heshima ambayo inatunuku uwezo wao na thamani yao kwake. Sikiliza maneno haya, yaliyosemwa na Yohana Mbatizaji wakati Ukuhani wa Haruni ulirejeshwa: “Juu yenu ninyi watumishi wenzangu, katika jina la Masiya ninawatunukia Ukuhani wa Haruni, ambao hushikilia funguo za huduma za malaika, na za injili ya toba na za ubatizo kwa uzamisho kwa ajili ya ondoleo la dhambi na hizi kamwe hazitaondolewa tena kutoka duniani, mpaka wana wa Lawi watakapotoa tena matoleo kwa Bwana katika haki.”7

Ukuhani wa Haruni ni kiambatanisho kwa ule Ukuhani mkubwa wa Melkizedeki.8 Kama rais wa makuhani wote, Rais wa Kanisa husimamia ukuhani andalizi vile vile. Ujumbe wake kwa miaka mingi wa kwenda kuwaokoa unarandana vyema kabisa na agizo la kupeleka injili ya toba na ubatizo katika maisha ya wengine.

Jamii za mashemasi, walimu, na makuhani wanashauriana mara kwa mara kuvuta kila mshiriki kwa Bwana. Urais huwapa kazi washiriki ya kuwafikia wengine katika imani na upendo. Mashemasi hupitisha sakramenti kwa unyenyekevu na kwa imani ili washiriki wahisi athari njema za Upatanisho na wawe radhi kutii amri wanapochukua nembo hizo takatifu.

Walimu na makuhani huomba na wenza wao ili kutimiza jukumu la kulilinda Kanisa, mtu mmoja hadi kwa mwingine. Na wenza hao husali pamoja wanapogundua mahitaji na matumaini ya wakuu wa familia. Wanapofanya hivyo, wanakuwa wanatayarishwa kwa ajili ya siku kuu wakati watakaposimamia kama baba kwa imani katika familia yao wenyewe.

Ninashuhudia kwamba wote wanaotumikia pamoja katika ukuhani wanawandaa watu kwa ajili ya ujio wa Bwana katika Kanisa Lake. Mungu Baba yu hai. Mimi najua---mimi najua---kwamba Yesu ndiye Kristo na kwamba anatupenda. Rais Thomas S. Monson ni Nabii wa Bwana anayeishi. Ninashuhudia hivyo katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.