2010–2019
Ulisawazishe Pito la Mguu Wako
Oktoba 2014


Ulisawazishe Pito la Mguu Wako

Tunapomwangalia Yesu kama Mfano wetu na kufuata nyayo Zake, tunaweza kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni salama.

Kina ndugu na dada zangu wapendwa, ninanyenyekezwa ninaposimama mbele yenu asubuhi hii. Ninaomba imani na maombi yenu kwa niaba yangu ninaposhiriki nanyi ujumbe wangu.

Kila mmoja wetu tulianza safari mzuri na muhimu tulipoondoka ulimwengu wa roho na kuingia hali hii ambayo mara nyingi huwa ni changamoto iitwayo maisha ya mauti. Malengo ya msingi ya uwepo wetu duniani ni kupata mwili wa nyama na mifupa, kupata uzoefu ambao ungekuja tu kupitia kutengwa kutoka kwa wazazi wetu wa mbinguni, na kuona kama tutatii amri. Katika kitabu cha Ibrahimu, mlango wa 3 , tunasoma: “Nasi tutawajaribu kwa njia hii, ili kuona kama wao watafanya mambo yote yale ambayo Bwana Mungu wao atawaamuru.”1

Tulipokuja duniani tulileta pamoja nasi karama kuu kutoka kwa Mungu---hata wakala wetu. Kwa maelfu ya njia tuna fursa ya kujichagulia wenyewe. Hapa tunajifunza kutoka kwa mahitaji magumu ya uzoefu wa kibinafsi. Tunabainisha kati ya mema na maovu. Tunatofautisha kati ya chungu na tamu. Tunajifunza kwamba maamuzi yanaamua hitimisho.

Nina uhakika tulimwacha Baba yetu tukiwa na nia kuu ya kumrudia Yeye, ili kwamba tuweze kupokea kuinuliwa Yeye aliotupangia na ambako sisi, wenyewe, tulitaka sana. Ingawa tumeachwa tupate na tufuate njia hiyo inayotuelekeza ya kumrudia Baba yetu aliye Mbinguni, hakututuma hapa bila mwelekeo na mwongozo. Badala, ametupa vifaa tunavyohitaji, na atatusaidia tunapotafuta usaidizi Wake na kujitahidi kufanya yote tuwezayo kuvumilia hadi mwisho na kupokea uzima wa milele.

Ili kusaidia kutuongoza tunayo maneno ya Mungu na ya Mwanawe yanayopatikana katika maandiko matakatifu yetu. Tunao ushauri na mafunzo ya manabii wa Mungu. Cha muhimu sana, tumepewa mfano kamili wa kufuata---hasa mfano wa Bwana na Mwokozi, Yesu Kristo---na tumeshauriwa tuufuate mfano huo. Alisema Mwokozi mwenyewe: “Njoo unifuate.”2 “vitendo ambavyo mmeniona nikifanya, hivyo pia mtafanya.”3 Aliuliza swali, “mnapaswa kuwa watu wa aina gani?” Na kisha akajibu” “Amin, nawaambia, hata vile nilivyo.”4 “Alitengeneza njia na kuongoza mbele.”5

Tunapomtazamia Yesu kama Mfano wetu na tunapofuata katika nyayo Zake, tunaweza kurudi kwa usalama kwa Baba yetu wa Mbinguni kuishi Naye milele. Alisema nabii Nefi, “Bila ya mwanadamu kuvumilia hadi mwisho, kwa kufuata mfano wa Mwana wa Mungu aliye hai, hawezi kuokolewa.”6

Mwanamke mmoja, kila wakati alisimulia yale aliyopitia wakati wa ziara kule Nchi Tukufu, angesema, “Nilitembea ambapo Yesu alitembea!”

Alikuwa katika eneo ambapo Yesu aliishi na kufundisha. Pengine alisimama kwenye jiwe ambapo Yeye aliwahi kusimama ama alitazama milima ambapo Yeye alikuwa amewahi kutazama. Matukio, yenyewe, yalimfurahisha; lakini kutembea pale alitembea Yesu si muhimu kuliko kutembea kama alivyotembea Yeye. Kuiga vitendo Vyake na kufuata mfano Wake ni muhimu zaidi kuliko kujaribu kutafuta mabaki ya nyayo zake kwenye njia alitembea duniani.

Wakati Yesu alimpa tajiri fulani mwaliko, “Njoo unifuate,”7 hakukusudia kwamba tajiri amfuate tu juu na chini kwenye milima na mabonde ya mji.

Hatufai kutembea kwenye fuo za Galilaya ama kati ya milima ya Yuda ili kutembea ambapo Yesu alitembea. Sote tunaweza kutembea njia alitembea wakati, tukikumbuka maneno Yake, roho Yake akijaza mioyo yetu, na mafundisho Yake yakiongoza maisha yetu, tunachagua kumfuata tunaposafari duniani. Mfano Wake unaonyesha njia. Akasema Yeye, “Mimi ndimi njia, na kweli na uzima.”8

Tunapochunguza njia Yesu alitembea, tutaona kwamba ilimpeleka kupitia changamoto nyingi sawa na zile sisi wenyewe tutakumbana nazo maishani.

Kwa mfano, Yesu alitembea njia ya kukata tamaa. Ingawa alipitia kukatizwa tamaa kwingi, moja iliyogusa moyo kabisa ilionyeshwa katika maombolezi Yake juu ya Yerusalemu alipokamilisha huduma Yake ya umma. Watoto wa Israeli walikuwa wamekataa usalama wa bawa la ulinzi ambao alikuwa amewatolea. Alipotazama mji uliokaribia kuachwa katika uangamizi, alijawa na hisia za huzuni kali. Kwa majonzi alilia, “Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauwaye manabii na kuwapiga kwa mawe waliotumwa kwako, mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkutaka!”9

Yesu alitembea njia ya majaribio. Lusiferi, yule muovu, akukusanya nguvu zake kuu, ujanja wake mkuu, alimjaribu Yeye ambaye alikuwa amefunga kwa siku 40 na mchana na usiku. Yesu hakukubali, bali, alipinga kila jaribio. Maneno Yake ya kuondoka: “Nenda zako Shetani.”10

Yesu alitembea njia ya uchungu. Zingatia Gethsemane, ambapo alikuwa katika “dhiki...na hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.”11 Na hakuna awezaye kusahau mateso Yake kwenye msalaba katili.

Kila mmoja wetu atatembea njia ya kukatizwa tamaa, pengine kwa sababu ya fursa iliyopotezwa, ama mamlaka yaliyotumiwa vibaya, chaguo za mpendwa, ama chaguo sisi wenyewe tunafanya. Njia ya majaribio pia itakuwa njia kila mmoja wetu atapitia. Tunasoma katika sehemu ya 29 ya Mafundisho na Maagano: “Na hapana budi kwamba ibilisi lazima awajaribu wanadamu, vinginevyo hawangeweza kujiamulia wao wenyewe.”12

Vile vile tutatembea njia ya uchungu. Sisi, kama watumishi, hatuwezi kutarajia kiwango cha chini kuliko Mwalimu, ambaye aliondoka duniani tu baada ya uchungu mwingi na mateso.

Ijapo tutapata njiani mwetu huzuni kali, tunaweza pia kupata furaha kubwa.

Sisi, pamoja na Yesu, tunaweza kutembea njia ya utiifu. Haitakuwa rahisi kila mara, lakini misemo yetu iwe urithi ambao Samweli alitupa. “Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, na kusikia kuliko mafuta ya beberu.”13 Tukumbukeni kwamba matokeo ya kutotii ni ufungwa na kifo, wakati zawadi ya utiifu ni uhuru na uzima wa milele.

Sisi, kama Yesu, tunaweza kutembea njia ya huduma. Kama mfano mkuu wa wema ni maisha ya Yesu alipohudumu miongoni mwa watu. Alileta nguvu kwa miguu ya vilema, kuona kwa macho ya vipofu, kusikia kwa viziwi.

Yesu alitembea njia ya sala. Alitufundisha jinsi ya kusali kwa kutupa sala mzuri tujuayo kama Sala ya Bwana. Na nani anaweza kusahau sala yake katika Gethsemane: “Si mapenzi yangu, bali yako yatendeke”?14

Maelekezo mengine yaliyotolewa kwetu na Mwokozi yanapatikana virahisi, yanapatikana katika maandiko matakatifu. Katika Mahubiri Yake Mlimani, anatuambia tuwe wenye huruma, tuwe wanyenyekevu, tuwe waadilifu, tuwe wenye mioyo safi, tuwe wenye kupenda amani. Anatuelekeza tusimame kwa ujasiri kwa ajili ya imani yetu, hata wakati tunadharauliwa na kuteswa. Anatuuliza tuache nuru zetu ziangaze ili wengine waweze kuziona na pengine watamani kumtukuza Baba yetu wa Mbinguni. Anatufundisha kuwa wasafi kimaadili katika mawazo yetu na matendo yetu. Anatuambia ni muhimu zaidi kuweka hazina mbinguni kuliko duniani.15

Mafumbo Yake yanafundisha kwa nguvu na mamlaka. Na hadithi ya Msamaria mwema, anatufundisha sisi kupenda na kuhudumia majirani zetu.16 Katika fumbo lake la talanta, anatufundisha kujiimarisha na kutia bidii ili kukamilika.17 Na fumbo la kondoo aliyepotea, anatufundisha kuwaokoa wale ambao wameacha njia na wamepotea.18

Tunapojitahidi kumweka Kristo kama kitovu cha maisha yetu kwa kujifunza maneno Yake, kwa kufuata mafundisho Yake, na kutembea katika njia Yake, amaahidi kushiriki nasi uzima wa milele ambayo Yeye alikufa ili kuyapata. Hakuna lengo kuu kushinda hili, kwamba tunapaswa tuchague kukubali njia Yake na kuwa wafuasi Wake na kufanya kazi Yake maishani mwetu wote. Hakuna chochote kingine, hakuna chaguo lingine tunafanya, linaweza kutufanya kile Yeye anaweza kutufanya tuwe.

Ninapofikiria kuwahusu wale ambao hakika wamejaribu kufuata mfano wa Mwokozi na ambao wametembea katika njia Yake, kunakuja kwa urahisi akilini mwangu majina ya Gustav na Margarete Wacker---wawili wa watu binafsi wa Kikristo nimewahi kujua. Walikuwa wazaliwa wa Ujerumani ambao walikuwa wamehamia Kanada mashariki, na nilikutana nao nilipohudumu kama rais wa misheni huko. Ndugu Wacker alipata ujira wake kama kinyozi. Ingawa walikuwa hawana mengi, walishiriki yote waliyokuwa nayo. Hawakubarikiwa na watoto, lakini waliwalea wote walioingia nyumbani kwao. Waume na wanawake walio na elimu na wastaarabu waliwatafuta hawa watumishi wanyenyekevu, wa Mungu wasio na elimu na walijiona wenye bahati ikiwa wangeweza kuwa katika uwepo wao kwa saa moja.

Muonekano wao ulikuwa wa kawaida, Kiingereza chao duni na kigumu kueleweka, nyumba yao wastani. Hawakuwa na gari ama televisheni, wala hawakufanya vitu vyovyote vile ambavyo dunia kwa kawaida huzingatia. Hata hivyo waaminifu waliwatembelea kila mara ili kufurahia roho iliyokuwa pale. Nyumba yao ilikuwa mbinguni duniani, na roho walioangaza ilikuwa amani safi na wema.

Sisi pia tuna hiyo roho na tunaweza kushiriki na dunia tunapotembea njia ya Mwokozi wetu na kufuata mfano Wake kamilifu.

Tunasoma katika Mithali onyo dogo, “Ulisawazishe Pito la Mguu Wako.”19 Tunapofanya hivyo, tutakuwa na imani, hata hamu, kutembea njia ambayo Yesu alitembea. Hatutakuwa na shaka kwamba tuko kwenye njia ambayo Baba yetu angetaka tufuate. Mfano wa Mwokozi unatupa mfumo kwa kila kitu tunachofanya, na maneno Yake yanatoa mwongozo dhabiti. Njia yake itatupeleka nyumbani salama. Hii iwe baraka yetu, ninaomba, katika jina la Yesu Kristo, ambaye ninampenda, ambaye ninamtumikia, na kumhusu ninashuhudia, amina.