2010–2019
Fanya Utumizi wa Imani Kuwa Kipaumbele Chako cha Kwanza
Oktoba 2014


Fanya Utumizi wa Imani Kuwa Kipaumbele Chako cha Kwanza

Licha ya changamoto zote mbaya tunazo maishani, lazima tutafute muda wa kutumia imani yetu.

Wakati Adamu na Hawa walikuwa katika Bustani ya Edeni, yote waliyohitaji kwa ajili ya kutimiza mahitaji yao ya kila siku yalitolewa kwao kwa wingi. Hawakuwa na shida, changamoto, ama uchungu. Kwa sababu hawakuwai kupitia shida, hawakujua wangeweza kuwa na furaha. Hawakuwai kuhisi zahama, basi hawangeweza kuhisi amani.

Hatimaye Adamu na Hawa walivunja amri kutokula tunda la mti wa ujuzi na wema. Kwa kufanya hivyo hawakuwa tena katika hali ya kutojua. Walianza kupitia kanuni za upinzani. Walianza kukumbana na ugonjwa uliodhohofisha afya yao. Walianza kuhisi huzuni pamoja na shangwe.

Adamu na Hawa kupitia kula tunda lililokatazwa, ufahamu wa mema na maovu ulikuja duniani. Uchaguzi wao uliwezesha kila mmoja wetu kuja duniani humu kujaribiwa na kutahiniwa.1 Tumebarikiwa na wakala ambao ni uwezo wetu wa kufanya maamuzi na kuwajibika kwa ajili ya maamuzi hayo. Anguko liliwezesha hisia za furaha na huzuni maishani mwetu. Tunaweza kuelewa amani kwa sababu tunahisi zahama.2

Baba yetu wa Mbinguni alijua haya yangetokea kwetu. Yote ilikuwa sehemu ya mpango wa furaha Wake mkamilifu. Alitayarisha njia kupitia maisha ya Mwanawe mtiifu kikamilifu, Yesu Kristo, Mwokozi wetu, kwa Upatanisho Wake kushinda kila ugumu tunaoweza kupitia duniani.

Tunaishi katika nyakati ngumu. Sihitaji kuorodhesha vyanzo vyote vya maovu duniani. Haiitajiki kueleza changamoto ziwezekanazo na huzuni mkubwa ambayo ni sehemu ya maisha duniani. Kila mmoja wetu anafahamu kwa kina juu ya mapambano yetu wenyewe na majaribu, uchungu na huzuni.

Tulifundishwa katika maisha kabla ya maisha duniani kwamba lengo letu la kuja hapa ni kutahiniwa, kujaribiwa, na kufikishwa ukingoni wa uwezo wetu.3 Tulijua tungekumbana na maovu ya adui. Wakati mwingine tunaweza kuhisi uwepo zaidi wa mambo mabaya ya maisha duniani kuliko wa mambo mazuri. Nabii Lehi alifundisha, “Kwani lazima, kuwe na upinzani katika vitu vyote.”4 Licha ya changamoto zote mbaya tulizonazo maishani, lazima tutenge muda wa kufanya imani yetu. Matumizi kama hayo hualika nguvu nzuri zilizojawa na imani ya Upatanisho wa Yesu Kristo maishani mwetu.

Baba yetu wa Mbinguni ametupa zana za kutusaidia kumjia Kristo na kufanya imani katika Upatanisho Wake. Wakati zana hizi zinapokuwa tabia za msingi, hutoa njia rahisi sana ya kupata amani katika changamoto za maisha duniani. Leo nimechagua kujadili nne kati ya zana hizi. Ninapozungumza, zingatia kupima matumizi yako ya kibinafsi ya kila zana, kisha tafuta uongozo wa Bwana kubainisha jinsi ungezitumia vyema zaidi kila moja yazo.

Sala

Zana ya kwanza ni sala. Chagua kuzungumza na Baba yako aliye Mbinguni kila mara. Chukua wakati kila siku kushiriki fikra na hisia zako Naye. Mwambie kila kitu kinachokutatiza. Anajali kuhusu zile sehemu muhimu kabisa na za kawaida za maisha yako. Shiriki Naye hisia zako zote na yale unayopitia.

Kwa sababu anaheshimu wakala wako, Baba wa Mbinguni hatawai kukulazimisha usali Kwake. Lakini unapotumia wakala huo na kumjumuisha katika kila kitengo cha maisha yako ya kila siku, moyo wako utaanza kujawa na amani ya furaha. Amani hiyo italenga nuru ya milele katika masambuko yako. Itakusaidia kukumbana na changamoto hizi kutoka kwa mtazamo wa milele.

Wazazi, saidieni kulinda watoto wenu kwa kuwapa ulinzi kila asubuhi na usiku unaokuja kutoka kwa sala ya familia. Watoto huvamiwa kila siku na maovu ya tamaa, uchoyo, kiburi na tabia zingine nyingi za dhambi. Lindeni watoto wenu kutoka kwa shawishi nyingi mbaya za kidunia kwa kuwaimarisha na baraka ya uwezo unaotokana na sala ya familia. Sala ya familia inapaswa iwe kipaumbele ambacho hakina mjadala katika maisha yako ya kila siku.

Kujifunza Maandiko

Zana ya pili ni kujifunza neno la Mungu katika maandiko na maneno ya manabii walio hai. Sisi huzungumza na Mungu kupitia sala. Yeye mara nyingi huwasiliana nasi kupitia neno lake lililoandikwa. Ili kujua kile sauti ya Uungu inavyosikika na kuhisika, soma maneno Yake, soma maandiko, na yatafakari.5 Yafanye yawe sehemu muhimu ya maisha ya kila siku. Ukitaka watoto wako watambue, waelewe, na kutendea misukumo ya Roho, lazima usome maandiko pamoja nao.

Usikubali uongo wa Shetani kwamba hauna wakati wa kujifunza maandiko. Chagua kutenga muda wa kuyasoma. Kufurahia neno la Mungu kila siku ni muhimu zaidi kuliko usingizi, shule, kazi, maonyesho ya televisheni, michezo ya video, au vyombo vya kijamii. Huenda ukahitaji kupanga upya vipaumbele vyako ili kutoa muda kwa kujifunza neno la Mungu. Kama ni hivyo, fanya hivyo!

Kuna ahadi nyingi za kinabii za baraka za kujifunza maandiko kila siku.6

Ninaongeza sauti yangu na ahadi hii: unapotenga muda kila siku, kibinafsi na pamoja na familia yako, wa kujifunza neno la Mungu, amani itakuwa katika maisha yako. Amani hiyo haitakuja kutoka duniani. Amani itakuja kutoka ndani ya nyumba yako, kutoka ndani ya familia yako, kutoka ndani ya moyo wako. Itakuwa karama ya Roho. Itaonekana iking’aa kutoka kwako na kuwashawishi wengine walio karibu nawe. Utakuwa unafanya kitu cha maana sana kuongezea kwa amani ya jumla duniani.

Sisemi kwamba maisha yako yatakosa kuwa na changamoto. Kumbuka wakati Adamu na Hawa walikuwa katika bustani, walikuwa hawana changamoto, lakini walikuwa hawawezi kupata furaha, shangwe na amani.7 Changamoto ni sehemu muhimu ya maisha duniani. Kupitia kujifunza kila siku, bila kukoma, utapata amani katika zahama inayokuzingira na nguvu kushinda majaribu. Utakuza imani ya nguvu katika neema ya Mungu na utajua kwamba kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo yote yatafanywa yawe sawa kulingana na mpangilio wa Mungu.

Jioni ya Familia Nyumbani

Unapotia bidii kuimarisha familia yako na kukuza amani, kumbuka zana hii ya tatu: jioni ya familia nyumbani kila wiki. Tahadhari usifanye jioni ya familia nyumbani kuwa jambo la kushtukia baada ya siku yenye shughuli nyingi. Amua kwamba Jumatatu usiku familia yako itakuwa nyumbani pamoja kwa jioni hiyo. Usikubali masharti ya ajira, spoti, shughuli za kando, kazi ya nyumbani, ama chochote kingine kiwe na umuhimu zaidi kuliko wakati huo unatumia pamoja nyumbani na familia yako.

Muundo wa jioni yako si muhimu kama vile muda unaoweka. Injili inapaswa kufundishwa kwa rasmi na pia isiwe rasmi. Ifanye iwe uzoefu wa maana kwa kila mwanafamilia. Jioni ya familia nyumbani ni wakati wa thamani kushuhudia katika mazingira salama; kujifunza kufundisha, kupanga, na ujuzi wa mpangilio; kuimarisha mahusiano ya familia, kukuza tamaduni za familia; kuzungumziana; na muhimu kabisa, kuwa na wakati wa ajabu pamoja!

Katika mkutano mkuu uliopita wa Aprili, Dada Linda  S. Reeves alitangaza kwa ushujaa: “Lazima nishuhudie baraka za kujifunza maandiko kila siku na sala na jioni ya familia nyumbani kila wiki. Hivi ndivyo vitendo vyenyewe ambavyo husaidia kuondoa dhiki, hutoa muongozo kwa maisha yetu, na huongeza ulinzi kwa makao yetu.”8 Dada Reeves ni mwanamke mwenye hekima sana. Ninawahimiza kwa dhati mpate ushuhuda wenu wenyewe wa desturi hizi tatu za maana.

Kuhudhuria Hekalu

Zana ya nne ni kwenda hekaluni. Sote tunajua hakuna mahali penye amani zaidi duniani kuliko katika mahekalu ya Mungu. Kama hauna sifu ya hekalu, hitimu kuipata moja sasa. Wakati ukipata sifu, itumie kila mara.9 Panga wakati kwa mfululizo kuwa katika hekalu. Usikubali yeyote ama chochote kikuzuie kuwa hapo.

Unapokuwa hekaluni, sikiliza maneno ya maagizo, yatafakari, sali kuyahusu, na tafuta kuelewa maana yake. Hekalu ni mojawapo ya mahali bora kabisa kuja kuelewa nguvu ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Mtafute Yeye huko. Kumbuka kwamba baraka nyingi zaidi huja kutokana na kupeana majina ya familia yako mwenyewe katika hekalu.

Zana hizi nne ni desturi za msingi za kulinda maisha yako katika nguvu ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Kumbuka Mwokozi wetu ndiye Mfalme wa Amani. Amani katika maisha haya duniani huja kutoka kwa dhabihu Yake ya Upatanisho. Wakati tunasali kila mara asubuhi na usiku, tunajifunza maandiko yetu kila siku, tunakuwa na jioni ya familia nyumbani kila wiki, na tunahudhuria hekalu kila mara, tunajibu aliko Lake kwa kutenda la “kuja Kwake.” Zaidi tunavyokuza tabia hizi, ndivyo zaidi Shetani anataka kutudhuru, lakini ndivyo uwezo wake wa kufanya hivyo unapunguzwa. Kupitia matumizi ya zana hizi, tunatumia wakala wetu kukubali karama kamili za dhabihu Yake ya Upatanisho.

Sipendekezi kwamba masumbuko yote ya maisha yatapotea unapofanya vitu hivi. Tulikuja katika maisha duniani hasa kukua kutokana na majaribio na mtihani. Changamoto hutusaidia kuwa kama Baba yetu aliye Mbinguni, na Upatanisho wa Yesu Kristo huwezesha kupitia changamoto hizo.10 Ninashuhudia kwamba tunapomjia kwa matendo, tunaweza kushinda kila jaribio, kila huzuni kubwa, kila changamoto tunayopitia, katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona Musa 5:11.

  2. Ona Musa 4–5.

  3. Ona Ibrahimu 3:25.

  4. 2 Nefi 2:11.

  5. Ona Mafundisho na Maagano 18:36; ona pia mistari ya 34–35.

  6. Baadhi ya mifano inajumuisha:Rais Thomas S. Monson alisema: “Tunaposoma na kutafakari maandiko, tutapata minong’onomtamu ya Roho katika nafsi zetu. Tunaweza kupata majibu ya maswali yetu. Tunajifunza kuhusu baraka ambazo huja kupitia kutii amri za Mungu. Sisi hupata ushahidi wa uhakika wa Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wetu, Yesu Kristo, na wa upendo Wao kwetu. Wakati kujifunza maandiko kunaambatanishwa na sala zetu, tunaweza kwa uhakika kujua kwamba injili ya Yesu Kristo ni ya kweli. ... Tunapokumbuka sala na kuchukua muda wa kurejelea kwa maandiko, maisha yetu yatabarikiwa zaidi heri na mizigo yetu itafanywa iwe miepesi” (“We Never Walk Alone,” Ensign auLiahona, Nov. 2013, 122).Rais Gordon  B. Hinckley: “Bila wasiwasi ninawaahidi kwamba ikiwa kila mmoja wenu atafuata mpango huu rahisi, bila kujali mara ngapi hapo awali huenda ulisoma Kitabu cha Mormoni, kuta kuja katika maisha yako na katika nyumba yako kipimo zaidi cha Roho wa Bwana, azimio la nguvu kutembea katika kutii amri Zake, na ushuhuda wa nguvu wa uhalisi wa uhai wa Mwana wa Mungu” (“A Testimony Vibrant and True,” Ensign orLiahona, Aug. 2005, 6).Rais Howard  W. Hunter alisema: “Familia hubarikiwa sana wakati kina baba na mama wenye hekima huwaleta watoto wao kando yaokusoma kutoka kwa kurasa za maandiko pamoja, na kisha wanajadili wazi hadithi nzuri na fikira kulingana na ufahamu wa kila mmoja. Mara nyingi vijana na watoto huwa na mtazamio mwema na shukrani kwa ajili ya fasihi ya msingi ya dini” (“Reading the Scriptures,” Ensign, Nov. 1979, 64).Rais Ezra Taft Benson alisema: “Mara nyingi sisi hutumia juhudi nyingi katika kujaribu kuongeza kiwango cha ushiriki katika vigingi vyetu. Sisi hutia bidii ili kuinua asilimia ya wale wanaohudhuria mikutano ya sakramenti. Sisi hufanya kazi kupata asilimia ya juu ya wavulana wetu kwenda misheni. Sisi hutia bidii kuboresha idadi ya wale wanaooa hekaluni. Hizi zote ni jitihada za kupongezwa na muhimu katika ukuaji wa ufalme. Lakini wakati washiriki binafsi na familia zinajitumbukiza zenyewe katika maandiko kila mara na kwa ustadi, sehemu hizi zingine za ushiriki zitakuja moja kwa moja. Shuhuda zitaongezeka. Kujitolea kutaimarishwa. Familia zitahimiliwa. Ufunuo wa kibinafsi utakuja” (“The Power of the Word,” Ensign, May 1986, 81).Rais Spencer  W. Kimball alisema: “Mimi hupata kwamba wakati ninachukulia kuwa kawaida mahusiano yangu na uungu na wakati inaonekana kwamba hakuna sikio la uungu linasikiliza na hakuna sauti ya uungu inazungumza, kwamba niko mbali, mbali sana. Nikijitumbukiza mwenyewe katika maandiko umbali hupungua na roho hurudi. Mimi hujipata nikiwapenda zaidi wale ambao lazima niwapende na moyo wangu wote na akili na nguvu, na nikiwapenda zaidi, Mimi hupata kuwa rahisi kuishi kulingana na ushauri wao. ”

    (Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball [2006], 67).Rais Marion  G. Romney alisema: “Ninauhakika kwamba ikiwa, katika nyumba zetu, wazazi watasoma kutoka kwa Kitabu cha Mormoni kwa maombi na kila mara, wenyewe na pia pamoja na watoto wao, roho ya kitabu hicho kikuu itajaza nyumba zetu na wote wanaoishi humo. Roho ya kumcha Mungu itaongezeka, kuheshimiana na kuzingatia kwa ajili ya kila mmoja kutakua. Roho ya ubishi itaondoka. Wazazi watawashauri watoto wao kwa upendo na hekima zaidi. Watoto watakuwa wasikivu na watiifu zaidi kwa ushauri wa wazazi wao. Wema utaongezeka. Imani, tumaini na hisani---upendo safi wa Kristoutakuwa kwa wingi katika nyumba zetu na maisha yetu, ikileta amani, shangwe, na furaha” (“The Book of Mormon,” Ensign, May 1980, 67).Rais Boyd  K. Packer alisema: “Mafundisho ya kweli, yakifahamiwa, hubadilisha mitazamo na tabia. Kujifunza kwa mafundisho ya injili kutaboresha tabia haraka zaidi kuliko kujifunza tabia kutaboresha tabia” (“Do Not Fear,”Ensign orLiahona, May 2004, 79).Mzee David  A. Bednar alisema: “Kila sala ya familia, kila sehemu ya kujifunza kwa familia maandiko, na kila jioni ya familia nyumbani ni alama kwenye turubai wa roho zetu. Hakuna tukio moja linaloweza kuonekana kuwa la kuvutia sana amala kukumbukwa. Lakini tu kama vile alama zarangi ya njano na dhahabu na zambarau zinasaidia kila mmoja na kuzalisha kito ya kuvutia, hivyo pia msimamo wetu kwa kufanya mambo madogo unaweza kusababisha matokeo muhimu ya kiroho” (“More Diligent and Concerned at Home,”Ensignor Liahona, Nov. 2009, 19–20).

  7. Ona 2 Nefi 2:13.

  8. Linda S. Reeves, “Protection from Pornography—a Christ-Focused Home,” Ensign orLiahona, May 2014, 16–17.

  9. Rais Howard  W. Hunter alisema: “Katika roho hiyo ninawaalika Watakatifu wa Siku za Mwisho kutengemea hekalu la Bwana kama ishara kubwa ya ushiriki wao. Ni shauku ya ndani kabisa ya moyo wangu kuwa na kila mshiriki wa Kanisa anastahili kuingia hekaluni. Itamfurahisha Bwana kama kila mshiriki mtu mzima atastahili---na kubeba---sifu ya hekalu. Mambo ambayo tunapaswa tufanye na tusifanyeili kustahili sifu ya hekalu ni mambo yale yale yanayohakikisha tutakuwa na furaha kama watu binafsi na kama familia. Tuweni watu wanaohudhuria hekalu. Huhudhurieni hekalu mara nyingi kama vile hali ya kibinafsi inaruhusu. Weka picha ya hekalu katika nyumba yako ili kwamba watoto wenu waione. Wafundishe kuhusu madhumuni ya nyumba ya Bwana. Wafanye wapange kutoka miaka yao ya mapema kwenda huko na kubaki kuwa wanastahili kwa baraka hiyo” (“Exceeding Great and Precious Promises,” Ensign, Nov. 1994, 8).

  10. Ona 2 Nefi 2:2.