2010–2019
Uzima wa milele---Kumjua Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe, Yesu Kristo
Oktoba 2014


Uzima wa milele---Kumjua Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe, Yesu Kristo

Mungu na Kristo kihalisi ni Baba na Mwana---walio tofauti, dhahiri, binafsi ambao wameungalishwa katika dhamira Yao

Miaka mingi iliyopita nilichukua nafasi ya kujifunza shuhuda za mwisho za manabii katika kila kipindi. Kila mmoja alitoa ushahidi wa nguvu wa Mungu Baba na Mwanawe, Yesu Kristo.

Ninaposoma hizi shuhuda---na zinginezo nyingi kama hizo katika miaka mingi---daima zimegusa moyo wangu kujua jinsi Baba wa Mbinguni anavyompenda Mwanawe mkubwa na jinsi Yesu anavyoonyesha upendo Wake kwa utiifu kwa mapenzi ya Baba Yake. Nashuhudia kwamba tunapofanya kile kinachohitajika kuwajua Wao na kujua upendo Wao kwa mmoja na mwingine, tutapata “kilicho kikuu kati ya vipawa vyote vya Mungu”---hata uzima wa milele. 1 Kwani “uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.”2

Je! Kipawa hiki kinaweza kuwa chetu vipi? Kinakuja kupitia njia ya ufunuo wa kibinafsi, ambayo imesemwa juu yake na kuwafunza asubuhi hii.

Je! Unakumbuka mara ya kwanza ulipojua kulikuwa na Mungu na kuweza kuhisi upendo Wake? Kama mvulana, nilikuwa nikitazama anga yenye nyota nyingi na kutafakari na kuhisi uwepo Wake. Nilifurahia kuvumbua urembo mkuu wa uumbaji wa Mungu---kutoka vijidudu hadi miti mikubwa. Nilipotambua urembo wa ulimwengu huu, nilijua kwamba Baba wa Mbinguni anatupenda. Nilijua kwamba mimi nilikuwa mtoto wake wa kiroho kihalisi, kwamba sisi sote tu wana na mabinti wa Mungu.

Nilijua haya vipi? Unaweza kuuliza. Maandiko yanafunza, “Kwa wengine inatolewa na Roho Mtakatifu kujua kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu, na … kwa wengine imetolewa kuamini juu ya maneno yao, ili hao pia waweze kuwa na uzima wa milele kama wataendelea kuwa waaminifu.”3 Kutoka kwa mtazamo wangu, hii haimaanishi kwamba watu fulani watategemea shuhuda za wengine milele.

Ushuhuda wangu alikua nilipojifunza kuhusu Baba wa Mbinguni na Mwokozi kutoka ufundishaji na ushuhuda wa wazazi wangu, walimu, maandiko, ---ambayo niliyasoma kwa bidii----na hasa Roho Mtakatifu. Nilipofanya imani na kutii amri, Roho Mtakatifu alishuhudia kwamba kile nilichokuwa nikijifunza ni cha kweli. Hivyo ndivyo nilikuja kujijulia mwenyewe.

Katika mchakato huu, kutafuta ufunuo wa kibinafsi ndiyo funguo. Nefi anamwalika kila mmoja wetu: “shiriki maneno ya Kristo; kwani tazama maneno ya Kristo yatawaelezea vitu vyote mnavyostahili kutenda.”4

Kabla ya siku ya kuzaliwa yangu ya mwaka wa nane, nilitafuta kujua zaidi kuhusu ubatizo. Nilisoma maandiko na kusali. Nilijifunza kwamba ninaweza kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu nitakapothibitishwa. Pia nilianza kuelewa kwamba Mungu na Kristo ni halisi Baba na Mwana---ni viumbe tofauti, dhahiri, binafsi ambao wameungana kabisa katika madhumuni Yao. “Twawapenda [Wao], kwa sababu [Wao] kwanza walitupenda sisi.”5 Tena na tena nimeona jinsi wanavyopendana mmoja na mwingine na wanavyofanya kazi pamoja kwa wema wetu. Sikiliza machache ya maandiko mengi yanayofunza ukweli huu:

Akifundisha kuhusu maisha yetu kabla kuzaliwa, Baba wa Mbinguni alimtaja Yesu Kristo kama “Mwanangu Mpendwa, ambaye alikuwa Mpendwa na Mteule tangu mwanzo.”6 Wakati Baba aliumba ulimwengu, Yeye alifanya hivyo “kwa njia ya Mwanangu wa Pekee.7

Mama yake Yesu, Mariamu, aliambiwa angemzaa “Mwana wa Aliye Juu.”8 Na wakati Yesu alipokuwa kijana, alimwambia mama Yake kwamba Yeye “lazima inapasa kuwa katika kazi ya Baba [Yake].”9 Miaka baadaye, wakati Mwokozi alipobatizwa, Baba wa Mbinguni alizungumza kutoka mbinguni, akisema, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.”10

Kuwafunza wanafunzi Wake kusali, Yesu alisema maneno haya:

“Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe,

“Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.”11

Yeye alimfunza Nikodemo, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee.”12 Na akaelezea miujiza Yake kwa kusema, “Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona [Baba] analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.”13

Saa la Upatanisho lilipokaribia, Yesu alisali, akisema: “Baba, saa imekwisha kufika. … Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.”14 Kisha, mzigo wa dhambi zetu ulipomwangukia, Yeye alisihi, “Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.”15 Katika dakika Zake za mwisho kwenye msalaba, Yesu aliomba, “Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo” na kisha akatoa sauti. “Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.”16

Kisha Yeye akatembelea roho za wale ambao walikuwa wamekufa, katika ulimwengu wa Roho, ili “kuzipa uwezo wa kutoka, baada ya ufufuko wake kutoka kwa wafu, ili kuingia katika ufalme wa Baba yake.”17 Baada ya Ufufuko wa Mwokozi, alimtokea Mariamu Magdalene, akisema, “Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu.”18

Alipokuja kwa watu kwenye bara la Amerika, Baba Yake alimjulishana akisema, “Tazama Mwana wangu Mpendwa ninayependezwa na yeye, ambaye ndani yake nimetukuza jina langu.”19 Wakati Yesu alishuka miongoni mwa watu katika hekalu Yeye alijitambulisha Mwenyewe akisema: “Tazama, Mimi ni Yesu Kristo. … nimemtukuza Bwana kwa kujivika dhambi za ulimwengu.”20 Alipokuwa akifunza fundisho Lake, alielezea:

“Ni mafundisho ambayo Baba amenipatia; na ninashuhudia mwenyewe kwa Baba, na Baba anashuhudia mwenyewe kwangu.”21

“Kwani … Baba na Mimi tuna umoja.”22

Je! Tunaweza kuona utaratibu katika maandiko haya ambao unashuhudia juu ya Baba na Mwana kama viumbe dhahiri, na binafsi? Kivipi, basi Wao mmoja? Siyo kwa sababu Wao ni mtu mmoja bali kwa sababu Wao wameungana katika madhumuni, bidii sawa “kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu.”23

Yesu ni Mungu, hali Yeye anaendelea kujitofautisha Mwenyewe kama kiumbe tofauti, binafsi kwa kusali kwa Baba Yake na kwa kusema kwamba Yeye anafanya Mapenzi ya Baba Yake. Wakati wa huduma Yake miongoni mwa Wanefi, Yeye alisihi, “Baba siombei dunia, lakini wale ambao umenipatia kutoka duniani, … kwamba niwe ndani yao vile wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, ili tuwe kitu kimoja, kwamba nipate kutukuzwa ndani yao.”24

Tukiwa na haya akilini, haitushangazi kwamba Urejesho wa injili ulianza na kutokea si kwa kiumbe kimoja bali viumbe viwili vitukufu. Juu ya Ono la Kwanza, Nabii Joseph Smith alishuhudia, “Mmoja wao akaniambia, akiniita mimi kwa jina na kusema, huku akimwonyesha yule mwingine —— Huyu ni Mwanangu Mpendwa. Msikilize Yeye,”!25

Nabii kijana, ambaye alienda katika kichaka kujua ni kanisa gani anapaswa kujiunga nalo, alikwenda kwa imani isiyotingika, na akatoka nje na elimu na ushahidi wa Mungu wa Pekee wa kweli na Yesu Kristo, ambaye Mungu alimtuma. Joseph, kama manabii waliomtangulia, alikuwa basi chombo cha kurejesha kwenye dunia elimu ambayo inaelekeza kwenye uzima wa milele.

Ninyi pia mnaweza kumtafuta Baba yetu wa Mbinguni na “Huyu Yesu ambaye manabii na mitume [wameshuhudia]”26 katika maandiko na katika huu mkutano mkuu. Unapotafuta, ushahidi wa kibinafsi---ufunuo wako wa kibinafsi--- utagundua kwamba Baba wa Mbinguni amepatiana njia maalum kwenu ya kujijulia ukweli wenyewe; kupitia mshiriki wa tatu wa Uungu, mtu wa roho tunayemjua kama Roho Mtakatifu.

“Na mtakapopokea vitu hivi,” ikijumuisha kile ninachoshiriki leo— “ningewashauri kwamba mngemwuliza Mungu, Baba wa Milele, katika jina la Kristo, ikiwa vitu hivi si vya kweli; na ikiwa mtauliza na moyo wa kweli, na kusudi halisi, mkiwa na imani katika Kristo, atawaonyesha ukweli wake kwenu, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu mtajua ukweli wa vitu vyote.”27

Kina ndugu na kina dada, Mimi nashuhudia kwamba Baba yetu wa Mbinguni anatutaka sisi tufafute elimu sasa. Maneno ya nabii Helamani yanalia kutoka mavumbini: “Kumbukeni, kumbukeni kwamba ni juu ya mwamba wa Mkombozi wetu, ambaye ni Kristo, Mwana wa Mungu, kwamba lazima mjenge msingi wenu … , msingi ambako watu wote wakijenga hawataanguka.”28 Hakika, hatutaanguka.

Huo msingi thabiti ni Yesu Kristo. Yeye ndiye “Mwamba wa Mbinguni.”29 Tunapojenga nyumba yetu juu Yake, mvua za siku za mwisho zinaweza kunyesha, gharika ikaja, na dhoruba zikavuma, lakini hatutaanguka. Hatutaanguka kwani nyumba zetu na familia zetu zimeundwa juu ya Kristo.30

Nashuhudia kwamba nyumba kama hiyo ni “nyumba ya utukufu.”31 Hapo tunaweza kukusanyika pamoja kusali kwa Baba yetu wa Mbinguni katika jina la Yesu Kristo, Mwanawe Mpendwa. Hapo tunaweza kuwatukuza na kuwashukuru Wao. Hapo tunaweza kupokea Roho Mtakatifu na “ahadi ambayo [Yeye hutoa] [kwetu] ya uzima wa milele, hata utukufu wa ufalme wa selestia.”32

Mimi natoa ushahidi wangu maalum kwamba Mwokozi wetu, Yesu Kristo yu Hai. Baba yetu wa Mbinguni wa Milele anatupenda na anatutunza, kwamba tuna nabii katika kipindi hiki---Rais Thomas S. Monson---kutuongoza na kutuelekeza. Roho Mtakatifu hushuhudia kwamba haya ni kweli kwa kila mmoja ambaye anaendenda na kutafuta elimu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.