2010–2019
Kuwaidhinisha Maafisa wa Kanisa
Oktoba 2014


Kuwaidhinisha Maafisa wa Kanisa

Inapendekezwa kwamba tumuidhinishe Thomas S. Monson kama nabii, muonaji na mfunuaji na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho; Henry Bennion Eyring kama Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza; na Dieter Friedrich Uchtdorf kama Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza.

Wale wanaounga mkono waonyeshe.

Wale wanaopinga, kama kunao, wanaweza kuonyesha.

Inapendekezwa kwamba tumuidhinishe Boyd Kenneth Packer kama Rais wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili na wafuatao kama washiriki wa jamii hiyo: Boyd  K. Packer. L.  Tom Perry, Russell  M. Nelson, Dallin H. Oaks, M.  Russell Ballard, Richard G. Scott, Robert  D. Hales, Jeffrey  R. Holland, David  A. Bednar, Quentin  L. Cook, D.  Todd Christofferson, na Neil  L. Andersen.

Wale wanaounga mkono, tafadhali onyesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha.

Inapendekzwa kwamba tuwaidhinishe washauri katika Urais wa Kwanza na wale Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji, na wafunuaji.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onyesheni.

Kinyume, kama kuna yeyote, kwa ishara hiyo hiyo.

Inapendekezwa kwamba tuwaachilie kwa shukrani kwa ajili ya huduma yao ya kuheshimika Mzee Carlos  H. Amado na William  R. Walker kama washiriki wa Jamii ya Kwanza ya Sabini na kuwateua kama Viongozi wenye Mamlaka waliosaafu na kubaki na heshima.

Wale ambao wangependa kujiunga nasi katika kuonyesha shukrani zetu kwa huduma yao ya kujitolea, tafadhali onyesheni.

Wazee Arayik  V. Minasyan na Cvido Senkans wameachiliwa kama Sabini wa Eneo. Inapendekezwa kwamba tuwape kura ya shukrani kwa huduma yao.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onyesheni.

Inapendekezwa kwamba tuwaidhinishe wale Viongozi wenye Mamlaka wengine, Sabini wa Eneo, na urais wa makundi saidizi kama ilivyo kwa sasa.

Wale wanaounga mkono, tafadhali onyesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha.

Asanteni, kina ndugu na kina dada, kwa uaminifu na maombi yenu kwa niaba yetu.