2010–2019
Chagua kwa Hekima
Oktoba 2014


Chagua kwa Hekima

“Kuyakataa mabaya na kuyachagua mema” (Isaya 7:15).

Ndugu zangu wapendwa, hamu yangu jioni ya leo ni kushiriki baadhi ya ushauri kuhusu maamuzi na chaguo.

Nilipokuwa mwanasheria kijana katika eneo la San Francisco Bay, Kampuni yetu ilifanya baadhi ya kazi za kisheria za kampuni ambayo ilitayarisha kipindi cha Charlie Brown holiday TV specials.1 Nikawa shabiki wa Charles Schulz na ubunifu wake---Peanuts, pamoja na Charlie Brown, Lucy, Snoopy, na wahusika wengine wa ajabu.

Mojawapo ya vibonzo nilivyovienzi vilihusisha Lucy. Kama ninavyokumbuka, timu ya Charlie Brown ya besiboli ilikuwa katika mchezo muhimu sana---Lucy alikuwa anacheza uwanjani kulia, na mpira wa juu ulipigwa kwake, mchezo ulikuwa umekaribia kuwagekia, na ulikuwa ni mpigo wa tisa na mwisho wa mchezo. Ikiwa Lucy angeunyaka mpira, timu yake ingeshinda. Kama Lucy angeangusha mpira, ile timu nyingine ingeshinda.

Kama inavyoweza tu kutendeka katika vibonzo, timu yote ilimzunguka Lucy mpira ulipokuwa unakuja chini. Lucy alikuwa anafikiria, “Kama nikinyaka mpira, nitakuwa shujaa; kama sitaunyaka, nitakuwa bene.”

Mpira ukashuka chini, na wanatimu yake wakitazama kwa hamu, Lucy akaangusha mpira. Charlie Brown akatupa chini glovu zake kwa hasira. Lucy kisha akawatazama wanatimu wake, akajishika kiuno, na kusema, “Ninyi mnanitarajia mimi nishike mpira wakati mimi nina wasi wasi kuhusu sera za nchi za uhusiano wa mambo ya kigeni.

Huu ulikuwa ni mmoja kati ya mipira mingi Lucy ambayo aliangusha chini kwenye miaka mingi, na alikuwa na kisingizio kipya kila wakati. 2 Huku daima ilikuwa mizengwe, visingizio vya Lucy vilikuwa urazini; vilikuwa si sababu za kweli za kushindwa kwake kunyaka mpira.

Katika wakati wa huduma ya Rais Thomas  S. Monson, yeye kila mara amefundisha kwamba uamuzi huthibitisha kudura.3 Katika roho hiyo ushauri wangu jioni ya leo ni kuondoka kwenye urazini wowote ambao unatuzuia kufanya maamuzi mema, hasa kuhusu kumtumikia Yesu Kristo. Katika Isaya tunafunzwa, sharti “tuyakatae mabaya, kuyachgua mema.”4

Naamini ni muhimu sana katika siku yetu, ambapo Shetani anawaka sana katika mioyo ya watu katika njia nyingi mpya na zilizofichika sana, kwamba chaguo na maamuzi yetu yafanywe kwa makini, kulingana na malengo na shabaha ambazo sisi tunakiri kuishi. Tunahitaji sharti lisiwe la kugeuzwa kwa amri na kwa nidhamu kali kushikilia maagano matakatifu. Tunaporuhusu urazini kutuzuia kutokana na endaumenti za hekalu, misheni inayostahiki, na ndoa ya hekaluni, unadhuru hasa. Inavunja moyo sana tunapokiri imani katika malengo haya, pasipo kutelekeza tabia zinazohitajika kuyafikia.5

Baadhi ya vijana wanakiri malengo yao ni kuoana katika hekalu lakini hawafanyi miadi na watu ambao ni wastahiki wa hekalu. Kuwa wazi kabisa, baadhi hata hawafanyi miadi kamwe, kabisa! Ninyi wasaje wanaume, mradi mnavyobakia waseja, baada ya umri unaofaa na kukomaa, ndivyo mnavyoridhika mnaweza kuwa na hali hiyo. Lakini kadiri mnavyopaswa kujihisi kusumbuka ! Tafadhali jihusisheni”6 kwa ari katika mambo ya kiroho na shughuli za kijamii zinazoambatana na malengo yenu ya ndoa ya hekalu.

Baadhi mnahairisha ndoa mpaka elimu imemalizwa na ajira kupatikana. Ingawa inakubalika sana ulimwenguni, wazo hili halionyeshi imani, haliambatani na ushauri wa manabii wa kisasa, na haiambatani na fundisho sahihi.

Hivi majuzi nilikutana na kijana mzuri. Malengo yake yalikuwa nikwenda misheni, na kupata elimu, kuoa katika hekalu, na kuwa na familia aminifu yenye furaha. Nilipendezwa sana na malengo yake. Lakini wakati wa mazungumzo zaidi, ilikuwa wazi kwamba tabia yake na chaguo alizokuwa anafanya hazikuwiana na malengo yake. Nilihisi kuwa kwa kweli yeye alikuwa anataka kwenda misheni na alikuwa anaepukana na dhambi nzito ambazo zingemzuia kuhudumu katika misheni, lakini tabia yake ya siku hadi siku haikuwa inamtayarisha yeye kwa changamoto za kimwili, kimhemko, kijamii, kimafikira, na kiroho ambazo angekumbana nazo.7 hakuwa amejifunza kufanya kazi kwa bidii. Hakuwa anatiabidii shuleni au kwenye seminari. Alihudhuria kanisa, lakini hakuwa anasoma Kitabu cha Mormoni. Alikuwa anatumia wakati wake mwingi kwenye michezo ya video na mtandao wa kijamii. Alionekana kufikiria kwamba kufika kwenye misheni yake ingetosha. Wavulana, tafadhali jitoleeni upya kuwa na tabia ya kustahili na matayarisho ya kweli kuwa wajumbe wa Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo.

Wasiwasi wangu siyo tu kuhusu maamuzi makubwa sana bali pia maamuzi madogo madogo---maisha ya kila siku na maamuzi yanayoonekana kama ya kawaida ambapo tunatumia wakati wetu mwingi. Katika maeneo haya, tunahitaji kusisitiza kiasi, wastani na hasa hekima. Ni muhimu kuondoka kutoka kwa urazini na kufanya chaguo zilizo bora zaidi.

Mfano wa ajabu wa haja ya kuwa na kiasi, wastani, na hekima ni matumizi ya Intaneti. Inaweza kutumika kufanya kazi ya kufikia ya umisionari, kusaidia katika majukumu ya ukuhani, kuwatafuta wahenga wenye thamani kwa maagizo matakatifu ya hekalu, na mengine mengi. Uwezakano wa wema ni mpana sana. Tunajua pia kwamba inaweza kupisha mengi ambayo ni uovu, ikijumuisha picha za ngono, ukatili wa dijitali,8 na mazao yasiyojulikana. Pia inaweza kukuza upumbavu. Kama vile Ndugu Randall L. Ridd alivyofunza kwa nguvu sana katika mkutano mkuu uliopita, akiongea juu ya Intaneti, “Unaweza kushikwa katika vitanzi visivyo na mwisho vya kipuuzi ambavyo vinapoteza muda wako na kushusha uwezo wako.”9

Vishawishi na upinzani dhidi ya wema havipo tu kwenye Intaneti, vipo kila mahali. Haiwadhuru vijana tu bali sisi sote. Tunaishi katika ulimwengu ambamo kihalisi upo katika vurugu.10Tunazungukwa na maonyesho yanayonasa ya “burudani na michezo” na maisha ya uovu na uozo. Haya yanawasilishwa kama tabia ya kawaida katika vyombo ya habari vingi.

Mzee David  A. Bednar majuzi aliwaonya washiriki wawe halisi katika matumizi ya vyombo vya kijamii.11 Kiongozi maarufu kimawazo, Arthur  C. Brooks, amesisitiza jambo hili. Anasema kwamba tunapotumia vyombo vya kijamii, tunapenda kutangaza utondoti wa maisha wenye furaha lakini siyo wa nyakati ngumu shuleni. Tunatoa picha ya maisha yasiyo kamili---wakati mwengine katika njia ya majisifu au ghusi. Tunashiriki maisha haya, na kisha tunatumia “maisha ghusi ya marafiki zetu wa vyombo vya kijamii.” Brooks anatamka, “Je! Inawezaje usihisi vibaya kutumia sehemu ya muda wako ukijifanya kuwa una furaha sana kuliko ulivyo, ile sehemu ingine ya muda wako ukiona jinsi wengine wana furaha sana kukushinda?”12

Wakati mwengine inaonekana kama tunazama ndani ya upumbavu usio na maana, makelele ya upuuzi, na mabishano yanayoendelea. Tunapozima kelele hizi na kukagua hali halisi, kuna kidogo sana ambacho kitatusaidia utafutaji wa milele wetu wa malengo mema. Baba mmoja kwa hekima alijibu watoto wake wenye maombi yao mengi ya kushiriki katika vishawishi hivi. Yeye kwa urahisi kuwauliza, “Je! Hii itakufanya wewe kuwa mtu bora?”

Tunapofanya urazini wa chaguo mbaya, kubwa au ndogo, ambazo haziambatani na injili rejesho, tunapoteza baraka na ulinzi tunaohitaji na mara nyingi tunategwa katika dhambi au kwa urahisi tunapotea njia.

Mimi nina wasi wasi hasa kuhusu upumbavu13 na kushikamana na “kila kitu kipya.” Katika Kanisa tunahimiza na kusherekea kweli na elimu ya kila aina. Lakini wakati tamaduni, elimu, na tabia za kijamii vinatengwa kutoka kwa mpango wa furaha wa Mungu, wajibu muhimu wa Yesu Kristo, kuna uvunjikaji wa jamii. 14 Katika siku yetu, licha ya maendeleo katika nyanja nyingi zisizo na kifani, hasa sayansi na mawasiliano, viwango vya msingi vinamomonyoka na furaha yote na hali njema kufifia.

Wakati Mtume Paulo alipoalikwa kuhutubia katika Mars Hill katika Athene, alipata baadhi ya kujikweza kielimu huko na kukosekana kwa hekima ya kweli inayopatikana siku ya leo. 15 Katika Matendo ya Mitume tunasoma taarifa hii: “Kwa maana Waathene na wageni waliokaa huko walikuwa hawana nafasi kwa neno lo lote ila kutoa habari na kusikiliza habari za jambo jipya.” 16 Msisitizo wa Paulo ulikuwa ni Ufufuko wa Yesu Kristo. Wakati umati ulitambua uhalisi wa kidini wa ujumbe wake, baadhi walimkejeli, wengine wakampuuza wakisema, “Tutakusikiliza tena katika habari hiyo.”17 Paulo aliondoka Athene bila mafanikio yoyote. Dean Frederic Farrar aliandika juu ya safari hii: “Huko Athene hakupata Kanisa, na kwa Athene hakuandika waraka, na katika Athene, mara alipopita katika mitaa yake, kamwe hakukanya tena.”18

Naamini ujumbe wenye maongozi wa Mzee Dallin  H. Oaks ukibainisha kati ya “zuri, zuri sana, bora” unatoa njia bora ya kutathimini chaguo na vipaumbele.19 Chaguo nyingi si ovu kwa kawaida, bali kama zinachukua muda wetu mwingi na kutuzuia kutokana na chaguo bora, basi zinakuwa hatari.

Hata kila juhudi bora inahitaji utathimini ili kutambua kama inakuwa kichaganishi kuondoa malengo bora. Nilikuwa na mazungumzo ya kufana na baba yangu nilipokuwa kijana. Yeye hakuamini ya kutosha kuwa vijana walikuwa makini sana juu ya au matayarisho kwa malengo muhimu ya muda mrefu---kama vile ajira na kukimu familia.

Kujifunza kwa maana na uzoefu wa kazi ya matayarisho daima vilikuwa kwanza katika vipaumbele alivyopendekeza. Alitambua kwamba shughuli za ziada kama vile mdahalo na serikali ya wanafunzi vinaweza kuwa na muunganisho wa moja kwa moja na baadhi ya malengo yangu muhimu, Hakuwa na uhakika kuhusu muda mwingi niliotumia kushiriki katika mpira, mpira kikapu, besiboli, na mbio. Alikubali kwamba michezo ya riadha ingeweza kujenga nguvu, ustahimilifu, na umoja kazini bali alisisitiza kwamba labda kuzingatia mchezo mmoja kwa muda mfupi ingekuwa bora. Katika mtazamo wake, michezo ilikuwa mizuri lakini haikuwa bora kwangu. Alikuwa na hofu kwamba baadhi ya michezo ilikuwa kuhusu kujenga umashuhuri au sifa badala ya malengo muhimu sana ya muda mrefu.

Kwa sababu ya historia hii, moja ya sababu mimi napenda tukio la Lucy la kucheza besiboli ni kwamba katika mtazamo wa baba yangu, ningepaswa kuwa nilikuwa ninajifunza sera za mambo ya na si kujihusika kama nitanyaka mpira. Wacha niseme wazi kwamba mama yangu alikuwa anapenda michezo. Ingebidi yeyekuwa mgonjwa ndio akose michezo yangu.

Nilikuwa nimeamua kufuata ushauri wa baba yangu na sikucheza michezo ya mashindano ya chuoni. Basi kocha wa timu ya mpira ya shule yangu ya upili aliniambia kwamba kocha wa mpira wa Stanford alikuwa anataka tukutane kwa chakula na mchana pamoja na Merlin Olsen nami. Wale ambao ni wa umri mdogo mnaweza msimjue Merlin. Alikuwa mpambanaji wa ajabu wa Amerika yote kwenye timu ya mpira ya Logan High School pale ambapo mimi nilicheza kama beki kiungo, na nilinyaka mpira ya na kuweka kwenye goli salama. Katika shule ya upili Merlin alisailiwa na timu maarufu sana kote nchini. Chuoni alinyakua tuzo la Outland Trophy kama mtu wa mstarini bora katika taifa. Merlin hatimaye alikuwa wa tatu kuchaguliwa katika National Football League na alicheza kwa ustadi katika misimu 14 ya Pro Bowls. Aliteuliwa kuwa mchezaji wa Pro Football Hall of Fame katika mwaka wa 1982.20

Chakula cha mchana na kocha wa Stanford kilikuwa katika mkahawa wa Bluebird katika Logan, Utah. Baada ya salamu za mikono, yeye kamwe hakunitazama mimi macho kwa macho. Alizungumza moja kwa moja na Merlin na hakuzungumza nami. Na mwisho wa chakula, kwa mara ya kwanza, aligeuka kwangu lakini angeweza kukumbuka jina langu. Kisha akamtaarifu Merlin, “Kama ukichagua Stanford na unataka kuja na rafiki yako, yeye ana gredi nzuri ya kutosha na inawezakana kufanya mipango. Uzoefu huu ulithibitisha kwangu kwamba nilipaswa kufuata ushauri wa busara wa baba yangu.

Nia yangu si kuvunja moyo kushiriki katika michezo au kutumia Intaneti au shughuli za kustahili wanazofurahia vijana. Hizi ni aina ya shughuli ambazo zinahitaji kiasi. Wastani, na hekima. Ikiwa zitatumika kwa hekima, zinarutubisha maisha yetu.

Hata hivyo, ninamhamasisha kila mtu, vijana na wazee, kurejelea malengo na shabaha zake na kujitahidi kufanya nidhamu ya hali ya juu sana. Katika tabia na chaguo zetu za kila siku tunapaswa kuzingatia malengo yetu. Tunahitaji kuinuka juu ya urazini na vichanganishi. Ni muhimu hasa kufanya chaguo zinazoambatana na maagano yetu ya kumtumikia Yesu Kristo kwa wema.21 Kamwe tusiondoe macho yetu kwenye mpira au kuuangusha mpira huo kwa sababu yoyote.

Maisha haya ni wakati wa kujitayarisha kukutana na Mungu.22 Sisi ni watu wa furaha, wenye shangwe. Tunakubali ucheshi mzuri na tunathamini muda usiopangiliwa na marafiki na familia. Lakini tunahitaji kutambua kwamba kuna uzito wa madhumuni ambayo sharti yawe msingi wa maisha na chaguo zetu zote. Vichanganishi na urazini ambao unazuia maendeleo unaathiri sana, lakini wakati unadidimiza imani yetu katika Yesu Kristo na Kanisa Lake, ni hatari.

Ombi langu ni kwamba kama mwili wa wenye ukuhani, tutafanya tabia yetu itaambatana na madhumuni yetu matukufu yanayohitajika kwa wale ambao wako katika huduma ya Bwana. Katika vitu vyote tunapaswa kukumbuka kwamba kuwa “ujasiri katika ushuhuda wa Yesu” ndio mtihani wa kutenganisha katika falme wa selestia na terestria.23 Tunataka kuwa kwenye upande wa selestia wa mpaka. Kama mmoja wa Mitume Wake, mimi natoa ushuhuda wa dhati wa uhalisi wa Upatanisho na utukufu wa Yesu Kristo, Mwokozi wetu. Katika jina la Yesu Kristo, amina

Muhtasari

  1. Lee Mendelson-Bill Melendez ProductionTV Specials, 1966.

  2. Kutoka katika miezi ya Zohari ikimchanganya, akihofia kuhusu sumu kati glovu yake, Lucy alirazini daima kwa nini aliachilia mpira.

  3. Ona “Decisions Determine Destiny,” sura ya 8 katika Pathways to Perfection: Discourses of Thomas S. Monson(1973), 57–65.

  4. Isaya 7:15.

  5. “Kama kufanya ingekuwa rahisi kama vile kujua kuna maanga gani basi kufanya, makanisa madogo yamekuwa makaisa, na nyumba kwa maskini kasri kwa mwanafalme” (William Shakespeare, The Merchant of Venice, mchezo wa 1, sehemu ya 2, mistari ya 12–14).

  6. Mafundisho na Maagano 58:27.

  7. Ona Adjusting to Missionary Life (booklet, 2013), 23–49.

  8. Ona Stephanie Rosenbloom, “Dealing with Digital Cruelty,” New York Times, Aug. 24, 2014, SR1.

  9. Randall  L. Ridd, “The Choice Generation,” Ensign orLiahona, May 2014, 56.

  10. Ona Mafundisho na Maagano 45:26.

  11. Ona David A. Bednar, “To Sweep the Earth as with a Flood” (hotuba iliyotoleewa katika BYU Campus Education Week, Aug. 19, 2014); lds.org/prophets-and-apostles/unto-all-the-world/to-sweep-the-earth-as-with-a-flood.

  12. Arthur C. Brooks, “Love People, Not Pleasure,” New York Times, July 20, 2014, SR1.

  13. Bahati mbaya, uchepukaji mmoja ambao umeongezaka katika siku yetu ni upumbavu. Wakati Mwokozi alipoorodhesha baadhi ya vitu ambayo vinavyoweza kufanya mtu kuwa najisi, Yeye alijumuisha upumbavu (ona Marko 7:22).

  14. Hii ilitokea katika staarabu za Ugriki na Urumi ya kale, vile vile za Kitabu cha Mormoni.

  15. Ona Frederic W. Farrar, The Life and Work of St. Paul (1898), 302. Kulikuwa na wanafalsafa wa aina nyingi, ikijumuisha Waepikureona Waistoiko, makundi pinzani ambayo yalisemwa kuwa Wafarisayo na Wakaldayo wa ulimwengu wa Makafiri, Ona pia Quentin L. Cook, “Looking beyond the Mark,” Ensign, Mar. 2003, 41–44;Liahona, Mar. 2003, 21–24.

  16. Matendo ya Mitume 17:21.

  17. Matendo ya Mitume 17:32.

  18. Farrar, The Life and Work of St. Paul,312.

  19. Ona Dallin H. Oaks, “Good, Better, Best,” Ensign auLiahona, Nov. 2007, 104–8.

  20. Merlin Olsen wa mchezaji wa mpira wa Hall of Fame, mcheza sinema, mchanganuzi wa NFL. Katika Jimbo la Utah, alishinda tuzo la Outland Trophy kama mtu wa mstarini mlinda ngome. Aliteuliwa kwenye Hall of Fame ya Wachezaji wa Mpira Kulipwa mnamo 1982. Kwenye Runinga alicheza Jonathan Garvey sawa na Michael Landon katika Little House on the Prairie na alikuwa na kipindi chake cha Runinga, Father Murphy.. Merlin sana marehemu (Machi 11, 2010), na tunamkosa sana.

  21. Ona Mafundisho na Maagano 76:5.

  22. Ona Alma 34:32.

  23. Mafundisho na Maagano 76:79.