2010–2019
Chagua kwa Busara
Oktoba 2014


Chagua kwa Busara

Tathmini chaguzi zako kwa kujiuliza mwenyewe swali, “Je, maamuzi yangu yamepandwa imara katika udongo wenye rutuba wa injili ya Yesu Kristo?

Akina ndgu na dada, maamuzi tunayofanya katika maisha haya yanaathiri pakubwa sana mkondo wa maisha yetu. Kuna nguvu dhahiri na za siri zinazoshawishi chaguzi zetu. Swala hili nilijifunza miaka mitano iliyopita katika njia ambayo karibu inigharimu sana.

Tulikuwa tunasafiri na familia na marafiki kusini mwa Oman, nchi juu ya ncha ya Ghuba la Arabia. Tuliamua kubarizi katika pwani ya Bahari ya Hindi. Mara tu baada ya kuwasili kwetu, binti yetu mwenye umri wa miaka 16, Nellie, aliuliza kama angeweza kuogelea kwa kile alichokidhania kuwa fungu la mchanga. Nilipoona maji yenye mkondo, nilimwaambia kwamba nitaenda kwanza, nikifikiri huenda kuna mikondo hatari.

Baada ya kuogelea kwa muda mfupi, nilimwita mke wangu nikiuliza kama nilikuwa karibu na fungu la mchanga. Majibu yake yalikuwa, “Umeivuka kwa umbali.” Bila kujua nilinaswa ndani ya mkondo1 na nilikuwa nikivutwa kwa kasi kuingia baharini.

Sikuwa na hakika cha kufanya. Kitu tu ambacho ningeweza kufikiria ilikuwa ni kugeuza na kuogelea kuelekea ufuoni---hiyo ndiyo makosa kabisa. Nilikosa la kufanya. Nguvu kupita udhibiti wangu ilikuwa ikinivuta zaidi kuingia baharini. Kitu ambacho kilifanya mambo kuwa mabaya zaidi ni kwamba mke wangu, akiamini uamuzi wangu, alinikuwa amenifuata.

Ndugu na dada, nilifikiri kulikuwa na uwezekano mkubwa kwamba singeweza kunusurika na kwamba mimi, kwa sababu ya uamuzi wangu, ningesababisha kifo cha mke wangu. Baada ya juhudi kubwa na kile ambacho naamini ilikuwa ni msaada wa Mungu, miguu yetu kwa namna fulani iligusa sakafu yenye mchanga na tuliweza kutembea salama kwa marafiki zetu na binti yetu.

Kuna mikondo mingi katika maisha ya dunia hii---mingine ni salama na mingine si salama. Rais Spencer W. Kimball alifundisha kuwa kuna nguvu nyingi katika maisha yetu kama vile mikondo ya siri ya bahari.2 Nguvu hizi ni halisi. Hatufai kuzipuuza.

Acha niwaambie kuhusu mkondo mwingine, mkondo mtakatifu, ambao umekuwa baraka kubwa katika maisha yangu. Mimi ni mwongofu kwa Kanisa. Kabla ya kuongoka kwangu, tamaa ya maisha yangu ilikuwa ni kucheza mchezo wa kuteleza kwenye barafu na, hivyo, nilihamia Ulaya baada ya shule ya sekondari ili kutimiza lengo hilo. Baada ya miezi kadhaa ya kile kilichoonekana kama maisha bora, nilihisi kuwa nilipaswa niondoke. Wakati huo sikuelewa chanzo cha hisia hiyo, lakini niliamua kuifuata. Hatimaye nilifika Provo, Utah, na marafiki wema wachache ambao, kama mimi, walikuwa washiriki wa imani tofauti.

Nilipokuwa huko Provo, nilikutana na watu ambao walikuwa wakiishi maisha tofauti na yangu. Nilihisi kuvutiwa kwao, ingawa sikujua ni kwa nini. Awali, nilipuuza hisia hizi, lakini mara tu nilipata amani na faraja ambayo sikuwa nimewahi kujua. Nilianza kuzingatia mkondo tofauti--ambao ulinileta kwa uelewa wa Baba wa Mbinguni mwenye upendo na Mwanawe, Yesu Kristo.

Nilibatizwa pamoja na marafiki zangu mnamo 1972. Mkondo huu mpya nilioamua kufuata, injili ya Yesu Kristo, ulinipa mwelekeo na maana kwa maisha yangu. Hata hivyo, haikukosa changamoto zake. Kila kitu kilikuwa kipya kwangu. Wakati mwingine nilihisi kupotea na kuchanganyikiwa. Maswali na changamoto zilizuliwa na marafiki wote na familia.

Nilikuwa na chaguo la kufanya. Baadhi ya maswali yao yalizua mashaka na wasiwasi. Chaguo lilikuwa muhimu. Ni wapi ambapo ningegeukia kwa majibu? Kulikuwa na wengi waliotaka kunishawishi juu ya makosa ya njia zangu---“mikondo mikali” ilinuia kunivuta mbali kutoka kwa mkondo mtulivu ambao ulikuwa chanzo ajabu cha furaha. Nilijifunza vyema kanuni kwamba, kuna “upinzani katika mambo yote” na umuhimu wa kujitendea mwenyewe wala si kuacha wakala wangu kwa wengine.3

Nilijiuliza, “Kwa nini nikatae kile ambacho kiliniletea faraja kuu kama hiyo?” Kama vile Bwana alivyomkumbusha Oliver Cowdery, “Sikusema amani akilini mwako kuhusiana na jambo hili?”4Uzoefu wangu ulikuwa sawa. Kwa hiyo, niligeuka, kwa dhamira zaidi, kwa Baba mwenye upendo wa Mbinguni, kwa maandiko, na kwa marafiki waaminifu.

Bado, kulikuwa na maswali mengi ambayo singeweza kujibu. Ningeeleza vipi wasiwasi yaliyosababisha? Badala ya kuwaruhusu kuharibu amani na furaha ambayo ilitokea katika maisha yangu niliamua kuyaweka kando kwa muda, nikiamini kwamba katika wakati wa Bwana, Atafunua mambo yote. Nimeona amani katika Taarifa yake kwa Nabii Joseph: “Tazama, ninyi ni watoto wadogo na hamuwezi kuyastahimili yote hivi sasa; na lazima mkue katika neema na katika ujuzi wa kweli.”5 Nilichagua kutoacha kile nilichokijua kuwa ni kweli kwa kufuata mkondo usiojulikana na wenye wasiwasi---“mikondo halisi.” Kama vile Mzee N. Eldon Tanner alivyosema, nilijifunza, “Ni hekima na bora kiasi gani kwa mtu kukubali kweli rahisi za injili... na kukubali kwa imani mambo yote ambayo… hawezi kuelewa.”6

Je, hii inamaanisha kwamba hakuna nafasi kwa uchunguzi wa dhati? Uliza kijana aliyekimbilia katika kichaka kitakatifu akitaka kujua ni gani kati ya makanisa yote anapaswa kujiunga. Shikilia Mafundisho na Maagano katika mkono wako, na ujue kwamba sehemu kubwa ya yale yaliyofunuliwa katika rekodi takatifu imekuwa ni matokeo ya utafutaji mnyenyekevu wa kweli. Kama vile Joseph alivyogundua, “Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, …naye atapewa.”7 Kwa kuuliza maswali kamili na kutafuta majibu ya Mungu, tunajifunza “mstari juu ya mstari, amri juu ya amri,”8 tunapoongezeka katika maarifa na hekima.

Swali siyo “Je, kuna nafasi ya uchunguzi wa kweli, na wa dhati?” lakini badala yake ni “Ni wapi ambako nitageukia kwa kweli wakati maswali yanapotokea?’ “Je, nitakuwa na hekima ya kutosha ili kushikilia kwa nguvu kile ninachokijua kuwa ni kweli licha ya maswali machache ninayoweza kuwa nayo?” Nashuhudia kuna msingi mtakatifu---Mmoja anayejua mambo yote---mwisho toka mwanzo. Vitu vyote viko mbele Yake.9 Maandiko yanashuhudia kwamba Yeye “haenendi katika njia zisizo nyoofu ..., wala habadilishi kauli kutoka ile aliyosema.”10

Katika safari hii ya dunia lazima kamwe tusifikiri kwamba chaguzi zetu zinatuathiri sisi tu. Juzi, kijana mdogo alinitembelea nyumbani. Alikuwa anajihisi vizuri, lakini nilihisi hakuwa akishiriki kikamilifu katika shughuli za Kanisa. Aliniambia kwamba alilelewa katika nyumba inayozingatia injili hadi wakati baba yake alipoanza kuwa mdanganyifu kwa mama yake, na kusababisha wao kutengana na kushawishi watoto wao wote kuhoji Kanisa na kupotoka. Moyo wangu ulikuwa mzito nilipokuwa nikizungumza na mzazi huyu kijana wa watoto watano ambaye sasa, aliathirika na chaguo la baba yake, alikuwa akilea roho hawa wa thamani nje ya baraka za injili ya Yesu Kristo.

Mtu mwingine niliyemjua, ambaye wakati mmoja alikuwa mshiriki wa Kanisa mwaminifu, alikuwa na maswali kuhusu mafundisho fulani. Badala ya kuuliza Baba wa Mbinguni kwa majibu, alichagua kutegemea tu juu ya vyanzo vya kidunia kwa ajili ya uongozi. Moyo wake uligeuka upande usiofaa alipotafuta kile kilichoonekana kama heshima ya wanadamu. Kiburi chake kinaweza kuwa kilitukuzwa, angalau kwa muda, lakini alizuiliwa kushiriki uwezo wa mbinguni.11 Badala ya kupata ukweli, alipoteza ushuhuda wake na kuenda pamoja na wanafamilia wengi.

Wanaume hawa wawili walinatwa katika mikondo makali na kuleta wengi pamoja nao.

Kinyume chake, nadhani LaRue na Louise Miller, wazazi wa mke wangu, ambao kamwe hawakuwa na utajiri mwingi wa kidunia, walichagua siyo tu kufundisha mafundisho halisi ya injili rejesho kwa watoto wao lakini kuiishi kila siku ya maisha yao. Kwa kufanya hivyo wamebariki wazao wao, ambao sasa wanazidi 100, kwa matunda ya injili na matumaini ya uzima wa milele.

Katika nyumba zao walianzisha muundo ambapo ukuhani uliheshimiwa, ambapo upendo na maelewano yalikuwa tele, na ambapo kanuni za injili ziliongoza maisha yao. Louise na LaRue, kando kando, walionyesha maana ya kuishi maisha ya mfano wa Yesu Kristo. Watoto wao wangeweza kuona kwa uwazi aina ya mikondo ya maisha ambayo ingeleta amani na furaha. Na walichagua vipasavyo. Kama vile Rais Kimball alivyofunza, “Kama tunaweza kuunda ... mkondo wa nguvu na imara inayoelekea katika lengo letu la maisha ya haki, sisi na watoto wetu tunaweza kuvutwa mbele licha ya upepo pinzani wa ugumu, tamaa, [na] majaribu.”12

Je, chaguo zetu zina maana? Je, zinatuathiri sisi pekee? Je, tumeweka mwelekeo wetu imara katika mkondo wa milele wa injili iliyorejeshwa ya Yesu Kristo?

Mara kwa mara, nina picha inayonishtua. Ingekuaje siku hiyo ya Septemba, nikipumzika juu ya pwani ya Bahari Hindi, ningemwambia binti yangu, Nellie, “Ndiyo, endelea. Ogelea nje kwa fungu la mchanga.” Au kama yeye pia angefuata mfano wangu kisha ashindwe kuongelea? Na kama ingebidi niishi maisha nikijua kwamba mfano wangu ulimfanya kutupwa katika kina cha bahari na mkondo mkali, kamwe asiweze kurudi?

Je, mikondo tunayochagua kufuata ni muhimu? Je, mifano yetu inajalisha?

Baba wa Mbinguni ametubariki na karama takatifu ya Roho Mtakatifu ili kuongoza chaguzi zetu. Ametuahidi uongozi na ufunuo tunapoishi kitakatifu ili kupokea hayo. Nakualika kujinufaisha na karama hii takatifu na kutathmini chaguzi zako kwa kujiuliza mwenyewe swali, “Je, maamuzi yangu yamepandwa imara katika udongo wenye rutuba wa injili ya Yesu Kristo?” Nakualika ufanye marekebisho yoyote inaohitajika, iweni kidogo au kubwa, ili kuhakikisha baraka za milele za mpango wa Baba wa Mbinguni kwako na kwa wale unaowapenda.

Nashuhudia kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi na Mkombozi wetu, Ninashuhudia kwamba maagano tunayoyafanya naye ni mtukufu na matakatifu. Sharti kamwe tusicheze na mambo matakatifu.13 Na tuweze kubakia waaminifu Katika jina la Yesu Kristo, amina.