2010–2019
Joseph Smith
Oktoba 2014


Joseph Smith

Yesu Kristo alimchugua mtu mtakatifu, mtu mwema, kuongoza Urejesho wa ujalivu wa injili Yake. Alimchagua Joseph Smith.

Katika matembezi yake ya kwanza kwa Nabii Joseph Smith katika umri wa miaka 17, malaika alimwita Joseph kwa jina na kumwambia kuwa yeye alikuwa ni, Moroni, mjumbe aliyetumwa kutoka katika uwepo wa Mungu na kwamba Mungu alikuwa na kazi kwake ya kufanya. Fikiria kile Joseph lazima alifikiria wakati malaika alimwambia kwamba jina lake “litajulikana kwa wema na uovu miongoni mwa mataifa yote, koo, na ndimi.”1 Labda hofu, mshangao katika macho ya Joseph yalimfanya Moroni kurudia tena, kwamba yote wema na uovu yangesemwa juu yake miongoni mwa watu wote.2

Wema uliosemwa juu ya Joseph Smith ulikuja pole pole; maongezi maovu yalianza mara moja. Joseph aliandika: “Ni ya kushangaza jinsi gani mvulana asiyefahamika ... afikiriwe  … ya kutosha kuwavutia ... huzuni kubwa kwangu.”3

Vile upendo kwa Joseph uliongezeka, ndivyo pia uhasama. Akiwa na umri wa miaka 38, aliuawa na kundi la wanaume 150 waliojipaka nyuso rangi.4 Hali maisha ya Nabii yaliiisha ghafla, wema na uovu juu ya Joseph ulikuwa ndiyo tu unaanza.

Je! Tunapaswa kushangzwa na uovu uliozungumziwa dhidi yake? Mtume Paulo aliitwa mwenda wazimu na kichaa.5 Mwokozi wetu Mpendwa, Mwana wa Mungu alibandikwa mlafi, mlevi, na aliyeingiwa na iblisi.6

Bwana alimwambia Joseph juu ya kudra yake:

“Miisho ya dunia itaulizia jina lako, na wapumbavu watakudhihaki, na jahanamu itapigana nawe kwa hasira;

“Wakati walio wasafi moyoni, … na wenye hekima, … na walio wema, watafuta … baraka kutoka chini ya mkono wako daima.”7

Kwa nini Bwana huruhusu maongezi mabaya yaandame wema? Sababu moja ya upinzani dhidi ya mambo ya Mungu hufanya watafutaji wa ukweli kwenda kwenye magoti yao kwa kutafuta majibu.8

Joseph Smith ni Nabii wa Urejesho. Kazi yake ya kiroho ilianza na kutokea kwa Baba na Mwana, ikifuatiwa na matembezi mengi ya viumbe wa mbinguni. Alikuwa chombo katika mikono ya Mungu katika kuleta maandiko matakatifu, mafundisho yaliyopotea, na urejesho wa ukuhani. Umuhimu wa kazi ya Joseph huhitaji zaidi kuliko tathimini za kiakili; huhitaji kile sisi, kama Joseph, “kuomba Mungu.”9 Maswali ya kiroho yahahitaji majibu ya kiroho kutoka kwa Mungu

Wengi wa wale wanaopuuza kazi ya Urejesho kwa kawaida hawaamini kwamba viumbe wa mbinguni wanaweza kuzungumza na watu ulimwenguni. Haiwezekani, wao husema, kwamba mabamba ya dhahabu yaliletwa na malaika na yakatafsiriwa kwa uwezo wa Mungu. Kutokana na kutoamini huku, walikaata upesi ushuhuda wa Joseph, na wachache kwa bahati mbaya wakaangukia kushambulia maisha ya Nabii na kusema masingizio juu ya silka yake.

Sisi hasa uhuzunika wakati mtu ambaye wakati mmoja alimstahi Joseph anapogeuka kutoka kwa usadiki wake na kisha kumkashifu Nabii.10

“Kujifunza Kanisa kupitia macho ya waasi wake,” Mzee Neal  A. Mazwell wakati mmoja alisema, “ni kama kuwahoji kina Yuda ili kumwelewa Yesu. Waasi daima hutwambia zaidi kuhusu wao wenyewe kuliko kuhusu kile ambacho kilichowasababisha kuondoka.”11

Yesu alisema, “Wapendeni adui zenu, … waombeeni wanaowaudhi, na wanaowatesa.”12 Acheni tufanye ukarimu kwa wale wanaomkashifu Joseph Smith, tukijua mioyo yetu wenyewe kwamba alikuwa nabii wa Mungu na kuwa na faraja kwamba haya yote yalitabiriwa kitambo na Moroni.

Tunapaswa kumjibu vipi muuliza wa dhati ambaye angependa kujua maneno hasi aliyosikia au kusoma kuhusu Nabii Joseph Smith? Hakika, daima tunakaribisha maswali ya uaminifu na haki.

Kwa maswali kuhusu silka ya Joseph, tunaweza kushiriki maneno ya maelfu ambao walimjua kibinafsi na ambao walijitolea maisha yao kwa kazi aliyosaidia kuanzisha. John Taylor, ambaye alipigwa risasi mara nne na kundi ambalo lilimuua Joseph, alitangaza baadaye: “Mimi nashuhudia mbele za Mungu, malaika, na watu, kwamba [Joseph] alikuwa mtu mzuri, wa kuheshimika, [na] mwema---…[na] kwamba silka yake kindani na kwa umma ilikuwa halisi---na kwamba aliishi na kufariki kama mtu wa Mungu.”13

Tunaweza kumkumbusha muulizaji wa dhati kwamba habari za Intaneti hazina kichungi cha “ukweli.” Baadhi ya habari, hata kama zinasadikika, kwa kawaida sio za kweli.

Miaka mingi iliyopita, nilisoma makala ya gazeti la Time ambayo ilitoa taarifa za uvumbuzi wa barua, ikisemekana iliandikwa na Martin Harris, ambayo ilitofautiana na habari za Joseph Smith za kupata mabamba ya Kitabu cha Mormoni.14

Washiriki wachache waliacha Kanisa kwa sababu ya hati hiyo.15

Cha kuhuzunisha, waliondoka upesi sana. Miezi baadaye wataalamu waligundua (na mbini alikiri) kwamba barua ilikuwa udanganyifu kabisa.16 Mnaweza kueleweka kutilia shaka kile mmesikia kuhusu habari, lakini hamna haja kamwe ya kushuku ushuhuda wa manabii wa Mungu.

Tunaweza kumkumbusha muulizaji kwamba baadhi ya habari kumhusu Joseph, hali zikiwa ni kweli, zilisemwa kwa njia ya ufumaji katika siku yake na hali.

Mzee Russell  M. Nelson alionyesha pointi hii. Alisema: “Nilikuwa nikihudumu kama mshauri wa serikali ya Marekani katika National Center for Disease Control katika Atlanta, Georgia. Wakati mmoja nikingojea teksi inipeleke kwenye uwanja wa ndege baada ya mikutano yangu kumalizika, nilinyosha miguu kwenye bustani ili nipigwe na miale michache ya jua kabla kurudi … kwenye baridi ya Utah. … Baadaye nilipokea picha katika barua iliyopigwa na mpiga picha akitumia lenzi ya masafa, akipiga picha ya dakika ya mapumziko yangu kwenye bustani. Chini yake kulikuwa na maneno, ‘Mshauri wa serikali katika Kituo cha Kitaifa.’ Picha ilikuwa kweli, maneno yalikuwa kweli, lakini ukweli ulitumiwa kueneza onyesho la uongo.”17 Hatuwezi kutupilia mbali kitu tunachojua kuwa ni cha kweli kwa sababu hatukielewi bado.

Tunaweza kumkumbusha muulizaji kwamba Joseph hakuwa peke yake katika matembezi ya malaika.

Mashahidi wa Kitabu cha Mormoni waliandika: “Na tunatangaza kwa maneno ya kiasi, kwamba malaika wa Mungu aliteremka kutoka mbinguni, na ... tukatazama na kuona hizo bamba.”18 Tunaweza kunukuu wengine wengi pia.19

Muulizaji wa dhati anapaswa kuona kuenezwa kwa injili ya urejesho kama tunda la kazi ya Bwana kupitia Nabii.

Sasa kuna zaidi ya mkusanyiko 29,000 na wamisionari 88,000 wanaofunza injili kote duniani. Mamilioni ya Watakatifu wa Siku za Mwisho wanatafuta kumfuata Yesu Kristo, kuishi maisha ya heshima, kuwatunza maskini, na kutoa muda wao na talanta zao kuwasaidia wengine.

Yesu alisema:

“Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. …

“ …Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.”20

Maelezo haya yanasadikika, lakini muulizaji mwaminifu hapaswi kuyategemea tu hayo peke yake ili kusitisha upekuzi wake wa ukweli.

Kila muumini anahitaji thibitisho la kiroho la huduma takatifu na silka ya Nabii Joseph Smith. Hii ni kweli kwa kila kizazi. Maswali ya kiroho yanahitaji majibu ya kiroho kutoka kwa Mungu.

Hivi majuzi Mimi nikiwa kwenye Pwani ya Mashariki ya Marekani, mmisionari aliyerejea alizungumza nami kuhusu rafiki ambaye alikuwa amekanganywa na habari alizopokea kuhusu Nabii Joseph Smith. Walikuwa wameongea mara kadhaa, na mmisionari aliyerejea alionekana kuwa na shaka yeye mwenyewe kama matokeo ya mazungunzo hayo.

Ingawa nilitumaini angemuimarisha rafiki yake, nilihisi wasi wasi kuhusu ushuhuda wake mwenyewe. Ndugu na kina dada, acha niwape tahadhari: hamtakuwa wa msaada wowote kwa wengine kama imani yenu wenyewe haijakita vyema.

Wiki chache zilizopita niliabiri ndege kwenda Amerika Kusini. Mhudumu wa ndege alielekeza usikivu wetu kwenye video ya usalama. “Si kawaida,” tulionywa, “lakini kama kanieneo ya chumba ikibadika, vifiniko vilivyo juu ya viti vyenu vinafunguka, vifuniko vya oksijeni vitatokea. Hii ikitokea, inuka na uvute kifuniko kukwelekea. Weka kifuniko kwenye pua na mdomo wako. Vuruta mshipi wa mpira kwenye kichwa chako na utengeneze kifuniko kama inahitajika.” Kisha, tahadhari hii: “Hakikisha kutengeneza kifuniko chako mwenye kabla ya kusaidia wengine.”

Habari hasi kuhusu Nabii Joseph Smith zitaongezeka tunapokaribia Ujio wa Pili wa Mwokozi. Kweli nusu na udanganyifu usioeleweka kwa urahisi hautafifia. Kutakuwa na wanafamilia na marafiki ambao wanahitaji msaada wako. Sasa ndiyo wakati wa kutengeneza kifuniko cha oksijeni cha kiroho chako mwenyewe ili kwamba uwe tayari kuwasaidia wengine ambao wanatafuta ukweli.21

Ushuhuda wa Nabii Joseph Smith unaweza kuja kwa njia tofauti kwa kila mmoja wetu. Unaweza kuja unapopiga magoti katika sala, ukimwomba Mungu athibitishe kwamba alikuwa nabii wa kweli. Unaweza kuja unaposoma habari za Nabii za Ono la Kwanza. Ushuhuda bado unaweza kutiririka kwenye nafsi yako unaposoma Kitabu cha Mormoni tena na tena. Unaweza kuja unapotoa ushuhuda wako mwenyewe wa Nabii au unaposimama katika hekalu na kutambua kwamba kupitia Joseph Smith nguvu takatifu za kufunganishwa zilirejeshwa ulimwenguni.22 Kwa imani na nia halisi, ushuhuda wako wa Nabii Joseph Smith utaimarishwa. Vipigo vya maji kutoka pande zote mara kwa mara vinawafanya mlowe, lakini kamwe, kamwe havitaweza kuzima moto uwakoa wa imani,

Kwa vijana wanaosikiliza leo au watakaosoma maneno katika siku zijazo, ninawapatia changamoto mahususi: “Pateni ushahidi wa kibinafsi wa Nabii Joseph Smith. Acha sauti zenu zisaidie kutimiza maneno ya kinabii ya Moroni kusema wema wa Nabii. Hapa kuna mawazo mawili: Kwanza, tafuta maandiko katika Kitabu cha Mormoni ambayo unahisi na unaamini ni kweli kabisa. Kisha yashiriki na familia na marafiki katika jioni ya familia nyumbani, seminari, na madarasa yenu ya Wavulana ma Wasichana, mkikiri kwamba Joseph alikuwa chombo katika mikono ya Mungu. Kisha, someni ushuhuda wa Nabii Joseph Smith katika Lulu ya Thamani Kuu au katika kijitabu hiki, sasa iliyoko katika lugha 158. Mnaweza kuipata kwenye mtandao katika LDS.org, au kwa wamisionari. Huu ndiyo ushuhuda wa Joseph mwenyewe wa kile hasa kitakachotokea. Uusome kila mara. Fikiria kunasa ushuhuda wa Joseph Smith kwa sauti yako mwenyewe, uusikilize kila mara, na kuushiriki na marafiki. Kusikiliza ushuhuda wa Nabii katika sauti yako mwenyewe kutakusaidia kuleta ushahidi unaotafuta.

Kuna siku kuu na za ajabu zinazokuja. Rais Thomas  S. Monson amesema: “Hii kazi kuu … inataendelea mbele, ikibadilisha na kubariki maisha. … Hakuna nguvu katika duniani yote inayoweza kusimamisha kazi ya Mungu. Licha ya kile kinachotokea, kazi hii kuu itaenda mbele.”23

Natoa ushahidi wangu kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwokozi na Mkombozi wetu. Yeye alimchagua mtu mtakatifu, mtu mwema, kuongoza Urejesho wa ujalivu wa injili Yake. Yeye alimchagua Joseph Smith.

Ninashuhudia kwamba Joseph Smith alikuwa mtu mwaminifu na mwema, mwanafunzi wa Bwana Yesu Kristo. Mungu Baba na Mwanawe, Yesu Kristo alimtokea. Alitafsiri Kitabu cha Mormoni kwa kipawa na uwezo wa Mungu.

Katika jamii yetu iliyo upande wa utandu wa kifo, tutaelewa kwa uwazi wito mtakatifu wa huduma takatifu ya Nabii Joseph Smith. Katika siku isiyo mbali sana, wewe na mimi na mamilioni [zaidi] watamjua ‘Ndugu Joseph’ tena.”24 Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Joseph Smith—Historia 1:33.

  2. Ona Joseph Smith—Historia 1:29–46.

  3. Joseph Smith—Historia 1:23.

  4. Ona Mafundisho na Maagano 135:1.

  5. Ona Matendo ya Mitume 26:24.

  6. Ona Mathayo 11:19; Yohana 10:20.

  7. Mafundisho na Maagano 122:1–2.

  8. Rais Dieter  F. Uchtdorf alisema: “Kwanza shuku shaka zako kabla haujashuku imani yako. Ni sharti kamwe tusiruhusu shaka kushika mateka na kutuzuia kutoka kwa upendo mtakatifu, amani, na vipawa ambavyo huja kupitia imani katika Bwana Yesu Kristo” (“Come, Join with Us,” Ensign or Liahona, Nov. 2013, 23). Mzee Jeffrey R. Holland alisema: “Hii ni kazi takatifu katika mchakato, ikiwa na maonyesho na baraka za ikizangaa kila upande, kwa hivyo tafadhali msishikamane ikiwa mara kwa mara mambo yatazuka ambayo yanahitaji kukaguliwa, na kueleweka, na kusuluhishwa. Yanatokeza na yatatokeza. Katika Kanisa hili, kile tunachojua daima kitashinda kile tusichokijua” (“Lord, I Believe,” Ensign or Liahona, May 2013, 94).

  9. Yakobo 1:5; ona pia Joseph Smith—Historia 1:11–13.

  10. Daniel Tyler akumbuka: “Ndugu Isaac Behunin nami [tulimtembelea Nabii] katika nyumbani kwake. Mateso yake yalikuwa mada ya mazungumzo. Alirudia taarifa nyingi za uongo, za kuchanganya zilizofanywa na waasi. … Pia alitwambia jinsi wengi wa maafisa ambao wange… twaa uhai wake kama [wangependa], wakati aliokamatwa, lakini walimpendelea baada [kumjua vyema]. …“ … Ndugu Behunin asema: “Ikiwa nitaliacha Kanisa hili singefanya kama watu hawa walifanya: Nitaenda mahali fulani pa mbali ambapo Umormoni haujasikika kamwe, nifanya makazi na hakuna mtu atakaye jua kwamba nilijua chochote kulihusu.“[Joseph] mara moja akajibu: Ndugu Behunin, haujui kile ungefanya. Hamna shaka watu hawa wakati mmoja walidhania kama unavyodhania. Kabla ya kujiunga na Kanisa hili ulisimama kwenye uwanda msimamo kati. … Ulipojiunga na Kanisa hili usailiwa kumtumikia Mungu. Ulipofanya hivyo uliacha uwanda wa msimamo kati, na kamwe hauwezi kurudi huko. Kama unamwacha Bwana ulisailiwa kumtumikia, itakuwa ni kwa shinikizo la yule muovu, na utafuata maelekezo yake na utakuwa mtumishi wake’” (katika Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 324).

  11. Neal A. Maxwell, “All Hell Is Moved” (Brigham Young University devotional, Nov. 8, 1977), 3; speeches.byu.edu.

  12. Mathayo 5:44.

  13. Teachings of Presidents of the Church: John Taylor (2001), 83; ona pia Mafundisho na Maagano 135:3.

  14. Ona Richard N. Ostling, “Challenging Mormonism’s Roots,” Time, May 20, 1985, 44.

  15. Ona Ostling, “Challenging Mormonism’s Roots,” 44; ona pia Gordon B. Hinckley, “Lord, Increase Our Faith,” Ensign, Nov. 1987, 52; Neil L. Andersen, “Trial of Your Faith,” Ensign au Liahona, Nov. 2012, 41.

  16. Ona Richard E. Turley Jr., Victims: The LDS Church and the Mark Hofmann Case (1992).

  17. Russell M. Nelson, “Truth—and More,Ensign, Jan. 1986, 71.

  18. “Ushuhuda wa Mashahidi Watatu,” Kitabu cha Mormoni.

  19. Ona Joseph Smith—Historia 1:71, muhtasari; ona pia Mafundisho na Maagano 76:23.

  20. Mathayo 7:18, 20.

  21. Rais Henry  B. Eyring, katika kuzungumza kuhusu wale walio na shaka, alisema: Kwa upendo wako kwao unaweza kuamua kujaribu kuwapa kile wanachouliza. Unaweza kujaribiwa kwenda pamoja kupitia shaka zao, kwa tumaini kwamba unaweza kupata ushahidi au sababu za kuondosha shaka zao. Watu wenye shaka kila mara wanataka kuzungumza kile wanafikiria ni ukweli wa mambo au ubishi ambao ulisababisha shaka zao, na kuhusu jinsi inaumiza. …“Wewe na nami tunaweza kufanya vyema ikiwa hatutakaa sana na kile wanafunzi wetu wanaona kama ni chanzo cha shaka zao. … Shida yao haipo katika kile wanachofikiria wanaona; ipo katika kile bado hawawezi kuona. … Tunaweza kufanya ikiwa tutageuza mazungumzo mapema hadi kwenye mambo ya moyo, yale mabadiliko ya moyo ambayo yanafungua macho ya kiroho” (“‘And Thus We See’: Helping a Student in a Moment of Doubt” [address to Church Educational System religious educators, Feb. 5, 1993], 3, 4; si.lds.org).

  22. Rais Gordon  B. Hinckley alisema: “Miaka mingi iliyopita wakati nilikuwa na umri wa miaka kumi na miwili nilitawaza kuwa shemasi, baba yangu alikuwa rais wa kigingi chetu, alinipeleka katika mkutano wa kigingi wa ukuhani wangu kwa kwanza. [Wimbo wa kufungua ulikuwa “Praise to the Man,”] Walikuwa wanaimba kuhusu Nabii Joseph Smith, na walipokuwa wanafanya hivyo kulikuja ndani ya moyo wa mafuriko ya upendo kwa na imani katika huyu Nabii mkuu wa kipindi hiki. … Nilijua wakati huo, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kwamba Joseph Smith alikuwa kwa kweli nabii wa Mungu” (“Praise to the Man,” Ensign, Aug. 1983, 2; Tambuli, Jan. 1984, 1, 2).

  23. Thomas S. Monson, “As We Gather Once Again,” Ensign or Liahona, May 2012, 4.

  24. “Praise to the Man,” Hymns, no. 27.