2023
Kimbilio kutoka kwenye Dhoruba
Machi 2023


“Kimbilio kutoka kwenye Dhoruba,” Liahona, Machi 2023.

Karibu kwenye Toleo Hili

Kimbilio kutoka kwenye Dhoruba

Picha
mvua ikinyesha baharini

Picha kupitia Getty Images

Je, umewahi kuketi ndani ya hifadhi wakati wa dhoruba? Wakati maji yanaposhuka chini, yanaipiga paa na kuzamisha sauti zingine. Unawezaje kuwa mkavu katikati ya dhoruba? Nguvu na uwepo wa Mwokozi wetu ni kama hifadhi.

Toleo la Liahona linafokasi juu ya jinsi Yesu Kristo anavyoleta amani katika dhoruba za maisha. Hatuwezi kuepuka majaribu na changamoto. Lakini kama vile hifadhi inavyotuweka wakavu wakati wa mvua, tunapomwalika Yesu Kristo kutembea nasi katika safari yetu, Yeye hutusaidia kupata amani katika dhoruba. Ninawaalika msome makala ya Mzee Dieter F. Uchtdorf “Amani Yangu Ninawapa” (ukurasa wa 4). Anafundisha, “Yesu Kristo, ambaye anadhibiti vipengele, anaweza pia kuifanya rahisi mizigo yetu” na “amani haipaswi kuondolewa mioyoni mwetu, hata ikiwa lazima tuteseke, tuhuzunike na tumngojee Bwana.”

Mimi pia nimepitia “dhoruba” katika maisha yangu. Majaribu haya yamenifunza kwamba Yesu Kristo ndiye chanzo pekee cha kudumu cha msaada na amani. Kama ninavyoelezea katika makala yangu “Nguvu ya Kuinua” (ukurasa wa 40), Mwokozi wetu anaweza na ataweza kutembea pamoja nasi kwenye safari yetu ya kuelekea nyumbani. Yeye yu pamoja nasi wakati tunapongojea baraka zetu zilizoahidiwa. Na kamwe hatujachelewa kwa Yeye kutuinua. Yeye anakupenda. Ninaomba kwamba utamruhusu Yeye awe kimbilio lako na mahala pa usalama bila kujali unachopitia.

Kwa upendo,

Bonnie H. Cordon

Rais Mkuu wa Wasichana