2023
Inamaanisha Nini Kuitakasa Siku ya Sabato?
Machi 2023


“Inamaanisha Nini Kuitakasa Siku ya Sabato?,” Liahona, Machi 2023.

Njoo, Unifuate

Mathayo 12

Inamaanisha Nini Kuitakasa Siku ya Sabato?

Picha
Yesu pamoja na wengine kwenye shamba la nafaka

Kupita Mashamba ya Nafaka, na W. Paget © Providence Collection / imepata leseni kutoka Goodsalt.com

Rais Russell M. Nelson anaeleza jinsi, akiwa kama kijana, alijifunza orodha ya mambo ya kufanya au kutofanya katika siku ya Sabato. Baadaye alijifunza kutoka kwenye maandiko kwamba mwenendo wake na mtazamo wake juu ya Sabato vilikuwa ishara kati yake na Baba yake wa Mbinguni (ona Kutoka 31:13).

Alisema “Kwa uelewa huo, sihitaji tena orodha ya mambo ya kufanya na kutofanya. Nilipohitaji kufanya uamuzi ikiwa shughuli ilikuwa au haikuwa sahihi kwa ajili ya Sabato, nilijiuliza, ‘Ni ishara gani ninataka kumwonesha Mungu?’” (“The Sabbath Is a Delight,” Liahona, Mei 2015, 130; msisitizo kwenye halisi).

Shughuli

Soma mafundisho ya Kristo kuhusu siku ya Sabato katika Mathayo 12:1–13; ona pia Isaya 58:13 na Mafundisho na Maagano 59:9–13. Jaza chati yenye kanuni za injili unazozipata kwenye mafundisho haya. Kama familia, jadilini jinsi mnavyoweza kutumia mafundisho haya leo. Mnaweza kuandika mawazo yenu kwenye safu ya “Matumizi katika Siku za Leo”.

Mafundisho ya Yesu

Matumizi katika Siku za Leo