2023
Desturi za Maziko ya Kiyahudi
Machi 2023


“Desturi za Maziko ya Kiyahudi,” Liahona, Machi 2023.

Desturi za Maziko ya Kiyahudi

Lazaro, Martha na Mariamu walikuwa ndugu walioishi katika mji wa Bethania. Walikuwa marafiki wa Mwokozi na Mwokozi aliwatembelea mara kadhaa. Wakati fulani katika huduma Yake, Yesu aliondoka Yudea, ambapo Bethania inapatikana, kwa sababu Wayahudi katika eneo lile walitaka kumuua (ona Yohana 10:39–40). Wakati Yesu akiwa mbali, Lazaro aliugua, akafa na akazikwa kulingana na desturi za Kiyahudi (ona Yohana 11:1–17).

Hizi ni baadhi ya desturi ambazo yawezekana walizifuata kwenye kifo na maziko ya Lazaro.

Picha
Kimiminika kikimiminwa mkononi

Baada ya mtu kufa, macho yake yalifumbwa. Mwili ulioshwa kwa manukato kama vile, manemane, marhamu na uudi (ona Luka 23:56; Yohana 19:38–40).

Vielelezo na Noah Regan

Picha
watu wakiwa wamesimama pembeni ya mwili uliovikwa sanda

Mwili ulivikwa sanda na kupelekwa nyumbani kwa familia, ambapo ndugu na majirani wangeweza kuja kutoa pole (ona Matendo ya Mitume 9:37)

Picha
mwili ukiwa umebebwa juu ya jeneza

Kwa kawaida ndani ya masaa nane ya kifo, mwili ulipelekwa kaburini ukiwa juu ya jeneza hivyo wageni wote waliweza kuuona mwili (ona Luka 7:12–14). Wanawake waliongoza maandamano. Wanafamilia walichana mavazi yao kama ishara ya kuomboleza.

Picha
wanawake wakiingia ndani ya kaburi lililo wazi

Baadhi ya makaburi yalikuwa yamechongwa kwa mawe (ona Mathayo 27:58–60). Makaburi yalikuwa na uwazi mdogo hivyo watu ilibidi wainame ili kuingia.

Picha
mwili ukiwa juu ya meza ya jiwe ndani ya kaburi

Mwili ulilazwa kwenye meza iliyochongwa kwa jiwe. Kaburi lilifunikwa kwa jiwe kubwa la mviringo ili kuzuia wezi au wanyama kuingia.1

Baada ya Yesu kumfufua Lazaro kutoka wafu, wafuasi Wake walikuwa na sababu kubwa ya kutumaini badala ya kuomboleza vifo vya wapendwa wao. Wasingeweza kukana kwamba, kwa sababu ya Yesu Kristo, “kaburi lisiwe na ushindi, na kwamba kifo kisiwe na uchungu” (Mosia 16:7).

Muhtasari

  1. Ona Henri Daniel-Rops, Daily Life in Palestine at the Time of Christ (trans. Patrick O’Brian, 1962), 328–33; ona pia Kamusi ya Biblia, “Maziko.”