2023
Kutumaini katika Nguvu ya Bwana na Manabii
Machi 2023


“Kutumaini katika Nguvu ya Bwana na Manabii,” Liahona, Machi 2023.

Kwa ajili ya Wazazi

Kutumaini katika Nguvu ya Bwana na Manabii

Picha
Rais Nelson na Dada Nelson wakisalimiana na wavulana wawili

Picha imepigwa na Ravell Call, Deseret News

Wapendwa Wazazi,

Katika ulimwengu wetu wenye mkanganyiko unaoongezeka, ni rahisi kuhisi hofu na kutokuwa na uhakika. Lakini tunapomgeukia Yesu Kristo kwa ajili ya faraja, Yeye anaweza kutuletea amani katika dhoruba za maisha. Soma makala katika toleo hili ili kufahamu jinsi Mwokozi anavyoweza kukusaidia kupita changamoto zako.

Mijadala ya Injili

Mwokozi Kwa Utayari Hutoa Amani katika Nyakati za Kutatiza

Ukiwa na familia yako, someni makala ya Mzee Uchtdorf kwenye ukurasa wa 4 kuhusu jinsi kutumaini katika nguvu wezeshi ya Kristo kunavyoweza kuleta amani katika nyakati ngumu. Jadilini pamoja baadhi ya njia ambazo kwazo Yesu hutoa usaidizi. Ni kipi mnaweza kufanya ili kualika nguvu Yake kwenye maisha yenu?

Ni kwa Jinsi Gani Ukuhani Hubariki Familia Yetu?

Soma makala kwenye ukurasa wa 22 kuhusu baraka za ukuhani. Waalike wanafamilia washiriki nyakati ambapo walipokea baraka ya ukuhani. Je, walihisi vipi? Ni kwa jinsi gani baraka iliwasaidia? Je, kuna baraka ambayo inaweza kumsaidia mwanafamilia sasa?

Bwana Humtumia Nabii Wake ili Kutusaidia Tukuze Ujasiri

Katika makala kwenye ukurasa wa 30, Mzee Sikahema anazungumza kuhusu jinsi ambavyo kufuata mafundisho ya nabii kulimsaidia wakati wa kazi yake ya kuajiriwa kama mcheza soka la kulipwa wa Amerika na kote katika maisha yake. Baada ya kusoma makala hii, ungeweza kumruhusu kila mshiriki wa familia yako aelezee wakati ambapo kumfuata nabii kuliwasaidia kuwa na ujasiri.

Burudani ya Familia ya Njoo, Unifuate

Kukua, Kukua, Kila Siku

Kama waumini wa Kanisa la Yesu Kristo lililorejeshwa, tunao wajibu wa kusaidia kukuza ufalme wa Mungu duniani. Mathayo 13:31–32 inasema:

“Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya haradali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake:

“Nayo ni ndogo kuliko mbegu zote: lakini ikiisha kumea, huwa kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti.”

  1. Kaeni katika duara na mjikunje muwe wadogo kama punje ndogo ya haradali.

  2. Mruhusu kila mmoja kufanya zamu kutaja shughuli ambayo wataifanya kila siku ili kusaidia Kanisa likue (kutoa shuhuda zao, kushiriki andiko kwenye mtandao wa kijamii, kushiriki kweli za injili kwa rafiki, na kadhalika).

  3. Kila wakati mtu anapotaja shughuli ambayo husaidia Kanisa likue, kila mmoja anajikunjua wima kidogo kidogo na kisha kuanza kusimama mpaka wawe wamesimama wima.

  4. Jadili pamoja na familia yako kwa nini ni muhimu kwa kila mtu kufanya sehemu yake ili kuchangia kwenye ukuaji wa Kanisa.