“Johannesburg, Afrika Kusini,” Liahona, Machi 2023.
Kanisa Liko Hapa
Johannesburg, Afrika Kusini
Wamisionari wa kwanza wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho walifika Afrika Kusini mnamo 1852. Tangu mwaka huo na kuendelea, waumini wameshinda vikwazo vya kimbari na kiutamaduni ili kujenga umoja na urafiki. Leo, Kanisa katika nchi ya Afrika Kusini lina:
-
Waumini 69,400 (kwa makadirio)
-
Vigingi 17, kata na matawi 195, misheni 4
-
Mahekalu 2 (Johannesburg na Durban) na 1 limetangazwa (Cape Town)
Kubarikiwa na Injili
Akiwa amekumbatiwa na mpwa wake mkuu Thuto (kushoto) na mpwa wake Lizzie Mohodisa (kulia), Dimakatso Ramaisa (katikati) anasema kuishi injili pamoja kunabariki vizazi vitatu.
Picha imepigwa na Papama Tungela
Zaidi kuhusu Kanisa Afrika Kusini
-
Ukweli, takwimu na historia ya Kanisa ndani ya Afrika Kusini
-
mwanamume kutoka Afrika Kusini anatimiza lengo lake la kuhudhuria hekaluni.
-
Kitabu cha Mormoni kina matokeo ya kudumu kwa waumini wa Afrika Kusini.
-
Kanisa linatoa msaada wa viti mwendo na vifaa vya kutembelea kwenye jimbo la Afrika Kusini.
-
Mzee Ronald A. Rasband wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili anaweka wakfu hekalu la pili la Afrika Kusini
-
Waumini wanashiriki uzoefu wao tangu miaka ya 1980, wakati ambapo matawi ya Afrika Kusini yalianza kujumuika pamoja.
Usomaji binafsi wa maandiko ni sehemu ya maisha kwa Watakatifu wa Siku za mwisho wa Afrika Kusini, kama ilivyo kwa Watakatifu wa Siku za mwisho kote ulimwenguni.
Kujifunza maandiko kama familia pia ni kipaumbele cha juu kwa waumini wa Kanisa Afrika Kusini
Karibu na Cape Town, familia inatembea ufukoni, pamoja na mlima ukionekana upande wa nyuma.
Kundi la wanawake linakusanyika kando ya Hekalu la Durban Afrika Kusini kabla ya kuwekwa kwake wakfu.
Baba huko Johannesburg, Afrika Kusini, anawafunza watoto wake kuhusu nyenzo za Kanisa zinazopatikana mtandaoni.
Hekalu la Durban Afrika Kusini liliwekwa wakfu mnamo Februari 16, 2020.
Mzee Ronald A. Rasband pamoja na mkewe wakisalimiana na waumini baada ya mkutano huko Afrika Kusini.