2023
Mwokozi Anawezaje Kunisaidia?
Machi 2023


“Mwokozi Anawezaje Kunisaidia?,” Liahona, Machi 2023.

Njoo, Unifuate

Mathayo 8; Luka 7

Mwokozi Anawezaje Kunisaidia?

Picha
mtu akiwa amepiga magoti mbele ya Yesu

Kumponya Mwenye Ukoma, na E. S. Hardy © Providence Collection / imepata leseni kutoka Goodsalt.com

Yesu Kristo, “alizunguka huko na huko, akitenda kazi njema” (Matendo ya Mitume 10:38): Alimponya mwenye ukoma (ona Mathayo 8:2–3). Alimponya mtumishi wa akida, ambaye hakuhisi kustahili lakini aliamini Mwokozi angeweza kumsaidia tu (ona Mathayo 8:5–13). Alitoa amani kwa wanafunzi Wake wakati wa dhoruba (ona Mathayo 8:23–27). Alipomwona mwanamke aliyehuzunishwa kwa kifo cha mwanaye wa pekee, alimfariji na kumpa tumaini, kisha alimfufua mwanaye kutoka wafu (ona Luka 7:11–15).

Shughuli

Tunaweza kuuhisi uwezo wa Mwokozi leo pale tunapoonesha imani Kwake. Soma moja ya matukio kutoka kwenye usomaji wa Njoo,Unifuate wa wiki hii. Tilia maanani jinsi Mwokozi alivyoitikia mahitaji na imani za watu.

Tafakari au jadili maswali yafuatayo ili kuzingatia jinsi ambavyo Mwokozi amekusaidia katika maisha yako:

  • Ni lini nimeweka imani yangu katika Mwokozi na kuhisi uponyaji Wake (kihisia, kiakili, kiroho au kimwili)?

  • Ni lini nimehisi amani Yake?

  • Ni lini nimepokea usaidizi ambao sikuutarajia kutoka kwa Mwokozi?

  • Ni lini nimeuona mkono Wake kupitia muujiza au huruma nyororo?

  • Kwenye maisha yangu sasa, ninawezaje kuimarisha imani yangu Kwake na kupokea usaidizi Wake?