2023
Jinsi Utambulisho wa Kiungu Unavyoathiri Kuwa Sehemu ya, na Kuwa
Machi 2023


“Jinsi Utambulisho wa Kiungu Unavyoathiri Kuwa Sehemu ya, na Kuwa,” Liahona, Machi 2023.

Jinsi Utambulisho wa Kiungu Unavyoathiri Kuwa Sehemu ya, na Kuwa

Tunapoupa kipaumbele uhusiano wetu na Mungu na ufuasi wetu kwa Yesu Kristo, tutapata shangwe katika utambulisho wetu wa kiungu, tutajipatia hisia ya kudumu ya kuwa sehemu ya, na hatimaye kufikia uwezekano wetu wa kiungu.

Picha
kundi la watu mbalimbali

Chama cha Saikolojia cha Marekani kinafafanua kuwa sehemu ya, kama “hisia ya kukubalika na kuthibitishwa na kikundi.”1

Kwa bahati mbaya, siyo wote tunakuwa na hisia ya kuwa sehemu ya, na wakati mwingine tunajaribu kurekebisha uhalisia wetu ili tukubalike. “Sote tunataka kuonekana kuwa tanafaa mahala fulani,” anaeleza Joanna Cannon, mwanasaikolojia Mwingereza. “Ili kufanikisha hilo, mara kwa mara tunawasilisha toleo lililo tofauti kidogo la sisi ni nani, kutegemeana na mazingira tuliyomo na watu tunaokutana nao. Tunaweza kuwa wa ‘matoleo’ mengi ya sisi wenyewe—kazini au nyumbani au hata mtandaoni.”2

Ni muhimu kutambua kwamba kuna tofauti kati ya kufaa mahala fulani na kuwa sehemu ya. Brené Brown, Mmarekani mtafiti na mtunzi wa vitabu, alifafanua: “Kufaa mahala fulani na kuwa sehemu ya, sio kitu kimoja. Ukweli ni kwamba, kufaa mahala fulani ni moja ya kizuizi kikubwa cha kuwa sehemu ya. Kufaa mahala fulani ni kuhusu kutathmini hali na kuwa vile unavyohitaji kuwa ili ukubalike. Kuwa sehemu ya, kwa upande mwingine hakutuhitaji tubadili uhalisia wetu; kunatuhitaji tuwe kama tulivyo.”3

Kujua utambulisho wetu wa kiungu ni muhimu kwenye kuwa sehemu ya; vinginevyo tutatumia muda na juhudi zetu kujirekebisha wenyewe ili kutafuta kukubalika mahala ambapo hapaheshimu au hapalingani na asili yetu ya milele. Zaidi ya hayo, mahala tunapochagua kuwa sehemu ya, panaweza kuongoza kwenye mabadiliko katika maadili na tabia zetu pale tunapokubaliana na kanuni na viwango vya kikundi. Baada ya muda, mahala tunapochagua kuwa sehemu ya, panaathiri vile tunavyokua.

Kwa ufupi, kukumbatia utambulisho wetu wa kiungu kunashawishi wapi tunataka kuwa, na mahala petu tulipochagua kuwa hatimaye panatuongoza kwenye kuwa vile tunavyotaka kuwa.

Utambulisho wa Kiungu

Sote tuliishi na Mungu kabla ya maisha ya duniani (ona Mafundisho na Maagano 93:29; 138:55–56). Tuliumbwa kwa mfano Wake—mwanamume na mwanamke (ona Mwanzo 1:27). Yeye aliandaa mpango ili sisi tuwe kama Yeye (ona Mafundisho na Maagano 132:19–20, 23–24). Mpango wake wa furaha ulihusisha sisi kuja duniani ili kupata mwili wa nyama na mifupa, kupata maarifa na mwishowe kurejea nyumbani kwetu mbinguni ili kuishi pamoja na Yeye katika shangwe ya milele (ona 2 Nefi 2; 9; Ibrahimu 3:26). Mungu alifunua, “Hii ndiyo kazi yangu na utukufu wangu—kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu” (Musa 1:39). Cha kushangaza, sisi ndiyo kazi Yake na utukufu Wake! Hii inasema kitu fulani kuhusu thamani yetu kubwa na ustahiki wetu Kwake.

Kutokana na mabilioni ya watu duniani, wengine wanaweza kuona vigumu kukubali kwamba Mungu anamjali kila mtu. Natoa ushahidi kwamba Yeye anamjua kila mmoja wetu na pia anajua kile tunachofanya, mahali tulipo na hata “mawazo na matamanio ya mioyo [yetu]” (Alma 18:32). Siyo tu kwamba “tunahesabika kwa” Mungu (Musa 1:35) lakini pia Yeye anatupenda kikamilifu (ona 1 Nefi 11:17).

Kwa sababu ya upendo Wake mkamilifu kwetu, Baba wa Mbinguni anatamani kutupatia vyote alivyonavyo (ona Mafundisho na Maagano 84:38). Zaidi ya yote, sisi ni mabinti Zake na wana Wake. Anataka sisi tuwe kama Yeye, tufanye mambo anayofanya na tupitie shangwe aliyonayo Yeye. Tunapofungua mioyo na akili zetu kwenye ukweli huu, “Roho mwenyewe anashuhudia kwa roho zetu, kwamba sisi tu watoto wa Mungu: na kama watoto, basi tu warithi; warithi wa Mungu” (Warumi 8:16–17).

Tofauti za Maisha ya Duniani

Katika maisha kabla ya kuja duniani, tulitembea pamoja na Mungu, tulisikia sauti Yake na tulihisi upendo Wake. Tangu kipindi hicho tumepitia pazia la usahaulifu ili kuingia maisha ya duniani. Hatuna tena kumbukumbu kamili ya maisha yetu ya mwanzoni. Hali ya mazingira ya maisha ya duniani hufanya iwe vigumu zaidi kuhisi asili yetu ya kiungu na kuwa kwetu sehemu ya, tulikofurahia katika nyumba yetu ya mbinguni.

Kwa mfano, uzingatiaji sana wa tofauti zetu za kimaumbile na kimazingira kunaweza kuwa kizuizi kwenye muunganiko wetu kwa Mungu. Adui hujaribu kutumia tofauti hizi ili kutupotosha kutoka kwenye malezi yetu ya pamoja ya kiungu. Tunapokea majina kutoka kwa watu wengine na wakati mwingine hata sisi wenyewe kudhania kuwa ni yetu. Si jambo baya kujitambulisha kwa wengine kwa kuzingatia tabia za kidunia; kwa kweli, wengi wetu hupata furaha na msaada kutoka kwa wale wenye tabia na uzoefu unaofanana. Hata hivyo, tunaposahau utambulisho wetu muhimu kama watoto wa Mungu, tunaweza kuanza kuogopa, kutoaminiana, au kuhisi bora kuliko wale walio tofauti na sisi. Mitazamo hii mara nyingi huleta mgawanyiko, ubaguzi na hata maangamizo (ona Musa 7:32–33, 36).

Tunapokumbuka urithi wetu wa kiungu, utofauti wetu unaleta uzuri na utajiri kwenye maisha. Tunajiona kama kaka na dada, licha ya tofauti zetu. Tunakuja kuheshimiana na kufundishana. Tunajitahidi kutengeneza mazingira ya kusaidia wengine kuwa sehemu ya, hususani wakati tabia na uzoefu wao unapokuwa tofauti na wetu. Tunahisi shukrani kwa Mungu kwa ajili ya uumbaji Wake anuai.4

Wakati maumbile na mazingira yetu yanaathiri uzoefu wetu katika maisha ya duniani, vyote hivi havitufafanui sisi. Sisi ni watoto wa Mungu wenye uwezekano wa kuwa kama Yeye.

Kuwa sehemu ya, kupitia Yesu Kristo

Akijua kwamba tungekabiliana na changamoto za kipekee duniani, Mungu alimwandaa na kumtuma Mwanawe, Yesu Kristo, ili atusaidie tushinde vizuizi hivi. Kristo amejitolea kutusaidia kuanzisha tena uhusiano wa karibu tuliokuwa nao na Mungu katika maisha kabla ya kuja duniani. Kama Kristo alivyofafanua, “Mimi ndimi njia, kweli na uzima: mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi” (Yohana 14:6; ona pia Yohana 3:16–17).

Kristo daima yuko tayari kutusaidia. Sisi ni Wake (ona 1 Wakorintho 6:20), na anatamani tuje Kwake. Kwa maneno Yake mwenyewe, Mwokozi anaahidi, “Njoo kwangu kwa moyo wa lengo moja” (3 Nefi 12:24).

Hivyo, tunakujaje kwa Kristo kwa moyo wa lengo moja?

Kwanza, tunamkubali Yeye kama Mwokozi na Mkombozi wetu. Tunatambua ukuu wa Mungu, hali yetu ya upotevu na ya kuanguka na utegemezi wetu kamili kwa Yesu Kristo ili tuokolewe. Tunatamani kuitwa kwa jina Lake (ona Mosia 5:7–8) na tunataka kuwa wafuasi Wake “katika maisha yetu yaliyosalia” (Mosia 5:5).

Pili, tunakuja kwa Kristo kwa moyo wa lengo moja kwa kufanya na kushika maagano matakatifu na Mungu (ona Isaya 55:3). Maagano yanafanywa kupitia ibada okozi na za kuinua za injili ya Yesu Kristo zinazofanywa kwa mamlaka ya ukuhani.

Picha
mvulana akipitisha sakramenti kwa waumini

Kufanya na kushika maagano siyo tu hutuunganisha sisi kwa Mungu na kwa Mwanawe bali pia hutuunganisha sisi kwa sisi. Miaka kadhaa iliyopita, nilikuwa naitembelea Costa Rica pamoja na familia yangu na kuhudhuria mkutano wa sakramenti kwenye tawi moja la Kanisa. Tulipoingia, tulikaribishwa kwa ukarimu na waumini kadhaa. Wakati wa mkutano, tuliimba wimbo wa sakramenti pamoja na mkusanyiko huo mdogo. Tuliwaangalia makuhani wakiandaa sakramenti na kisha tukasikiliza walipokuwa wakisoma zile sala za sakramenti. Mkate na maji vilipokuwa vikipitishwa kwetu, nilizidiwa na upendo wa Mungu kwa kila mmoja wa hawa washika maagano wenzangu. Sikuwa nimewahi kukutana na yeyote kati yao hapo kabla lakini nilihisi umoja na udugu pamoja nao kwa sababu sisi sote tulikuwa tumeweka ahadi na tunajitahidi kushika ahadi zile zile kwa Mungu.

Tunapofanya na kujitahidi kushika maagano matakatifu kwa Mungu, tunaanza kupata hisia za kuwa sehemu ya, kubwa zaidi kuliko zinavyoweza kupatikana kupitia uhusiano na kikundi chochote cha kidunia au cha kimwili.5 Sisi “si wageni tena wala wapitaji, bali ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu” (Waefeso 2:19).

Ninatambua kwamba baadhi yetu, kutokana na hali za kidunia, hawatapata fursa ya kupokea kila ibada na kufanya kila agano katika maisha ya duniani.6 Katika hali kama hizo, Mungu anatutaka tutende “yote tuwezayo”(2 Nefi 25:23) ili kufanya na kutunza maagano tunayoweza kuyapata. Yeye kisha anaahidi kutupatia fursa ya kupokea ibada na maagano yoyote yaliyosalia katika maisha yajayo (ona Mafundisho na Maagano 138:54, 58)). Yeye atafanya iwezekane kwetu sisi kupokea kila baraka Yeye aliyonayo kwa ajili ya watoto Wake (ona Mosia 2:41).

Picha
mchoro wa Yesu akiwa pamoja na watoto

Kuwa kama Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo

Mungu anafurahi tunapohisi upendo, umoja na nguvu ambavyo huja kutokana na hisia ya kina ya kuwa sehemu ya, pamoja Naye, Mwanawe na wale wanaomfuata Yeye. Hata hivyo, Yeye anao mpango mkubwa zaidi kwa ajili yetu! Wakati Yeye akitualika tuje kama tulivyo, tamaa yake halisi ni kwa sisi kuwa kama Yeye.

Kufanya na kushika maagano siyo tu kunatusaidia sisi kuwa sehemu ya Mungu na Kristo lakini pia kunatuwezesha kuwa na nguvu ya kuwa kama Wao (ona Mafundisho na Maagano 84:19–22). Tunaposhika maagano yanayohusiana na ibada okozi na za kuinua za injili, uweza wa Mungu unaweza kutiririkia katika maisha yetu. Tunaweza kuiona njia ya agano kama mpango wa mafunzo wa kiungu. Tunapofanya na kushika maagano na Mungu, tunajizoeza kufikiri, kutenda na kupenda kama Yeye anavyotenda. Kidogo kidogo, kwa msaada Wake na nguvu Yake, tunawezeshwa kuwa kama Yeye.

Mungu anatamani sisi tuungane na Yeye na Mwanawe katika “kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu” (Musa 1:39). Ametupatia kila mmoja wetu muda hapa duniani, vipawa vya kiroho, na haki ya kujiamulia ili tuvitumie katika huduma kwa wengine. Sisi ni wana na mabinti Zake, na Yeye anayo kazi muhimu kwa ajili yetu kuifanya (ona Musa 1:4, 6).

Ili kuwa na tija katika kazi Yake, tunahitaji kujifunza kumweka Mungu kwanza na mara kwa mara kuweka mahitaji ya wengine mbele ya yale ya kwetu. Kufokasi huko kunahitaji dhabihu binafsi (ona Mafundisho na Maagano 138:12–13) lakini pia huleta maana ndani ya maisha yetu na huleta shangwe kuu zaidi (ona Alma 36:24–26).

Tunapojikita katika kazi ya Mungu, siyo tu tunakuwa washiriki wa kikundi; badala yake, tunakuwa wenzi halisi pamoja na Mungu na Mwanawe, Yesu Kristo. Hakuna hisia kubwa zaidi kuliko kujua kwamba Mungu anatutumaini sisi vya kutosha kufanya kazi kupitia sisi ili kuleta uzima wa milele kwa wengine.

Picha
kundi la watu mbalimbali wakijumuika

Mialiko Mitatu

Katika kuhitimisha, ninatoa mialiko mitatu ambayo inaweza kutusaidia kupata hisia za shangwe na za kudumu za utambulisho na za kuwa sehemu ya, na kutuwezesha kufikia uwezekano wetu wa kiungu.

1. Ninakualikeni kuwekea kipaumbele utambulisho wetu wa kiungu kama mabinti na wana wa Mungu. Hii inamaanisha kwamba tunaweka ustahiki wetu binafsi kwenye malezi yetu ya kiungu. Tunatafuta kujenga uhusiano wetu na Mungu kupitia sala na kujifunza maandiko, kuitakasa Sabato na kuabudu hekaluni na shughuli nyingine yoyote ambayo inamleta Roho Mtakatifu katika maisha yetu na kuimarisha muunganiko wetu Kwake. Tunamwacha Mungu ashinde katika maisha yetu.7

2. Ninakualikeni kumkubali Yesu Kristo kama Mwokozi wetu na kuweka ufuasi wetu Kwake juu ya mazingatio mengine. Hii inamaanisha kwamba tunajichukulia jina Lake juu yetu na kwamba tunatamani kujulikana kama wafuasi Wake. Tunatafuta kupata msamaha Wake na nguvu Zake kila siku. Tunafanya maagano na kuyashika. Tunajitahidi kuwa kama Yeye.

3. Ninakualikeni kujikita katika kazi ya Mungu kwa kuwasaidia wengine waje kwa Kristo na kupata uzima wa milele. Hii inamaanisha tunawasaidia wengine waone utambulisho wao wa kiungu na kupata hisia za kuwa sehemu ya. Kwa uwazi tunashiriki shangwe tuipatayo katika Yesu Kristo na injili Yake (ona Alma 36:23–25). Tunajitahidi kuwasaidia wengine wafanye na kushika maagano matakatifu kwa Mungu. Tunatafuta mwongozo wa Mungu ili kujua nani tunaweza kumbariki na jinsi ya kufanya hivyo.

Ninaahidi kwamba tunapowekea kipaumbele uhusiano wetu na Mungu na ufuasi wetu kwa Yesu Kristo, tutapata shangwe katika utambulisho wetu wa kiungu, tutapata hisia za kudumu za kuwa sehemu ya, na mwishowe kufikia uwezekano wetu wa kiungu.

Kutoka kwenye hotuba ya ibada, “Divine Identity, Becoming, and Belonging,” iliyotolewa Chuo Kikuu cha Brigham Young–Hawaii mnamo Mei 25, 2022.

Muhtasari

  1. APA Dictionary of Psychology, s.v. “belonging,” dictionary.apa.org.

  2. Joanna Cannon, “We All Want to Fit In,” Psychology Today (blog), Julai 13, 2016, psychologytoday.com.

  3. Brené Brown, Daring Greatly: How the Courage to Be Vulnerable Transforms the Way We Live, Love, Parent, and Lead (2015), 231–32.

  4. Kitabu cha Mormoni kinazungumzia wakati ambapo watu, ingawa walikuwa tofauti, waliungana katika Mungu (ona 4 Nefi 1:15–17). Kikundi hiki cha watu kilikumbuka urithi wao wa kiungu, wakaweka utiifu wao Kwake juu ya kingine chochote, wakaishi kwa umoja na upendo kwa wengine, licha ya tofauti za kimaumbile na kimazingira.

  5. Nyumba takatifu ya Mungu pia inatengeneza mazingira ya usawa na kuwa sehemu ya maagano. Zingatia yafuatayo kuhusu uzoefu wetu wa hekaluni: Sote tunaalikwa kujiandaa na kustahili kupata kibali cha kuingia hekaluni. Sote tunavaa mavazi meupe yakiashiria usafi wa jumla na usawa mbele za Mungu. Tunaitana kaka au dada na hatutumii vyeo vyetu vya kawaida vya kidunia. Sote tunapewa fursa sawa za kujifunza. Sote tunapewa ibada na maagano sawa na tunaweza kupokea baraka sawa za milele.

  6. Kati ya watu bilioni 117 waliowahi kuishi katika dunia hii (ona Toshiko Kaneda na Carl Haub, “How Many People Have Ever Lived on Earth?,” Population Reference Bureau, Mei 18, 2021, prb.org/articles/how-many-people-have-ever-lived-on-earth), wachache sana wamepata fursa ya kupata ibada okozi na za kuinuliwa za injili. Kama matokeo, umati mkubwa wa watoto wa Mungu watahitajika kupokea ibada hizi katika ulimwengu wa roho.

  7. Ona Russell M. Nelson, “Acha Mungu Ashinde,” Liahona, Nov. 2020, 92–95.