Mkutano Mkuu
Lakini Hatukuwasikiza
Mkutano mkuu wa Aprili 2022


Lakini Hatukuwasikiza

(1 Nefi 8:33)

Maagano na ibada hutuelekeza kwa na kutusaidia sisi daima kukumbuka uhusiano wetu na Yesu Kristo kadiri tunavyosonga mbele kwenye njia ya agano.

Mke wangu Susan, watoto wetu watatu wa kiume na wake zao, wajukuu wetu wote, na Mzee Quentin L.Cook, mwenzangu katika Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kwa takribani miaka 15, wote wako tayari kutoa ushahidi juu ya ukweli kwamba mimi siimbi vizuri. Lakini licha ya kukosa kwangu kipaji cha sauti, mimi ninapenda kuimba nyimbo za dini za Urejesho. Muunganiko wa mashairi yenye mwongozo wa kiungu na ukuu wa sauti tamu hunisaidia mimi kujifunza kanuni muhimu za injili na huamsha nafsi yangu.

Wimbo mmoja ambao umeyabariki maisha yangu kwa njia za ajabu ni “Let Us All Press On.” Hivi karibuni nimekuwa nikitafakari na kujifunza kuhusu kufungu maalumu cha maneno katika kiitikio cha wimbo huo. “Hatutasikiliza kile waovu wasemacho, bali Bwana pekee tutamtii.”1

Hatutasikiliza.

Niimbapo “Let Us All Press On,” Mara nyingi ninawafikiria watu wale katika ono la Lehi waliokuwa wakisonga mbele kwenye njia iongozayo kwenye mti wa uzima ambao si tu “walishikilia”2 bali walikuwa “wameendelea kuishikilia ile fimbo ya chuma, hadi wakaja mbele, na kuanguka chini na kula lile tunda la mti.”3 Lehi alielezea umati katika jengo kubwa na pana ambao walikuwa wakiwanyoshea “vidole vya madharau kwake [yeye] na wale … waliokuwa wakila tunda.”4 Majibu yake kwa wazomeaji na matusi yao ni makubwa na ya kukumbukwa.“Hatutasikiliza.”5

Ninaomba kwamba Roho Mtakatifu atubariki na kutuangazia kila mmoja wetu tunapozingatia jinsi tunavyoweza kuimarishwa kwa “kutosikiliza” ushawishi mbaya na sauti za kejeli za ulimwengu wa kisasa ambamo sisi tunaishi.

Usisikilize

Neno sikiliza hupendekeza fahamu kuwa au mwangalie fulani au jambo fulani. Hivyo, mashahiri ya wimbo huu “Let Us All Press On” yanatuasa sisi ili tufanye uamuzi thabiti wa kutosikiliza “kile waovu wasemacho.” Na Lehi na watu waliokuwa pamoja naye ambao walikuwa wakila tunda la mti ule wanatoa mfano imara wa kutosikiliza kejeli na madharau ambayo mara wa mara yanatujia kutoka kwenye lile jengo kubwa na pana.

Mafundisho ya Kristo yaliyoandikwa “kwa Roho wa Mungu aliye hai … katika mbao za nyama za [mioyo yetu]”6 huongeza uwezo wetu wa “kutosikiliza” vurugu, dhihaka, na upotoshaji mwingi katika ulimwengu wetu ulioanguka. Kwa mfano, imani inayolenga katika, na juu ya Bwana Yesu Kristo inatukinga sisi kwa nguvu za kiroho. Imani katika Mkombozi ni kanuni ya matendo na yenye nguvu. Tunapotenda katika kulingana na ukweli wa injili Yake, tunabarikiwa kwa kuwa na uwezo wa kiroho wa kusonga mbele kupitia changamoto za duniani wakati tukizingatia zile shangwe ambazo Mwokozi anatupatia sisi. Hakika, “kama tunafanya kile kilicho sahihi hatuhitaji kuogopa, kwani Bwana, msaidizi wetu, daima atakuwa karibu.”7

Uhusiano Binafsi kupitia Maagano

Kuingia katika maagano matakatifu na kwa kustahili kupokea ibada za ukuhani kunatufunga nira sisi pamoja na kutuunganisha na Bwana Yesu Kristo na Baba wa Mbinguni.8 Hii kwa urahisi kabisa inamaanisha kwamba tunatumaini katika Mwokozi kama Mwombezi wetu9 na Mpatanishi10 na tunategemea wema Wake, rehema, na neema11 wakati wa safari yetu ya maisha. Tunapokuwa imara katika kuja kwa Kristo na tukiwa tumefungiwa nira pamoja, sisi tunapokea baraka za utakaso, uponyaji, na baraka za kuimarishwa za Upatanisho Wake usiopimika na wa milele.12

Msimamo wa kuishi na kupenda maagano hujenga uhusiano na Bwana ambao ni wa kina na wa kipekee na ambao unakuwa na nguvu kiroho. Tunapoheshimu masharti ya maagano matakatifu na ibada, pole pole na kwa kuongezeka tunavutwa karibu zaidi na Yeye13 na tunayaona matokeo ya uungu Wake na uhalisia wa kuishi kwake katika maisha yetu. Yesu ndipo anakuja kuwa zaidi kuliko sifa kuu katika hadithi za maandiko matakatifu; mifano Yake na mafundisho Yake yanashawishi kila hamu, wazo na tendo letu.

Hakika sina uwezo wa kuelezea vya kutosha asili halisi na nguvu ya uhusiano wa agano letu na Mwana wa Mungu mfufuka. Lakini ninatoa ushahidi kwamba uhusiano wetu na Yeye na Baba wa Mbinguni ni halisia na ndio chanzo kikuu cha uhakika, amani, shangwe, na nguvu ya kiroho ambayo hutuwezesha sisi “kutokuogopa, hata kama adui anakejeli.”14 Kama wanafunzi wa Yesu Kristo wafanya-maagano na washika-maagano, tunaweza kubarikiwa “kujipa moyo, kwani Bwana yuko upande wetu”15 na tusisikilize ushawishi mbaya na kejeli za walimwengu.

Ninapowatembelea waumini wa Kanisa kote ulimwenguni, mara kwa mara ninawauliza swali hili: kitu gani kinakusaidia wewe “kutosikiliza” ushawishi wa ulimwengu, kejeli, na madharau? Majibu yao yanafundisha zaidi.

Waumini wajasiri mara kwa mara huelezea umuhimu wa kualika nguvu ya Roho Mtakatifu katika maisha yao kupitia mafunzo imara ya maandiko matakatifu, maombi yenye nguvu, na maandalizi sahihi ya kushiriki katika ibada ya sakramenti. Pia kinachotajwa mara kwa mara ni msaada wa kiroho wa washiriki wa familia walio waaminifu, na marafiki wenye kuaminika, masomo muhimu wanayojifunza kupitia kuwatumikia wengine na kuhudumu katika Kanisa lililorejeshwa la Bwana. Na uwezo wa kutambua utupu mkamilifu wa cho chote katika au kinachokuja kutoka kwenye lile jengo kubwa na pana.

Nimedondoa katika majibu haya ya waumini mpangilio fulani ambao ni wa kipekee sana. Kwanza na cha mbele kabisa, wanafunzi hawa wanazo shuhuda imara juu mpango wa furaha juu ya Baba wa Mbinguni na nafasi ya Yesu Kristo kama Mkombozi na Mwokozi wetu. Na cha pili, maarifa yao ya kiroho na usadiki ni wa mtu mmoja mmoja, wa kibinafsi, na maalumu; na sio wa ujumla na kinadharia. Ninawasikiliza viumbe hawa waliojitoa wakiongelea maagano yakiwapa nguvu ya kushinda upinzani na uhusiano wao na Bwana aliye hai ukiwasaidia katika nyakati zote nzuri na mbaya. Kwa watu hawa binafsi, hakika Yesu Kristo ni Mwokozi wao binafsi.

Picha
Dira

Maagano na ibada za injili hufanya kazi katika maisha yetu kama vile dira. Dira ni chombo kitumikacho kuonyesha uelekeo mkuu wa kaskazini, kusini, mashariki, na magharibi kwa madhumuni ya kuongoza njia na maelekezo ya kimazingira. Katika njia kama hiyo, maagano na ibada zetu hutuelekza kwa na kutusaidia sisi daima kukumbuka uhusiano wetu na Yesu Kristo kadiri tunavyosonga mbele kwenye njia ya agano.

Picha
Sanamu ya Kristo

Uelekeo mkuu kwetu sisi sote tukiwa katika mwili huu wenye kufa ni kuja kwa na kukamilishwa katika Kristo.16 Maagano na ibada takatifu zinatusaidia sisi kuendelea kuzingatia kwa Mwokozi na kujitahidi, pamoja na neema Yake,17 kuwa zaidi kama Yeye alivyo. Kwa hakikisho zaidi, “[nguvu] isiyoonekana itanisaidia mimi na wewe katika kazi tukufu ya ukweli.”18

Kushikilia kwa Nguvu Fimbo ya Chuma

Uhusiano wetu wa agano na Mungu na Yesu Kristo ndiyo njia ambayo kupitia kwayo sisi tunaweza kupokea uwezo na nguvu ya “kutosikiliza.” Na mkataba huu unaimarishwa kadiri tunavyoendelea kushikilia kwa nguvu ile fimbo ya chuma. Lakini kama ndugu wa Nefi walivyouliza, “Nini maana ya fimbo ya chuma ambayo baba aliona … ?

“Na [Nefi] akawaambia kwamba ilikuwa neno la Mungu; na yeyote atakayesikiliza hilo neno la Mungu, na alizingatie, hawataangamia; wala majaribu na mishale ya moto ya adui kuwalemea na kuwapofusha, ili kuwaelekeza kwenye maangamizo.”19

Tafadhali tambua kwamba uwezo wa kupinga majaribu na mishale ya moto ya adui umeahidiwa kwa watu binafsi wenye “kushikilia kwa nguvu” kuliko kwa wale wenye “kushikilia” tu neno la Mungu.

Ya kupendeza zaidi, Mtume Yohana anamwelezea Yesu Kristo kama hilo Neno.20

“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. …

“Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. …

“Naye Neno alifanyika mwili, na akakaa kwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana wa pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.”21.

Hivyo basi, moja ya majina ya Yesu Kristo ni “Neno.”22

Kwa nyongeza, makala ya imani ya nane inaeleza, “Tunaamini katika Biblia kuwa ni neno la Mungu alimradi imetafsiriwa kwa usahihi; pia tunaamini Kitabu cha Mormoni kuwa ni neno la Mungu.”23

Hivyo, mafundisho ya Mwokozi, kama yalivyoandikwa katika maandiko matakatifu, pia ni “neno.”

Wacha nipendekeze kwamba kushikilia kwa nguvu neno la Mungu kunahitaji (1) kukumbuka, kuheshimu, na kuimarisha uhusiano binafsi tulionao na Mwokozi na Baba Yake kupitia maagano na ibada za injili ya urejesho, na (2) kwa maombi, kwa dhati, na kwa uaminifu kabisa tumia maandiko matakatifu na mafundisho ya manabii na mitume walio hai kama vyanzo vya uhakika vya ukweli uliofunuliwa. Tunapolazimika na “kushikilia kwa nguvu” kwa Bwana na tunabadilika kwa sababu ya kuishi mafundisho Yake,24 Ninaahidi kwamba mtu mmoja mmoja na kwa pamoja tutabarikiwa ili “tusimame mahali patakatifu, na hatutaondoshwa.”25 Kama tunakaa katika Kristo, na Yeye atakaa ndani yetu na atatembea na pamoja na sisi.26 Hakika, “katika siku za majaribu ya Watakatifu Wake atawatia moyo, na kustawisha ukweli.”27

Ushuhuda

Endeleeni Mbele. Shikilia kwa nguvu. Usisikilize

Ninatoa ushahidi kwamba uaminifu kwenye maagano na ibada za injili ya urejesho ya Mwokozi unatuwezesha kuendelea mbele katika kazi ya Bwana, kwa kushikilia kwa nguvu kwake Yeye kama Neno la Mungu, na tusisikilize vivutio vya adui. Katika kupigania haki, kila mmoja wetu na ashike upanga, hata “upanga imara wa ukweli,”28 katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.