2013
Max na Mia Waokoa Siku
Aprili 2013


Max na Mia Waokoa Siku

Max alijiandaa kucheza shujaa jasiri. Alivaa t-shati yake nyekundu Alivaa kofia yake ya shujaa jasiri. Kisha akaenda chumbani mwa dadake mdogo.

“Njo Mia,” alisema Max. “Twende tukaokoe siku!”

Max na Mia walienda sebuleni. Waliona ndoo imejaa nguo.

“Mtanisaidia?” aliuliza Mama.

“SAWA,” Max akasema. “Kisha twende tukaokoe siku.”

Max na Mia walimsaidia Mama kukunja nguo zote na kuziweka kando.

Kisha Max akaona takataka kiasi kwenye sakafu. “Tuokote takataka zote,” alisema Max. “Kisha twende tukaokoe siku.”

Max na Mia wakashindana kote nyumbani. Wakatupa takataka zote walizoweza kupata.

Walimuona Mama akifagia sakafu ya jikoni “Tunaweza kukusaidia,” Max alisema.

Mia alishikilia kiokota taka Max akifagia sakafu.

“Sasa twende tukaokoe siku,” Max alisema.

Mama alitazama kote katika nyumba safi. Kisha akawakumbatia Max na Mia. “Nafikiri tayari mmeokoa siku!”

Michoro na Elise Black