2013
Simu Ilikatika
Aprili 2013


Simu Ilikatika

Seda Meliksetyan, Armenia

Mnamo Marchi 1997, nilipokuwa nikiishi katika jiji la Russia Rostov-on-Don, mume wangu nami tulibatizwa katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Nilipojifunza mafundisho ya Kanisa, mengi ya maswsali yangu yalijibiwa. Ilikuwa ya kuvutia kujifunza juu ya mpango wa wokovu, ikiwa pamoja na ibada ya ubatizo kwa wafu. Nilishangaa kujifunza kuwa tungeweza kubatizwa kwa niaba ya mababu zetu wafu.

Mwaka baada ya ubatizo wetu, rais wa misheni alitualika kujitayarisha kuenda hekaluni. Kama sehemu ya maandalizi yetu, tulianza kufanya utafiti wa historia ya familia. Siku moja nilipokuwa nikifikiria kuhusu kufanya kazi hii, simu ikapigwa. Ilikuwa ni mama mkwe wangu. Nilimuuliza ikiwa angeweza kunitumia orodha ya mababu wafu upande wa familia ya mume wangu. Alishangaa na kuniambia kuwa ubatizo kwa ajili ya wafu haikuwa fundisho la Kristo lakini badala yake ni kitu Wamormoni walikuwa wametunga. Sikuwa na uhakika jinsi ya kumjibu kwa sababu sikuwa na ufahamu na marejeleo ya maandiko yaliyounga mkono fundisho.

Nilipokuwa nikifikiria jinsi ya kujibu, simu ilikatika. Sikuwa na uhakika kwa muda kile kilichokuwa kimetendeka, lakini nilikata simu na kuenda chumbani mwangu. Nilichukuwa Agano Jipya mkononi mwangu, nikapiga magoti kuomba, na kumuliza Baba wa Mbinguni kunionyesha ni wapi ningalipata jibu.

Mwishoni mwa ombi langu, Nilifungua Bibilia. Nilihisi ni kama mtu alikuwa amenieleza nisome mstari wa 29 wa kurasa ule ule niliokuwa nimefungua. Nilikuwa katika sura ya 15 ya 1 Wakorintho, ambayo inazungumzia fundisho la ubatizo kwa ajili ya wafu.

Nilikuwa nimeguswa na kushangaa kuwa Baba wa Mbinguni alikuwa amejibu maombi yangu kwa wakati huo huo. Ilikuwa ni hisia nzuri.

Nilikuwa nikiwazia kwa kina kuhusu uzoefu huu ambapo kwa ghafla simu ikalia tena. Ilikuwa ni mama mkwe wangu, akiuliza ni kwa nini simu ilikuwa imekatika. Nilimuambia sikuwa najua ni kwa nini lakini nikamuuliza afungue Bibilia yaka na asome 1 Wakorintho 15:29.

Siku chache baadaye orodha ya jamaa marehemu ilikuwa mezani mwangu. Mama mkwe wangu alikuwa amesoma maandiko na sasa aliamini kuwa Mwokozi, kupitia mtume Paulo, alikuwa amefundisha fundisho la ubatizo kwa ajili ya wafu.

Mungu ameahidi baraka kuu kwa wale ambao wanafanya kazi hii ya wokovu. Ninajua hii ni kweli.