2013
Vijana Wamisionari wa Huduma wa Kanisa Wapata Furaha katika Huduma.
Aprili 2013


Vijana Wamisionari wa Huduma wa Kanisa Wapata Furaha katika Huduma

Mzee Ernesto Sarabia alivaa baji nyeusi ya umisionari kila siku ya misheni yake. Lakini misheni yake ilikuwa tofauti na ya watu wengine wengi—Mzee Sarabia alihudumu kama Vijana Wamisionari wa Huduma ya Kanisa (VMHK) katika ofisi ya Misheni ya Mexico Hermosillo.

Tunatambua kwamba huenda kuwa si busara kwa baadhi ya vijana wetu na wasichana kukabiliana na ugumu na changamoto za misheni ya muda, Mzee M. Russell Ballard wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili amesema. Lakini hii, alisema, haimaanishi hawawezi kushiriki katika baraka za huduma za umisionari (“One More”, Liahona, Mei 2005, 69).

Mzee Russell M. Nelson wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili, alisema, Kuhudumu misheni ni kitendo cha huduma ya kujitolea kwa Mungu na wanadamu (“Ask the Missionaries! They Can Help You!” Liahona, Nov. 2012, 18), na kuna njia nyingi za kutoa huduma hio.

Kwa wale ambao wamekubaliwa kwa heshima kutohudumu misheni ya kuhubiri ya muda, ama kwa wale ambao ni lazima warudi nyumbani mapema, mpango ya VMHK unaweza kutoa uzoefu wa maana wa misheni.

Mahitaji ya Kuhudumu

Wa VMHK ni lazima wawe na uwezo wa kimwili, kiakili, kiroho, na kihisia ili kutekeleza kazi za wito wao, ambao wanalinganishwa kwa makini.

Kazi ya VMHK inakuwa kutoka miezi 6 hadi 24 na inaweza kuwa na anuwai kuanzia kuhudumu kwa siku kadhaa za wiki hadi kufanya kazi kwa muda mzima. Kuna nafasi za kuhudumu katika jamii na pia kutoka nyumbani. Uwezekano wa kazi za VMHK inajumuisha utafiti wa historia ya familia, teknologia ya habari, wasaidizi wa ofisi ya misheni, hifadhi za askofu, na zaidi.

Uhimili wa Familia na Ukuhani

Wazazi, viongozi wa ukuhani, na washiriki wa Kanisa wanaweza kusaidia wa VMHK kujiandaa kutumikia misheni.

Familia changa ya Dada Eliza Joy Young imekuwa msaada wa nguvu kwake, kumwendesha kwa gari hadi na kutoka ofisi za Kanisa katika Sydney, Australia.

Mzee Michael Hillam, ambaye anafanya kazi katika Kituo cha Usambazaji cha Hong Kong, alisema, “Walimu wangu wa seminari ya asubuhi mapema na viongozi wa Wavulana hunisaidia kujiandaa.”

Dhabihu Huleta Baraka

Dada Young alijitolea siku zake za mapumziko kutokana na ajira yake ili kuhudumu Misheni ya Huduma ya Kanisa. Alisema, “Najisikia karibu na Baba yangu wa Mbinguni nikijua kwamba ninamsaidia.”

Kama ziada ya baraka za kiroho, kuhudumu misheni ya Huduma ya Kanisa huwapa wamisionari vijana fursa muhimu ya kijamii na kitaaluma. “Misheni yangu imenionyesha kwamba ninaweza kufanya kazi katika ajira ya huria,” Dada Young alisema. (Alikuwa awali amefanya kazi tu katika ajira ya kusaidiwa.)

Ingawa si vijana wote wazima ambao wangependa kuhudumu wanaweza, juhudi kubwa zinafanywa kuweza kuchukua kila kijana mzima mwenye kustahili. Wavulana na wasichana ambao wangependa kuhudumu katika njia hii wanaweza kuongea na askofu wao ama rais wa tawi, ambaye anaweza kupata fursa mwafaka kwa ajili yao.

Soma zaidi katika news.lds.org young church-service missionaries.