2013
Kupata Furaha Maishani
Aprili 2013


Kupata Furaha Maishani

Karen Rockwood, Idaho, USA

Katika wakati mmoja nilikuwa nikisoma hotuba ya mkutano mkuu ya Mzee Richard G. Scott wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili. Ingawa nilikuwa nimesikiza na kusoma hotuba hii awali, fungu moja lilinivutia na kubaki katika mawazo yangu.

Masaa machache baadaye mwana wangu, aliyekuwa akiishi katika fleti na marafiki, akaja matembezi. Alikuwa amehudumu katika misheni ya muda na kushiriki katika semesta chache za chuo. Alikuwa hana uhakika wa mwelekeo upi elimu angechukua na njia gani ya kazi angefuatilia. Kwa sababu alikuwa amechoshwa na kuhisi kuwa shule, kwa sasa, ilikuwa ni kupoteza wakati na pesa, alikatiza masomo yake na kuanza kufanya kazi kwa muda kamilifu.

Aliniambia kuwa mmoja wa marafiki zake alikuwa amependekeza kuwa waende katika kisiwa kule Bahamas ama Karebiani, wapate ajira, na kufurahia kwa miezi michache. Mwanagu alikuwa amefurahia kuhusu matarajio. Ningeona kwa urahisi jinsi uzoefu kama huo usio na kujali ungekuwa wa kuvutia kwa kijana mvulana.

Hapo tu, ujumbe wa Mzee Scott wa busara ukanijia akilini. Nilichukua Ensign na kumsomea mwanagu yafuatayo: “Uko hapa duniani kwa lengo tukufu. Si kuburudishwa bila msimamo ama kuwa daima katika kufuatilia anasa wakati wote. Uko hapa kujaribiwa, kujidhibitisha ili uweze kupokea baraka za ziada Mungu alizonazo kwa ajili yako. Athari ya kupunguza makali ya uvumilivu inahitajika”, (Finding Joy in Life, Ensign, Mai 1996, 25).

Bila neno, mwanangu alilichukua jarida, akatembea mbali, na kusoma hotuba yote. Baadaye yote aliyosema ilikuwa kuwa hangeendelea katika safari yake ya kisiwani.

Kwa muda aliingia katika akademi ya polisi, njia iliomwelekeza kwa mke wake wa siku za usoni. Walioana katika Hekalu la Mesa Arizona na leo wanalea watoto watatu wazuri. Mnamo 2012 mwanagu alimaliza shahada yake ya kwanza na kwa kweli “anapata furaha maishani.”

Safari iliyopendekezwa ya mwanagu ingekuwa uzoefu mzuri, kwa upande mwingine, ingeweza kuwa hatari ya kiroho. Kila wakati ninapotafakari tukio hili, Roho hugusa moyo wangu.

Ninashukuru kwa ajili ya maneno ya manabii na kuwa nilishawishiwa kukumbuka hotuba ambayo ilinisaidia kutoa mwongozo. Ninashukuru pia kuwa mwanangu alisikiliza mjumbe wa Bwana na kukubali Roho kumshawishi. Ninajua kuwa baraka nyingi na huruma huja tunaposikiliza na kufuata mafundisho ya Mwokozi na watumishi Wake.