2013
Maoni
Aprili 2013


Maoni

Roho Mtakatifu Hunifundisha Mimi

Tangu familia yangu kujiunga na Kanisa, nimeona nguvu inayokuja kutokana na kusoma Liahona. Ni kupitia maneno haya ya kina ndio kwamba nilishawishika kuhudumu misheni. Mada nyingi hujadiliwa katika gazeti, lakini kinachojalisha kwangu ni yale ambayo Roho Mtakatifu hunifundisha kila wakati ninapokisoma. Hakika, tutakuwa huru—hata katika “eneo la adui” (ona Boyd K. Packer, “How to Survive in Enemy Territory,” Liahona, Oct. 2012, 24)—tunapojifunza, tunaposoma, na kutumia kanuni zinazofundishwa. Mwokozi yu hai, ukuhani u duniani, na Mungu yu mbinguni.

Newton T. Senyange, Uganda

Marekebisho

Oktoba 2012 Liahona kimakosa ilihusisha picha katika hadithi “First Stake in India Organized” kwenye kurasa 76–77. Picha zilipigwa na Dada Gladys Wigg. Tunaomba radhi kwa makosa.

Katika Liahona, ya Desemba 2012 familia ya Vigil, iliojadiliwa katika makala “Sacred Transformations” katika ukurasa wa 36, ilibatizwa mnamo Julai 2010, si Juni 2011. Pia, Andrea Vigil alizaliwa mnamo Julai, si Agosti, 2012.

Katika Teachings of Presidents of the Church: Lorenzo Snow, picha katika ukurasa wa 2 imepatiwa jina lisilo sawa. Ni picha ya mwanawe Rais Snow, Oliver Goddard Snow. Pia, katika maelezo mafupi kwenye ukurasa wa 28 majina ya Brigham Young Jr. na Francis M. Lyman yanapaswa kubadilishwa.