2013
Roho Mtakatifu Afariji, Huhamasisha na Hushuhudia
Aprili 2013


Kile Tunachoamini

Roho Mtakatifu HUFARIJI, Huhamasisha na Hushuhudia

Kipawa cha Roho Mtakatifu ni mojawapo wa baraka kubwa tunaweza kupokea katika maisha haya, kwa kuwa Roho Mtakatifu, huhamasisha, hutuonya, hututakasa, na hutuongoza. Anaweza kutujaza na “tumaini na upendo kamili” (Moroni 8:26). Hufundisha “ukweli wa vitu vyote” (Moroni 10:5). Sisi hupokea ufunuo na vipawa vya kiroho kutoka kwa Mungu kupitia Roho Mtakatifu. Muhimu zaidi, sisi hupokea shuhuda zetu za Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kupitia Roho Mtakatifu.

Kabla ubatizwe, ungehisi Roho Mtakatifu mara kwa mara. Lakini tu kwa kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu baada ya kubatizwa kwako ndipo ungeweza kufurahia uenzi wa kudumu wa Roho Mtakatifu, mradi unastahili. Kipawa hicho kilipeanwa na mwenye Ukuhani wa Melkezediki kwa kuwekelea mikono (ona Matendo 19:6; M&M 33:15). Kila Sabato kufuatia, unaweza kufanya upya maagano yako ya ubatizo unapopokea sakramenti na hivyo kupokea baraka ya Bwana kuwa unaweza “daima kuwa na Roho Wake” kuwa pamoja nawe (M&M 20:77).

Roho Mtakatifu, kwa mara nyingi anajulikana kama Roho, ni mshiriki wa tatu wa Uungu. Nabi Joseph Smith alifundisha: “Baba ana mwili wa nyama na mifupa wenye kushikika kama wa mwanadamu; Mwana vile vile; lakini Roho Mtakatifu hana mwili wa nyama na mifupa, lakini ni mtu wa Kiroho. Kama isingekuwa hivyo, Roho Mtakatifu asingeweza kukaa ndani yetu” (M&M 130:22).

“Kwa sababu Roho wa Bwana haishi kwenye mahekalu yasio matakatifu” (Helamani 4:24), lazima tuwa wastahiki wa uenzi Wake. Tunafanya hivyo na, miongoni mwa mambo mengine, kuwa na mawazo mema, kuishi kwa uadilifu, na kutaka kutii amri.

Baada ya kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, tunaweza kufanya mambo mengi kualika ushawishi Wake katika maisha yetu:

  • Omba.

  • Jifunze maandiko.

  • Kushiriki katika sacramenti kwa ustahiki.

  • Kuabudu Hekaluni.

  • Tazama vyombo safi vya habari, tumia lugha safi, na kuwa na mawazo mema.

Kielelezo kwa picha na Christina Smith, Eve Tuft, Cody Bell, na Matthew Reier