2013
Kuitikia Wito kwa Wamisionari Zaidi: Kukuza Mawazo ya Umisionari Nyumbani na katika Kanisa
Aprili 2013


Kuitikia Wito kwa Wamisionari Zaidi: Kukuza Mawazo ya Umisionari Nyumbani na katika Kanisa

Askofu Victor Nogales wa kata ya Parque Chacabuco, kigingi cha Buenos Aires Argentina Congreso ameketi mbele ya ubao ya matangazo akiwa amefunikwa na picha za wavulana na wasichana 37 katika kata yake. Wakati mmoja wao anaondoka kuenda misheni, yeye huandika maneno kando ya picha.

Vijana wangu hufurahia wanapokuja ofisini mwangu na kuona picha na maneno, alisema. Inawatia moyo kujitayarisha kwa ajili ya misheni zao wenyewe.

Kata hii katika Buenos Aires inaelekeza roho ya kazi ya umisionari. Katika miezi sita za kwanza ya 2012, vijana 19—14 wakiwa waongofu—waliwacha nyumba zao ili kuhudumu misheni ya muda katika mataifa nane. Zaidi ya asilimia 80 ya vijana wanaostahili wamejitolea kuhudumu misheni.

Katika miaka ya hivi majuzi viongozi wa Kanisa wametoa maombi kadhaa kwamba vijana wengi zaidi wahudumu misheni.

Wakati wa mkutano mkuu wa Aprili 2005, punde tu baada ya Kanisa kutoa Hubiri Injili Yangu: Mwongozo wa Huduma ya Umisionari, Mzee M. Russell Ballard wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili alishauri familia na viongozi kukuza roho ya umisionari na kuandaa wavulana na wasichana zaidi kumtumikia kwa heshima kwa kuwasaidia kuelewa wao ni nani na kwa kuwafundisha mafundisho (ona “One More,” Liahona, Mai 2005, 69).

Tangazo la Rais Thomas S. Monson wakati wa mkutano mkuu wa Oktoba 2012 kwamba mipaka ya umri ya umisionari ingepunguzwa lilifanyanyika kama ukumbusho mwingine kuwa Bwana anaharakisha kazi Yake.

Leo familia nyingi na viongozi wengi wa Kanisa wanachukulia ujumbe huu moyoni na kuanzisha desturi nzuri ya huduma ya umisionari katika maeneo yao.

Kuwasiadia Vijana Kuelewa Wao ni Kina Nani

Kwa kujibu swali hili, Umewezaje kuwatayarisha vijana wengi kuwa tayari kuhudumu? Askofu Nogales alijibu, Nilipoitwa kama askofu, jambo la muhimu la kwanza lilikuwa vijana wa kata yangu, na niliifanya kuwa wazi kwa viongozi wengine wa kata kwamba tulihitajika kuwa sehemu ya maisha yao.

Kwa mfano, kila mmisionari wa Chacabuco alikuwa na wito katika kata kabla ya kuondoka kwao. Mara nyingi waongofu wapya na washiriki wasioshiriki kikamilifu walialikwa kuhudumu kama walimu, jambo ambalo liliwasaidia kujitayarisha kufundisha injili.

Askofu Nogales pia alipangia vijana kujiandaa kiroho kwa ajili ya misheni kwa kufanya kazi pamoja na wamisionari wa muda wa kwao.

Viongozi wa Kanisa na washiriki wanavyojitolea wenyewe kwa ajili ya vijana wa kata, wamezawadiwa kwa kuona roho ya umisionari ikikua sana.

Familia Yenye Wazo ya Umisionari

Garth na Eloise Andrus wa Draper, Utah, Marekani, wanajua inamaanisha nini kuwa na familia yenye wazo la umisionari. Wao wana wajukuu 17 ambao wameshiriki misheni, na wameshiriki misheni sita wao wenyewe.

Kukuza roho ya huduma ya umisionari katika familia yako ni kitu ambacho huanza kutoka wakati watoto ni wadogo, Ndugu Andrus alisema.

Dada Andrus alikubali. Hauwachi kushiriki misheni kuwa matarajio ya kimya, lakini unawazungumzia watoto wako na wajukuu kuihusu ni kama vile swali ni—wakati gani utaenda misheni yako, si kama alisema.

Kufundisha vijana wao ni kina nani kwa kuweka mfano wa huduma ya umisionari ni muhimu pia. Ndugu na Dada Andrus walipokea wito wao wa kwanza mnamo 1980, punde tu mtoto wao mdogo alipokuwa akiondoka kuenda misheni yake.

Mjukuu moja aliwandikia baada ya kupokea zawadi waliomtumia kumsaidia kujiandaa kwa ajili ya misheni yake. “Alituomba [zawadi], lakini akasema, ‘Ya muhimu zaidi ni kuwashukuru kwa mfano ambao mmeweka,’” Dada Andrus alisema.

Kufundisha Mafundisho

“Vijana wetu wana haki ya kutarajia kwamba wazazi wao na viongozi wa Kanisa na walimu watahakikisha kwamba wanajua na kuelewa injili ya Yesu Kristo,” Mzee Ballard alisema. “Roho Mtakatifu atathibitisha ukweli kwa mioyo yao, na atawasha Nuru ya Kristo katika roho zao. Na kisha utakuwa na mmisionari moja zaidi ambaye atakuwa tayari kikamilifu” (M. Russell Ballard, “One More”, 71).

Maili 6000 (9600 km) kutoka Buenos Aires, tawi la kijijini la Horseshoe Bend karibu na Boise, Idaho, Marekani, pia limeshuhudia ongezeko kubwa la huduma ya umisionari wakati familia na viongozi wakiweka mkazo juhudi za kufundisha injili kwa vijana wao.

Kutoka tawi dogo la washiriki 75, vijana tisa wanahudumu misheni.

Mzee Russell M. Nelson wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili alisisitiza sababu na faida ya kuhudumu. “Wamisionari wote hutumikia kwa matumaini ya pekee ya kufanya maisha yawe bora kwa watu wengine alisema. Uamuzi wa kuhudumu misheni utajenga hatima ya kiroho ya mmisionari, mume au mke wake na dhuria zao kwa vizazi vijavyo. Hamu ya kuhudumu ni matokeo asili ya uongofu wa mtu, ustahili, na maandalizi” (“Ask the Missionaries! They Can Help You!” Liahona, Nov. 2012, 18).

Martin Walker, rais wa kigingi cha Emmett Idaho, alikubali. Kuhudumu katika misheni humweka kijana katika njia ambayo itaathiri vizazi, alisema. Kama kigingi, tunafanya kila kitu tunachoweza ili kuwatayarisha vijana kwa ajili ya huduma ya umisionari.

Sehemu ya maandalizi hayo inajumuisha kuwafunza vijana mafundisho. Vijana katika tawi la Horseshoe Bend wana darasa la kila wiki la maandalizi ya umisionari linalofundishwa na rais wa zamani wa misheni—mafunzo ambayo yanajaliza mafunzo yaliyotolewa na mkutano wa kigingi wa kila mwezi wa vijana wa maandalizi ya umisionari na Kambi yake ya kila mwaka ya Ukuhani ya Haruni.

LaRene Adam—mmoja wa watoto sita wa Ndugu na Dada Andrus—alihudumu pamoja na mmewe, Jim, katika Misheni ya Copenhagen Denmark kutoka 2007 hadi 2009. Yeye alishuhudia umuhimu wa kuwafundisha watoto injili nyumbani.

“Mojawapo wa mambo makuu unayoweza kufanya ili kuwasaidia watoto wako kujenga ushuhuda wa kazi ya umisionari ni kufanya mkutano wako wa jioni ya familia nyumbani na kujifundisha maandiko na familia,” alisema. “Ukiwapa msingi huo dhabiti wa kujifundisha injili na ufahamu wa injili, wanakuwa tayari zaidi na wanajua mengi zaidi kuhusu Injili.”

Askofu Victor Nogales anasimama karibu na ubao wa matangazo ambao unaonyesha vijana wote wa kata yake, ikiwa ni pamoja na wale ambao kwa sasa wanahudumu misheni.

Picha kwa hisani ya Paul L. Garvin