2013
Mahali ambapo Kanisa Lilianzishwa
Aprili 2013


Katika Njia

Mahali ambapo Kanisa Lilianzishwa

Kuja pamoja nasi kugundua mahali pa umuhimu katika historia ya Kanisa!

Kama Maggie na Lily E. wanataka kuona pale ambapo ambapo Kanisa lilianzishwa kwa mara ya kwanza, hawafai kuangalia mbali sana. Ni hapo tu mlangoni mwa kanisa katika Fayette, New York, ambapo wanaenda kanisani kila Jumapili!

Kanisa halikuanzishwa katika jengo la kanisa, lakini katika nyumba la mbao. Nabii Joseph Smith alikuwa amekuja kukaa hupo na familia ya Whitmer mnamo 1829. Nyumba ya asili haisimami tena, lakini chumba hiki cha mbao kipo mahali pale pale.

Jengo la kanisa ambapo Maggie na Lily huenda kanisani lina kituo cha wageni na maonyesho kuhusu nyumba ya Whitmer na mambo maalum ambayo yalitendeka hapo.

1. Joseph Smith alimaliza kutafsiri Kitabu cha Mormoni hapa.

2. Nje, si mbali na nyumba, wanaume watatu walimuona malaika Moroni na mabamba ya dhahabu. Wanaitwa Mashahidi Watatu kwa sababu walishuhudia, au kuona, mabamba. Unaweza kupata ushahidi wao mbele ya Kitabu cha Mormoni.

3. Mnamo Aprili 6, 1830, takriban watu 60 walikuja kwenye mkutano maalum. Joseph Smith alianzisha rasmi Kanisa, na sakramenti ilibarikiwa na kupitishwa. Huu ulikuwa ya mkutano wa kwanza wa sakramenti!

4. Mara tu baada ya mkutano, wazazi wa Joseph Smith na watu kadhaa wengine walibatizwa nje.

Picha na Brent Walton; vielelezo na Robert T. Barrett © IRI; Uanzilishi wa Kanisa, na Robert T. Barrett, haiwezi kunakiliwa