2013
Kuwasaidia Watoto Kujitayarisha kwa ajili ya Ubatizo
Aprili 2013


Kuwasaidia WatotoKujitayarisha kwa ajili ya Ubatizo

Utotoni ni msimu wa vitu vya mara ya kwanza vya furaha. Mara ya kwanza kuendesha baiskeli, kuenda shuleni, au kujaribu chakula kipya ni baadhi ya matukio ya furaha yanayounda maisha ya mtoto. Kama watu wazima tuko na nafasi ya kuwasaidia watoto kwenye njia ya kugundua. Kama watu wazima Kanisani, tunayo pia nafasi ya kuwasaidia kukua katika injili (ona M&M 68:25). Tunaweza kufanya nini kuhakikisha ubatizo wa mtoto—agano la kwanza mtu hufanya na Baba yetu mpendwa wa Mbinguni—ni tukio la kupendeza na la maana?

“Ni lengo la msingi la Kanisa hili kufundisha vijana: kwanza nyumbani kisha kanisani,” alifundisha Rais Boyd K. Packer.1

Katika mifano ifuatayo, wazazi wanashiriki jinsi walivyowatayarisha watoto wao kwa ajili ya maagizo na maagano ya ubatizo na uthibitisho.

Sisi Huanza Mapema

“Mwaka ambao kila mtoto anafika miaka saba ni wakati wa kusherekea,” asema Lori, mama ya watoto wanne. Yeye na bwanake huwafundisha watoto wao kuhusu ubatizo kutoka siku wanapozaliwa. Hata hivyo, wakati kila mtoto hufika miaka saba, familia yao huanza matayarisho ya kipekee zaidi. Wao huwa na somo la Mkutano wa Jioni wa familia nyumbani kila mwezi kuhusu mada tofauti zinazohusiana na ubatizo, kama vila maagano na mfano wa Yesu.

Lori anasema kuwa masomo katika mwezi wa kuzaliwa wa mwaka ya nane ya watoto huwa nyeti zaidi. Huwa anawaonyesha watoto nguo walizovaa walipopokea jina na baraka, na huzungumuzia siku ambayo agizo hilo lilifanywa.

“Ni wakati bora wa kulenga baraka za maagano ya hekalu,” Lori anangazia. “Sisi huhakikisha kila mara kuwa tunafundisha kuwa chaguo la kubatizwa ni hatua ya kwanza katika kujitayarisha kwa ajili ya baraka za hekalu.”

Sisi Huifanya kuwa Shughuli ya Familia

Monica, Mama ya watoto wanne, anapendekeza kuwashughulisha watoto wakubwa kiasi katika kuwasaidia ndugu zao wadogo kujitayarisha panapowezekana. “Kuwasikia ndugu au dada yao kijana akishuhudia na kushiriki uzoefu wake kwa kweli huongeza nguvu,” anasema. Lori huongeza kuwa wakati mwingine wao huuliza watoto wanaojitayarisha kwa ajili ya ubatizo kufundisha yale waliyojifunza kwa ndugu zao wadogo.

Sisi Huitumia kama Kifaa cha Umisionari

Wakati binti wa Daniel alipofika miaka nane, alijua kuwa angetaka kushiriki siku yake ya ubatizo na marafiki wasiowashiriki wa Kanisa. Hivyo basi familia iliamua kuwaalika marafiki kutoka shuleni na ujirani kwa ubatizo wa Allison. Marafiki hawa waliombwa waje na mistari ya Bibilia wanayopenda katika ubatizo. Baada ya ubatizo, Allison aliweka mstari kwenye vifungu katika jozi la maandiko yake mapya na akaandika majina ya marafiki wake kwenye ukingo.

“Ndio, kama familia yake, tulishughulika kabisa siku hiyo. Lakini tulimkubalisha pia kuwa na marafiki baadaye kwa muda na kuzungumza nao kuhusu kile alichohisi,” Daniel alisema. “Ilikuwa wakati mzuri sana kuona mtoto wetu akiweka mfano.”

Sisi Hufanya zoezi la Mahojiano ya Askofu

Kimberly, mama wa watoto wanaokaribia umri wa kubatizwa, anakumbuka akitembea katika ofisi ya askofu kwa ajili ya mahojiano yake ya ubatizo alipokuwa na umri wa miaka nane. “Nilikuwa na wasi wasi sana!” Kimberly anasema.

Sasa yeye hujaribu kuhakikisha kuwa watoto wake hawakumbani na hisia za wasi wasi. Yeye na bwanake huzungumza na watoto wao kuhusu mahojiano ya askofu na kuwauliza maswali kuhusu ubatizo katika maandhari kama ya mahojiano. Mahojiano haya hufanya zaidi ya kuwafahamisha watoto na mpangilio wa mahojiano — huwa pia yanawahimiza watoto kufikiria kwa kina kuhusu kile agizo la ubatizo linamaanisha kwao.

Tuko na Nafasi Mzuri

Wazazi hawa kwa upesi huashiria kuwa hawajafanya chochote vya kupindukia katika kuwatayarisha watoto wao kwa ajili ya ubatizo na udhibitisho, lakini wengi wao walitumia maneno kama “kamili” na “dhabiti” kueleza masomo ambayo walifundisha kwa miaka iliyopita. “Tulihakikisha kuwa watoto wetu walifahamu kuwa hii ilikuwa hatua muhimu maishani mwao, na kuwa ilikuwa ni jambo kubwa,” Kimberly asema. Tulihakikisha kila mara kuwa tulikuwa wenye kuwatayarisha, na si tu kuwa na tumaini kuwa walimu wao wa Msingi walikuwa wakiwafunza.”

Ni nafasi nzuri vipi tumepewa kusaidia kuwatayarisha watoto tunaopenda kwa ajili ya ubatizo na udhibitisho! Tunapofanya hivyo kwa maombi, Bwana atakuwa nasi kufanyiza uzoefu huu wa kwanza wa kufanya agizo kuwa msingi mkuu wa ukuaji wa kiroho kwa siku za usoni.

Muhtasari

  1. Boyd K. Packer, “Teach the Children,” Liahona, May 2000, 16.

Kielelezo cha picha na John Luke, Craig Dimond, na Cody Bell