2013
Shauriana na Bwana
Aprili 2013


Shauriana na Bwana

Eduardo Oliveira, Ceará, Brazil

Nilipokuwa na umri wa miaka 15, nilimpenda msichana katika darasa langu shuleni na nilitaka kumpatia miadi. Alikuwa mrembo, lakini nilijiuliza kama ninapaswa kumuliza awe nami kabla ya kuwa na umri wa miaka 16. Nilikumbuka Alma 37:37, ambayo inasema, “Shauriana na Bwana kwenye matendo yako yote, na atakuongoza kwa yale mema.” Nikafanya hivyo. Niliomba na kusubiri siku kadhaa kwa jibu la Bwana kabla ya kufanya uamuzi.

Siku moja kanisani, Askofu wangu aliniita katika chumba na kunialika kutoa hotuba Jumapili ijayo. Fikiria mada ilikuwa gani? Usifanye miadi mpaka uwe angalau umri wa miaka 16. Nilihisi kuwa hii ilikuwa jibu la Bwana kwangu, na ilikuwa ni hapana. Ningewezaje kufundisha kitu ambacho sikuwa ninafanya?

Kwa sababu nilikuwa nimeushauriana na Bwana, niliweza kujifunza mapenzi ya Bwana kwa ajili ya maisha yangu na pia kuyakimbia majaribu. Najua kwamba tukishauriana na Bwana, Yeye atatuambia mapenzi Yake na tutabarikiwa sana.