2013
Wiki ya Pasaka
Aprili 2013


Wiki ya Pasaka

Mwokozi wetu Yesu Kristo alitekeleza Upatanisho—ambao ulijumuhisha mateso Yake Gethsemani, Usulubisho Wake kule Golgotha, na Ufufuo Wake kutoka kaburini—wiki ya mwisho ya maisha Yake.

Katika Baraza kule Mbinguni kabla dunia kuumbwa, Baba wa Mbinguni alitupa mpango Wake kwa ajili yetu, watoto Wake. Tulipiga kelele kwa furaha wakati Baba wa Mbinguni alimchagua Yesu Kristo kutekeleza mpango wa wokovu (ona Ayubu 38:7 na Ibrahimu 3:27). Akiwa amezaliwa na Maria kule Bethlehemu, Yesu aliishi maisha bila dhambi. Kwa sababu ya Upatanisho Wake, tunaweza kurudi kuishi na Baba yetu wa Mbinguni na kupokea uzima wa milele. Yesu Kristo atarudi tena kwa nguvu na utukufu kuishi duniani wakati wa Mileniumu, na atasimama kama Hakimu wa kila mtu siku ya mwisho.

Zifuatazo ni picha kutoka kwa video za Bibilia ambazo zinaeleza wiki ya mwisho ya maisha ya Mwokozi. Zingatia kusoma mistari ya maandiko iliyoorodheshwa kwa ajili ya kila picha. Kwa wendo wa kina wa kila tukio, rejelea upatanifu wa Injili nne katika Kamusi ya Bibilia, au Mwongozo wa Maandiko. Video za Bibilia zinapatikana biblevideos.lds.org.

Picha

Siku ya tano kabla ya Pasaka, Yesu alibebwa kuingia Yerusalemu kwenye punda kama ilivyotabiriwa. Watu walimtambua Yeye kama Mfalme wao, wakashangilia “Hosana” na kuweka nguo zao na matawi ya kuti ardhini mbele ya punda. (Ona Mathayo 21:1–11; Marko 11:1–11; Zekaria 9:9.)

Picha © IRI

Picha

Kwa mara ya pili wakati wa huduma Yake duniani, Yesu alisafisha kitala cha hekalu. “Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi,” aliwaambia wabadili pesa (Mathayo 21:13). Kisha wengi wa walio vipofu na walemavu wakaja Kwake hekaluni, na akawaponya. Lakini makuhani wakuu na waandishi walipoona miujiza Yake, walikuwa na hasira na wakatafuta njia ya kumwangamiza Yeye. (Ona Mathayo 21:12–17; Marko 11:15–19.)

Picha © IRI

Picha

Yesu Kristo, Mwana wa Pekee wa Baba, alijishusha hadhi kuja duniani kuokoa kila mtu kutokana na Kuanguka. (Ona 1 Nefi 11:16–22, 26–33; Alma 7:10–13.)

Picha © IRI

Picha

Wiki nzima, Mwokozi alitoa baadhi ya hotuba Zake za kukumbukwa, ikiwa mafundisho Yake juu ya senti ya mjane. (Ona Marko 12:41–44; Luka 21:1–4.)

Picha © IRI

Picha

Katika Bustani la Gethsemani, Mwokozi alipiga magoti na kuomba, mateso Yake kwa ajili ya dhambi ya dunia kusababisha Yeye “kutetemeka kwa sababu ya maumivu, na kutoka damu kwenye kila kinyweleo, na kuteseka mwili na roho” (M&M 19:18). Punde Yuda Eskariota na mkusanyiko wa watu waliojiami walimkamata Yesu, na wanafunzi wote wakamwacha Bwana na kutoroka. (Ona Mathayo 26:36–56; Marko 14:32–50; Luka 22:39–53.)

Picha © IRI

Picha

Wakati wa chakula Chake cha mwisho, Yesu aliwaahidi mitume Wake kuwa wangepokea Mfariji, au Roho Mtakatifu, atakapokuwa ameenda. Aliwafundisha kumkumbuka kwa kupokea sakramenti. Mwishoni mwa usiku, Yesu alitoa Ombi la Upatanishi, ambapo aliomba kuwa wanafunzi waweza kuwa na umoja. (Ona Mathayo 26:17–30; Marko 14:12–26; Luka 22:14–32; Yohana 13–17.)

Picha © IRI

Picha

Baada ya jaribio lisiohalali na mateso mabaya, Yesu Kristo alijitolea Mwenyewe kusulubiwa, akikamilisha “dhabihu kubwa na ya mwisho” iliyowezesha wokovu kwa watoto wote wa Mungu (ona Alma 34:14–15). Kabla ya giza kufika, wafuasi wa Yesu waliutoa mwili Wake msalabani, wakamvalisha kwa nguo ya kitani na vikolezo, na kumweka kaburini. (Ona Mathayo 27; Luka 23; Marko 15; Yohana 19.)

Picha © IRI

Picha

Asubuhi ya Jumapili ikapambazuka, na Maria Magdalena na wanawake wengine waaminifu wakafika kwenye kaburi kuupaka mafuta mwili wa Yesu zaidi. Walilipata jiwe la kaburi limetolewa na malaika wawili waliotangaza habari ya furaha: “Hayupo hapa, kwani amefufuka” (Mathayo 28:6). Mwokozi aliyefufuka alikuwa ameshinda kifo cha kimwili na kutuwezesha sisi sote kuishi tena: “Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa” (1 Wakorintho 15:22). (Ona Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20).

Picha © IRI