2013
Mawazo ya Mkutano wa Jioni wa familia nyumbani
Aprili 2013


Mawazo ya Mkutano wa Jioni ya Familia Nyumbani

Toleo hili lina makala na shughuli ambazo zinaweza kutumika kwa ajili ya jioni ya familia nyumbani ifuatayo ni mifano michache.

“Wito na Huduma ya Yesu Kristo,” ukurasa 18: Elder Russell M. Nelson ashiriki masuala matano ya maisha ya Yesu Kristo ambayo tunaweza kuiga. Zingatia kujadili masuala haya na jinsi ya kuyatumia maishani mwenu. Ungetaka kusoma hadithi ya maandiko kutoka kwa maisha ya Mwokozi ama kutazama video ya Bibilia (biblevideos.lds.org) ambayo inaonyesha mojawapo wa masuala hayo. Unaweza kuhitimisha kwa kutoa ushuhuda wa maisha Yake na huduma na kuimba “More Holiness Give Me” (Hymns, no. 131).

“Je, ni nani Rafiki wa Kweli?” ukurasa 52: Ungetaka kuanza kwa kuuliza, ni nani rafiki wa kweli? Soma fasili ya Mzee Robert D. Hales na jadili tunapaswa kuwa na rafiki wa aina gani. Zingatia kuelezea tokeo la wakati ambao mtu alikutendea kama rafiki wa kweli, na zungumzia sifa ambazo zinaweza kusaidia wanafamilia kuwa marafiki bora kwa wengine.

“Kusherehekea Mahekalu!” ukurasa 62: Pamoja na familia yako, tazama picha za njia tofauti watoto wamesherehekea mahekalu. Zingatia kuonyesha picha ya hekalu lililo karibu nanyi na kuzungumza kuhusu sababu mahekalu ni muhimu. Himiza kuwa katika hekalu peke yake ndiko familia zinaweza kuunganishwa. Ungependa kumaliza kwa kuimba “Families Can Be Together Forever” (ukurasa 65).

Katika Lugha Yako

Liahona na nyenzo zingine za kanisa zinapatikana katika lugha nyingi katika languages.lds.org.

Kielelezo kwa Picha na Cody Bell © IRI