2013
Kitu Kilikuwa Kibaya na Ndege Yangu
Aprili 2013


Kitu Kilikuwa Kibaya na Ndege Yangu

Craig Willie, Utah, USA

Jioni moja nilipokuwa nikiendesha ndege yangu ililojaa abiria kwenye barabara ya ndege, nilikuwa na hisia kuwa kitu kilikuwa kibaya na mfumo wa steringi ya ndege. Ili kuthibitisha ushawishi wangu wa kiroho, niliondoka kwenye njia ya kupaa na kufanya mageuzi machache ya digrii 360. Hakuna kilichoonekana kuharibika.

Nilishangaa, “Je, nipae na kuwapeleka abiria wanakoenda kwa muda mzuri, ama nirudi kwenye lango?” Nilijua kurudi ingesababisha kuchelewa sana. Njia ya kupaa huwa ni ya njia moja tu; ningehitajika kungoja wadhibiti njia wa chini kunitengeneza nafasi kuendesha kinyume cha nyendo. Kisha ingetubidi tungoje kikosi cha urekebishaji kukagua ndege. Kuchelewa kungesababisha shida kwa shirika la ndege na kwa abiria waliokuwa na watu wakukutana na maunganisho ya kufanya. Pia niliwazia jinsi idara ya urekebishaji ingesema kuhusu repoti yangu kuwa ndege lilikuwa na shida wakati sikuwa na chochote cha kuonyesha ila tu hisia wa nguvu.

Kama kapteni wa ndege, nilikuwa na jukumu la usalama wetu, kwa hivyo nikaamua kufuata msukumo wangu na kurudi.

Tulipofika langoni, nilimwambia mekanika kuwa nilihisi kitu kilikuwa kibaya na ndege lakini sikujua shida ilikuwa nini. Hakuamini kulikuwa na shida

“Pengine ilikuwa tu ni njia ya kupaa iliyokuwa na maji,” alisema. “Unaweza kuwa ulikuwa unateleza kwenye lami.” Alikubali, hata hivyo, kuangalia chombo cha steringi kwenye gurudumu la mbele. Baada ya kuiangalia, aliniuliza niwashukishe abiria ili aweze kupeleka ndege katika uendeshaji wa majaribio.

Aliporudi dakika 30 zilizofuata, alisikitika sana. Wakati wa uendeshaji wa majaribio, alikuwa amesikia sauti ya kusagasaga. Alipofunga breki alipokuwa akigeuka kurudi katika lango, alipoteza udhibiti wa ndege na akawa karibu kuondoka kwenye njia ya kupaa.

Ukaguzi wa karibu ulifunua kuwa breki zilikuwa zimepitia utengenezaji usiostahili jioni iliopita. Ningalishukisha ndege baada ya safari yetu, breki zingekataa, na ningepoteza udhibiti wa ndege.

Nilipokea ndege ingine ya kuendesha, na nikawapeleka abiria wangu kwa usalama walikokuwa wakienda masaa matatu baadaye.

Ninafurahia kuwa nilisikiliza ushawishi wa Roho. Ninajua kuwa Roho atatuongoza tukitafuta uongozi wa Bwana na kusikiliza ushawishi ambao unakuja.