2013
Viongozi Wakuu wa Wasichana na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama Wanazuru Eneo la Asia
Aprili 2013


Viongozi Wakuu wa Wasichana na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama Wanazuru Eneo la Asia

Kwa siku tisa Novemba 2012, Mary N. Cook, mshauri wa kwanza katika urais mkuu wa Wasichana, na Linda S. Reeves, mshauri wa pili katika urais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, walifundisha na kuvutia akina dada vijana kwa wazee kote katika Eneo la Asia.

Safari ilienda sambamba na tangazo ya marekebisho ya mtaala wa vijana, Njo, Mnifuateni, ambayo Wavulana, Wasichana na Shule ya Jumapili ya vijana itaanza kutumia Januari 2013. Mtaala mpya imeundwa kusaidia walimu kufundisha zaidi kama Mwokozi alivyofundisha na kuendeleza uhusiano bora zaidi na washiriki wa darasa.

Kufuatia safari ya Dada Cook na Dada Reeves katika Eneo la Asia, vijana wengi wa Kiasia na wazazi wao walitafakari kuwa walikuwa na motisha zaidi kutakasa na kuelekeza maisha yao na kuwa mifano kwa jamii zao.

Mjini Hong Kong, Dada Reeves aliahidi vijana, “Ukibaki kuwa msafi katika maisha yako, unaweza kusimama kwa kujiamini mbele ya mtu yeyote!”

Akiwa amevutiwa na maneno yake, Tang Kak Kei wa umri ya miaka 12 alinena baada ya mkutano, “Najua kwamba ninafaa kusoma Kitabu cha Mormoni kila siku. Kujifunza kutubu na kuishi kwa wema ndio kile Kwa Nguvu ya Vijana imenifunza kufanya ili Nuru ya Kristo na furaha ya kweli iweze kung’ara kupitia kwangu.”

Nchini India, Dada Cook alikutana na washiriki katika jumba jipya la mkutano katika Wilaya ya Chennai India na washiriki wa kigingi kipya cha Hyderabad India na aliwashauri vijana kujiandaa kwa ajili ya siku zijazo. “Jiitimisheni wenyewe kielimu,” alitoa wito, “na ujuzi wa kukusaidia kujenga ufalme. Zingatia familia yako na kile unaweza kufanya ili kubariki wanafamilia wako, na kwa maandalizi yako ya kiroho ili uwe mstahiki wa ushawishi wa kiroho na ili ujue mahali pa kwenda na jambo la kufanya.”

Nchini Indonesia, Dada Reeves alishiriki katika mkutano wa kwanza wa kigingi wa Kigingi cha Surakarta Indonesia kipya. “Tulihisi roho zao nyenyekevu na zenye upendo. Washiriki waaminifu vipi!” alisema.

Dada Reeves kisha akatemebelea Malaysia, ambapo alijadili na kundi la akina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, masuala makubwa zaidi ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Kama kama shirika katika Malaysia na jinsi Kanisa linaweza kutoa mwongozo na msukumo.

Nchini Taiwan, Dada Reeves alinena kuhusu nguvu na kujitolea kwa washiriki huko. “Tunafurahia sana kujua kuhusu maisha yao ya uaminifu na uendaji kwao hekaluni kwa udhabiti… Washiriki hao ni mfano wa kupendeza kwa marafiki zao na majirani,” alisema.

Nchini Taiwan, Mary N. Cook na Linda S. Reeves walikutana na viongozi wa eneo na viongozi wa ukuhani na washiriki wa Taiwan.

Picha na Yang Chieh-wen