2013
Kuelewa Ubatizo
Aprili 2013


Watoto

Kuelewa Ubatizo

Ni Nani atanibatiza?

Yeyote atakaye kubatiza anahitaji kuwa na ukuhani— uwezo wa kutenda katika jina la Mungu. Wakati Yesu alitaka kubatizwa, Alimuendea Yohana Mbatizaji, ambaye alikuwa na ukuhani (ona Mathayo 3:13).

Mtu atakaye kubatiza atapata ruhusa kutoka kwa askofu au rais wa tawi.

Je, ni lazima niende chini ya maji ili kubatizwa?

Yesu alibatizwa kwa kuzamishwa, inayomaanisha Alienda kabisa chini ya maji na kwa haraka kurudi juu tena. (ona Mathayo 3:16). Hivi ndivyo utakavyobatizwa. Kubatizwa katika njia hii kunatukumbusha kuwa tunawacha nyuma maisha yetu ya zamani na kuanza maisha mpya ya msimamo katika kumtumikia Mungu na watoto Wake.

Je, ni ahadi gani ninazoweka ninapobatizwa?

Unapobatizwa, unafanya agizo, ama ahadi ya njia mbili, na Baba wa Mbinguni. Unamuahidi kuwa utafanya vitu fulani, na Yeye anaahidi kukubariki. Agano hili limeelezwa katika maombi ya sakramenti yanayosemwa kila Jumapili (ona M&M 20:77–79). Unaahidi:

  • Kumkumbuka Yesu Kristo.

  • Kutii amri Zake.

  • Kuchukuwa juu yako jina la Kristo, ambayo humaanisha kuweka kazi Yake mbele maishani mwako na kufanya kile anachotaka badala ya kile dunia inataka.

Unapoweka ahadi hii, Baba wa Mbinguni anaahidi kuwa Roho Mtakatifu atakuwa nawe na kuwa dhambi zako zitasamehewa.

Roho Mtakatifu ni nini?

Kipawa cha Roho Mtakatifu ni mojawapo wa vipawa vya thamani kuu vya Baba wa Mbinguni. Ubatizo wako kwa maji si kamilifu hadi waume walio na Ukuhani wa Melkizediki wakupatie baraka ya kupokea Roho Mtakatifu (ona  Yohana 3:5).

Roho Mtakatifu ni mshiriki katika Uungu. Yeye hushuhudia Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo na hutusaidia kujua kile kilicho kweli. Yeye hutusaidia kuwa na nguvu kiroho. Yeye hutuonya juu ya hatari. Yeye hutusaidia kujifunza. Roho Mtakatifu anaweza kutusaidia kuhisi upendo wa Mungu.

Unapodhibitishwa kama mshiriki wa Kanisa, Roho Mtakatifu anaweza kuwa nawe daima ukichagua haki.

Je, ni kwa nini ninafaa kuwa anglau wa umri miaka nane ili kubatizwa?

Bwana anafundisha kuwa watoto hawapaswi kubatizwa hadi wawe wa umri ya kutosha kuelewa tofauti kati ya mema na mbaya, ambayo maandiko yanasema ni umri wa miaka nane. (ona Moroni 8:11–12; M&M 29:46–47; 68:27).

Picha© Dynamic Graphics; kielelezo cha picha na David Stoker, Matthew Reier, na Sarah