2013
Kuchagua Sehemu Bora
Aprili 2013


Kuchagua Sehemu Bora

Wakati mwingine unalazimika kuwacha kitu kizuri kwa ajili ya kitu bora.

Siku moja Zoltán Szücs wa Szeged, Hungary alimshangaza kocha wake wa kukayaki kwa kumuambia kuwa hangeenda Ujerumani kwa mashindano.

“Ilikuwa katika siku sawa na ubatizo wangu, kwa hivyo nilisema hapana,” Zoltán alisema.

Katika umri wa miaka 17, Zoltán alikuwa ameshinda mashindano mengi ya kukayaki. Ni mchezo maarufu katika Hungary, na Zoltán alikuwa mzuri—mzuri vya kutosha hadi kuwa mweledi alikuwa na uwezekano wa halisi. Zaidi ya kuamua kukosa shindano moja tu, Zoltán angewacha kukayaki kabisa hivi karibuni. Alikuwa na kitu bora cha kufanya

Kukayaki kulikuwa ni vizuri kwa Zoltán. Kwa miaka akifanya mazoezi na kocha wake, alikuwa amejifunza kujidhibiti, utiifu, na kutia bidii. Zoltán alikuwa amejifunza pia kuepuka dutu na tabia ambazo zingedhuru utendaji wake. Haikuwa maisha rahisi; ilikuwa ya upweke, na kuelekea kuwa mweledi kungechukua muda zaidi. Weledi hufanya mazoezi masaa 12 kila siku na ni lazima washindane Jumapili.

“Kukayaki kulichukuwa muda wa masaa yangu,” Zoltán anasema. “Nilikuwa mlokole. Kwa sababu hiyo, niliwacha vitu vingi nje ya maisha yangu.”

Hiyo ndiyo sababu Zoltán aliamua kuwa hangeweza kujishughulisha mwenyewe yote katika injili na kukayaki pia. Mnamo 2004 alimuambia kocha wake hatakayaki tena.

Awali mwaka huo wamisionari walikuwa wameanza kumfundisha mamake Zoltán. Hakushiriki katika masomo. Alikubali shingo upande mwaliko wa ubatizo wa mamake. Lakini moyo wake uliguswa na yale aliyohisi mara tu alipoingia katika jumba la kanisa. Zoltán alikubali kukutana na wamisionari, kwa sehemu kuwa angejitambulisha nao.

Wamisionari walinivutia kwa sababu walikuwa ni watu wa kawaida lakini waliishi kiwango cha juu, anasema.

Kwa sababu ya kiwango cha juu ambacho Zoltán alikuwa tayari anaishi kama mkayaki, alikubali mafundisho ya injili kwa urahisi kama ya thamani. Alibatizwa miezi miwili iliyofuata.

Mwanzoni alidhani kuwa angeendelea kukayaki lakini bila kufanya mashindano Jumapili. Lakini kwa sababu yeye ni aina ya mtu ambaye, mara tu anapoamua kutekeleza shughuli au mwendo, anataka kufanya vyema, alichagua kuwachana na kukayaki kabisa.

Alijaribu mara moja kukayaki kama jambo la kupitisha wakati baada ya ubatizo wake. Alipofanya hivyo, kocha alimuomba asaidie kuwafundisha wengine na kupanga safari kwa vile yeye hangeshindana. Lakini hakutaka kujitolea katika kukayaki—ama shughuli ingine—ambayo ingezuia ufuasi wake.

Hivyo basi Zoltán akaweka kafi yake kando na kujitolea mwenyewe kwa huduma katika uamuzi unaotukumbusha ule Rais Howard W. Hunter (1907–95) alifanya alipooa. Rais Hunter alikuwa mwanamuziki shupavu ambaye alicheza vyombo kadhaa vya muziki. Jioni alikuwa akicheza katika orkestra, lakini maisha ya wale aliohusiana nao yalikuwa hayapatani na viwango vya injili. Kwa hivyo Rais Hunter aliviweka vyombo vyake vya muziki mbali na kuvitumia katika fursa za kuimba na familia peke yake.1

Zoltán anakosa kukayaki, lakini alitambua kuwa upendo wake wa kukayaki ulikuwa na nguvu ya kutosha kushindana na, na labda kushinda, upendo wake wa Bwana kama angelikaa karibu sana na mchezo huu.

Kanuni hio hio inaweza kutumika kwa shughuli yoyote ile ambayo inatutoa kutoka kwa yule ambaye Mungu anataka tuwe. Kwa kila moja wetu inaweza kuwa bora kupitia maisha bila vitu fulani—hata kama ni vitu vizuri—badala ya kuhatarisha maisha yetu ya milele ili kuwa navyo.

“Kanisa likawa maisha yangu,” Zoltán asema. “Kujua kwamba kukayaki hakungekuwa hai ningalitaka kushughulika na kuwa ingekuwa jambo la kustarehe tu, ikawa rahisi kuwacha. Badala, nilitaka kumweka Baba wa Mbinguni kuwa fokasi yangu.”

Zoltán akaanza kujifunza injili kwa nguvu sawa yeye huleta kwa harakati yoyote ile. Akaweka lengo la kuhudumu misheni. Alitaka kubaki katika nchi yake na kuwafundisha wengine.

Alihudumu Hungary na sasa anafanya kazi kama mwalimu wa Kingereza wa sekondari. Anaendelea kuweka vipaumbele vyake katika injili. “Kuna vitu tunavyopaswa kuwacha kwa vile vinatuzuia na Mungu,” anasema. “Ni rahisi kuwachana na mabaya tunayojua tunapaswa. Mara nyingi hatutambua tunapopaswa kuwacha kitu kizuri kwa ajili ya kitu bora. Tunafikiria kuwa kwa sababu si kibaya, tunaweza kukishikilia na bado kufuata mpango wa Mungu.” Lakini Zoltán anajua kuwa ni lazima tuwache kile kizuri kama kinatuzuia kufuata mpango wa Mungu kwetu.

Muhtasari

  1. Ona Eleanor Knowles, Howard W. Hunter (1994), 81.

Zoltán Szücs, wa Szeged, Hungary, aliwacha kukayaki ili kuwa na muda zaidi kwa ajili ya injili.

Juu: picha © Thinkstock; chini:picha na Adam C. Olson