2013
Kwa nini Kanisa lina jina refu hivyo?
Aprili 2013


Shahidi Maalum

Kwa nini Kanisa lina jina refu hivyo?

Kutoka “Umuhimu wa Jina,” Liahona, Nov. 2011, 79–82.

Picha
Mzee M. Russell Ballard

Washiriki wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili ni mashahidi maalum wa Yesu Kristo.

Yesu Kristo mwenyewe alilipa Kanisa jina (ona Mafundisho na Maagano 115:4).

Maneno Kanisa la Yesu Kristo yanatangaza kuwa ni Kanisa Lake.

La Watakatifu wa Siku za Mwisho yanaeleze kuwa ni Kanisa sawa ni lile Kanisa Yesu Kristo alianzisha alipoishi duniani lakini limerejeshwa katika siku hizi za mwisho.

Watakatifu inamaanisha kuwa tunamfuata Yeye na kujaribu kufanya mapenzi Yake.

Washiriki wetu wameitwa Wamormoni kwa sababu tunaamini Kitabu cha Mormoni, lakini tunapaswa kutumia jina zima ya kanisa panapowezekana kila mara.

Mchoro na Brad Teare