2013
Kunywa kutoka Chemichemi
Aprili 2013


Mpaka Tutakapokutana Tena

Kunywa kutoka Chemichemi

Yesu Kristo ni chemchemi ya maji ya uzima.

Tunapozungumzia kuhusu uzuri wa mahekalu, kwa kawaida sisi hutaja minara, madirisha, na picha. Sisi huzungumzia kwa heshima juu ya vidimbwi vya ubatizo, vyumba vya endaumenti, vyumba vya maunganisho, na vyumba vya selestia.

Lakini wakati nabii huweka wakfu hekalu kwa Bwana, yeye huweka wakfu jumba lote, si tu sehemu nzuri ambazo kila mtu huona. Katika maombi ya kuweka wakfu Hekalu la Kansas City Missouri, Rais Thomas S. Monson alisema: “Tunaweka wakfu ardhi ambayo hekalu hili linasimama. Tunaweka wakfu kila sehemu ya muundo huu mzuri, kutoka kwa misingi usioonekana hadi kwa sanaa ya ajabu ya Moroni inayokaa kwenye kilele chake cha juu kabisa.”1 Wakati Rais Joseph Fielding Smith alitamka sala ya kuweka wakfu juu ya Hekalu la Ogden Utah, aliweka wakfu “misingi, kuta, sakafu, paa, mnara, na maeneo yote ya jengo,” na aliomba kwa ajili ya ulinzi wa “sehemu zote za kimitambo, mfereji ya mataa na vifaa, mashine ya hewa na lifti, na mambo yote yanayohusu jengo hili.”2

Ninashukuru kwamba Bwana huwashawishi manabii Wake kuweka wakfu kila sehemu ya hekalu. Ingawa bawaba la mlango au kiegezi mwanga kwa wazi kina lengo dogo kuliko madhabahu katika chumba cha maunganisho, vile vipande vidogo vinachangia kusudi kuu la hekalu la kutukuza.

Mojawapo wa vipande hivi vidogo vimenisaidia kujifunza somo la kudumu. Nilikuwa katika Hekalu ya Salt Lake siku moja, nikijiandaa kutoka chumba cha kuvalia baada ya kushiriki katika agizo kwa niaba ya wafu. Kuona chemichemi ya maji ya kunya, nikatambua kuwa nilikuwa na kiu, kwa hivyo nikainama chini kwa ajili ya kunywa haraka. Ujumbe ukaja akilini mwangu:

Wewe hunywa maji haya katika hekalu, lakini je, kweli wewe hunywa maji hai ambayo yanapatikana hapa?

Haikuwa hukumu ya nguvu—wala tu ukemeo mpole na swali la kupenya roho.

Jibu langu kwa swali hilo lilikuwa ni hapana. Sikuwa kabisa kimilifu nikinywa maji ya uhai ya hekalu. Ilinibidi nikubali kuwa akili yangu ilitanga dakika chache awali nilipokuwa nikipokea maagizo kwa niaba ya wafu. Ingawa nilikuwa nimefanya kazi nzuri kwa niaba ya watu waliohitaji msaada wangu, sikuwa nimejiruhusu kupokea msaada wote niliohitaji.

Sasa, kila wakati mimi huenda hekaluni, mimi hutafuta chemchemi ya maji ya kunywa na husimana kwa ajili ya kunywa. Mimi hujiuliza mwenyewe jinsi kwa undani mimi hunywa kutoka katika chemchemi ya maji hai. Jibu langu: Bado si kwa kina vya kutosha. Lakini kiu changu kinaongezeka.

Muhtasari

  1. Thomas S. Monson, katika “Kansas City Missouri Temple: ‘Beacon of Divine Light’—an Offering of Hands and Hearts,” Church News, Mei 12, 2012, ldschurchnews.com.

  2. Joseph Fielding Smith, katika “Ogden Temple Dedicatory Prayer,” Ensign, Mar. 1972, 12.

Picha © iStockphoto.com/Amphotora