2013
Umuhimu wa Marafiki Wema
Aprili 2013


Kufundisha Kwa Nguvu ya Vijana

Umuhimu wa Marafiki Wazuri

Marafiki wana ushawishi mkubwa juu ya matendo yetu, hasa katika ujana wetu. “Watashawishi jinsi unafikiri na kutenda, na hata kusaidia kuamua mtu utakaye kuwa.”1 Na unapochagua marafiki wazuri, “watakuwa nguvu na baraka kwako. Watakusaidia kuwa mtu bora na watafanya iwe rahisi kwako kuishi injili ya Yesu Kristo.”2

Fungua kurasa 52–53 katika toleo hili, Elaine S. Dalton, rais mkuu wa Wasichana, alifundisha umuhimu wa kutafuta na kuwa rafiki mzuri. “Kutaka wema wa mtu mwingine ni kiini cha urafiki wa kweli”, asema.

Kujenga urafiki juu ya kanuni hizi kutawasaidia vijana kutengeneza mahusiano ya kudumu na stadi za kijamii zinazokwenda mbali zaidi tu na kuwa “rafiki” katika maeneo ya mitandao ya kijamii. Kama mzazi unaweza kuwasaidia watoto wako kuelewa umuhimu wa kuwa rafiki mzuri na wa kuchagua marafiki ambao watawahimiza kuishi injili. Mapendekezo yafuatayo yanaweza kuwa ya manufaa.

Mapendekezo ya Kufundisha Vijana

  • Kama familia, yachunguze maandiko kwa mfano wa marafiki wazuri. Jadili sifa zilizofanya mahusiano hayo kuwa imara. Zingatia David na Jonathan (ona 1 Samueli 18–23), Ruth na Naomi (ona Ruth 1–2), na Alma na wana wa Mosia (ona Mosia 27–28; Alma 17–20).3

  • Rejelea sehemu ya marafiki katika Kwa nguvu ya Vijana Shiriki na vijana wako jinsi urafiki unaweza kuathiri maisha yako. Wahimize kushiriki jinsi wameathiri na kuathiriwa na marafiki wao.

  • Soma makala ya Dada Dalton katika toleo hili. Zungumza kuhusu lengo ambalo bintiye, Emi, aliweka kutafuta marafiki wazuri. Saidia watoto wako kuweka malengo kuhusu aina ya marafiki ambao wanataka kutafuta na kuwa.

  • Zingatia kuwa na Mkutano wa Jioni wa familia nyumbani kushiriki mawazo ya kujenga urafiki, kama vile: “Ili kuwa na marafiki wazuri, kuwa rafiki mzuri. Onyesha nia ya kweli kwa wengine; tabasamu na wajulishe unawajali. Tendea kila mtu kwa wema na heshima, na jiepushe na kuhukumu na kukosoa wale walio karibu nawe.”4

Mapendekezo ya Kufundisha Watoto

  • Kuwa rafiki kunajumuisha kusaidia wengine. Soma “Standing Up for Caleb” katika Liahona ya Machi 2009 na uzungumze na watoto wako kuhusu jinsi wanavyoweza kuwa wapole kwa kila mtu wanayekutana naye.

  • Katika kila hali, lazima tuamue ni aina gani ya rafiki tutakuwa. Imbeni pamoja “I’m Trying to Be Like Jesus”5 kisha zungumza na watoto wako kuhusu jinsi wanavyoweza kuchagua kuwa rafiki mzuri, kama Mwokozi, katika maandhari tofauti.

Muhtasari

  1. Kwa Nguvu ya Vijana (kijitabu, 2011), 16.

  2. Kwa Nguvu ya Vijana, 16.

  3. Ona Jeffrey R. Holland,” New Era, Juni 1998, 62–66.

  4. Kwa Nguvu ya Vijana, 16.

  5. “I’m Trying to Be Like Jesus,” Kitabu cha Watoto cha Wimbo, 78–79.

Kielelezo na Taia Morley