2013
Kwa nini Tunahitaji Kitabu cha Mormoni
Aprili 2013


Kwa nini Tunahitaji Kitabu cha Mormoni

Picha
Bibilia Takatifu, Kitabu cha Mormoni

Picha na Bryan Beach; video capture © 2001 IRI

Baadhi ya watu wanaweza kukuuliza ni kwa nini tunahitaji Kitabu cha Mormoni wakati tayari tuna Biblia. Kwa kweli, Yesu Kristo alishuhudia kuwa hili lingetokea (ona 2 Nefi 29:3). Kuna sababu nyingi kwa nini Kitabu cha Mormoni ni muhimu katika siku yetu (kwa mfano, ona 2 Nefi 29:7–11). Hizi ni sababu chache tu kwa nini ni muhimu.

Ushahidi Mwingine wa Yesu Kristo

Maandiko yanatuonyesha mpangilio wa kutumia mashahidi wengi ili kudhibitisha ukweli katika Kanisa la Kristo. Kitabu cha Mormoni kinaongeza ushahidi wa pili kwa Biblia kama ushuhuda wa Kristo. Mzee Mark E. Petersen (1900–84) wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili aliwaikusema, “Sababu kuu tuna Kitabu cha Mormoni ni kwamba kwa mawaidha ya mashahidi wawili au watatu, mambo yote yatadhihirishwa. (Ona 2 Wak. 13:1.) Tuna Biblia, pia tuna Kitabu cha Mormoni. Vinajumuisha sauti mbili—maandishi mawili ya maandiko—kutoka kwa watu wawili wa kale waliotenganishwa kwa upana, wote wakishuhudia uungu wa Bwana Yesu Kristo.”1 Rais Ezra Taft Benson (1899–1994) ameongeza, “Tusisahau kwamba Bwana mwenyewe alitoa Kitabu cha Mormoni kama ushahidi mkuu Wake.”2

Ukamilifu wa Injili

Tunajua kwamba “mambo wazi na ya thamani yalichukuliwa kutoka” Biblia katika wakati (1 Nefi 13:40). Kitabu cha Mormoni kinafafanua mafundisho ya Kristo na kuleta utimilifu wa injili duniani mara nyingine tena (ona 1 Nefi 13:38–41). Kwa mfano, Kitabu cha Mormoni kinatusaidia kujua kwamba ubatizo lazima ufanywe kwa kuzamishwa (ona 3 Nefi 11:26) na kwamba watoto wadogo hawana haja ya kubatizwa (ona Moroni 8:4–26).

Kitovu cha Kanisa la Urejesho

Joseph Smith alishuhudia ya kwamba Kitabu cha Mormoni ni “jiwe kuu la msingi katika dini yetu”3 (utangulizi wa Kitabu cha Mormoni). Kwa vile tunajua haya, haionekani bahati mbaya kwamba Kanisa la Yesu Kristo wa Watakatifu wa Siku za Mwisho liliundwa Aprili 6, 1830, siku 11 tu baada ya Kitabu cha Mormoni kuwa kinapatikana kwa mauzo kwa umma mnamo Machi 26, 1830. Kanisa halikuundwa mpaka maandiko yake makuu ya msingi yalikuwa yanapatikana kwa washiriki wake.

Baraka katika Maisha Yetu

Kuhusu Kitabu cha Mormoni, Joseph Smith alifundisha kwamba “mtu angemkaribia Mungu zaidi kwa kufuata mafunzo yake, zaidi ya kitabu kingine.”4 Kina uwezo wa kubadilisha maisha—ikiwa ni pamoja na yako na ya wale unaoshiriki Kitabu cha Mormoni nao. Rais Henry B. Eyring, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, ameshuhudia, “Athari ya Kitabu cha Mormoni juu ya tabia yako, nguvu, na ujasiri kuwa shahidi wa Mungu ni wazi. Mafundisho na mifano ya ujasiri katika kitabu hicho itakuinua, itakuongoza na kukutia moyo. Kujifunza Kitabu cha Mormoni kwa maombi kutajenga imani katika Mungu Baba, katika Mwanawe Mpendwa, na katika injili Yake. Kutajenga imani yako katika manabii wa Mungu, wa kale na wa kisasa. Kunaweza kukuleta karibu na Mungu kuliko kitabu chochote kingine. Kinaweza kubadilisha maisha kuwa bora.”5

Muhtasari

  1. Mark E. Petersen, “Evidence of Things Not Seen,” Ensign, May 1978, 63.

  2. The Teachings of Ezra Taft Benson (1988), 204.

  3. Joseph Smith, katika utangulizi wa Book of Mormon.

  4. Joseph Smith, katika utangulizi wa Book of Mormon.

  5. Henry B. Eyring, “A Witness,” Liahona, Nov. 2011, 69–70.

Masomo ya Jumapili

Mada ya Mwezi Huu: Uasi na Urejesho