2020
Wapendwa Wazazi
Aprili 2020


Wapendwa Wazazi,

Picha
Dear Parents

Mapema msimu wa kichipua mwaka 1820, karibu na wakati wa Pasaka, Joseph Smith aliomba na kuwaona Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Gazeti hili linazungumza kuhusu wakati huo maalum. Hizi ni kurasa chache za kutafuta:

  • Hadithi inayosimuliwa kwa picha inaelezea jinsi ambavyo Kanisa Lililorejeshwa ni sehemu ya mpango wa Mungu (R4–10).

  • Rais Nelson anatueleza jinsi ambavyo tunaweza kutoa msaada kwa Urejesho (R2).

  • Wimbo mpya unafundisha kuhusu Ono la Kwanza (R16–17).

  • Hadithi inafundisha jinsi Urejesho unavyoweza kubariki familia zetu (R20–21).

Je, si inapendeza kwamba tunaweza kuwa wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho? Acheni tushiriki habari njema ya Yesu na Kanisa Lake kwa ulimwengu!

Pasaka Njema,

Rafiki

© 2020 na Intellectual Reserve, Inc. Haki zote zimehifadhiwa

Tafuta Liahona iliyofichwa ndani!