2020
Ono la Kwanza
Aprili 2020


Ono la Kwanza

Kwa Unyenyekevu [quarter note] = 68

Picha
The First Vision

1. Joseph alikuwa na swali kuhusu njia ya kwenda,

Kwa hivyo kwa uaminifu alijifunza ili kusaidia kukuza ufahamu wake.

Andiko liligonga moyo wake, likimualika kusali,

Na Joseph alijua kwamba angeweza kumwomba Mungu amuoneshe njia.

2. Akitafuta kimya na utulivu, alichagua msitu

Akaomba kwa nguvu zake zote kwa ajili ya Mungu kusikia ombi lake.

Baba na Mwanae wakashuka chini

Kujibu swali la Joseph na pia kurejesha injili kwa upendo.

3. Kutoka kwenye ono lile la ajabu, ufunuo zaidi ulitiririka.

Bwana alirejesha injili ili kila mtu ajue:

Mbingu hazijafungwa; Bwana aongea leo.

Yeye humwita nabii katika wakati wetu ili aongoze hatua zetu katika njia Yake.

Kiitikio: Alisali kwa imani na mbingu ikajibu.

Baba na Mwana walifahamu jina lake.

Ninapiga magoti kuomba. Ninajua Mungu ananipenda

Na Yeye husikia maombi yangu vivyo hivyo.

Vielelezo na Sarah Keele