2020
Kutoa msaada kwa Urejesho
Aprili 2020


Kutoka kwa Urais wa Kwanza

Kutoa msaada kwa Urejesho

Imetoholewa kutoka “Hope of Israel” (ibada ya vijana kote ulimwenguni, Juni 3, 2018), 19, HopeOfIsrael.ChurchofJesusChrist.org.

Picha
Helping with the Restoration

Mwaka 1820, Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walimtokea Joseph Smith. Baba wa Mbinguni alisema, “Huyu ni Mwanangu Mpendwa. Msikilize Yeye!” Urejesho wa injili ulianza siku hiyo miaka 200 iliyopita. Unaendelea leo!

Siku moja Yesu Kristo atarudi duniani tena. Hizi ni njia nne unazoweza kutoa msaada kwa Urejesho na kujitayarisha kwa ajili ya wakati ambapo Yesu atarudi:

  • Jenga imani yako katika Yesu Kristo.

  • Fanya uchunguzi kuhusu familia yako na toa msaada ili kazi ya hekaluni ifanywe kwa niaba yao.

  • Jiandae kwenda hekaluni.

  • Wasaidie watu wajifunze kuhusu Yesu Kristo na Kanisa Lake.

Kufanya vitu hivi kutasaidia kuandaa ulimwengu kwa ajili ya siku ya kupendeza wakati Yesu atakaporudi tena. ●

Vielelezo na Katie McDee