2020
Hekalu na Wewe
Aprili 2020


Hekalu na Wewe

Picha
The Temple and You

Kabla ya kurejeshwa kwa Kanisa, watu waliamini kwamba ikiwa mtu fulani katika familia yao alifariki bila ya kubatizwa, hawangemuona tena. Lakini kwa sababu ya Urejesho, tunaweza kubatizwa kwa niaba yao katika hekalu. Tunaweza kuunganishwa pamoja milele!

Kama Joseph Smith, wewe pia umechaguliwa na Baba wa Mbinguni kufanya kazi muhimu maishani mwako. Baadhi ya kazi hiyo inaweza kufanyika katika mahekalu. Unaweza kukusanya majina ya mababu zako ambao hawakubatizwa wakati walipoishi duniani. Kisha, baada ya kupokea kibali cha hekaluni, unaweza kwenda hekaluni na kubatizwa kwa niaba yao.

Unapofanya kazi hii, sali kwa Baba wa Mbinguni akuongoze. Mababu zako wanaweza kukusaidia pia. Ni baraka muhimu na takatifu iliyoje hii itakuwa kwa ajili yako na kwa ajili yao!

Baadhi yenu mnaweza kuwa hamuwezi kufanya kazi ya hekaluni kwa wakati huu, lakini siku moja mtaweza. Kumbuka siku zote kwamba wewe ni mtoto wa Mungu. Yeye anakupenda kikamilifu.

Sikiliza uvuvio wa Roho Mtakatifu na kuwa tayari kwenda hekaluni siku moja. Kufanya hili kutakusaidia kujenga maisha mazuri kwa ajili yako na kwa ajili ya familia zako za awali, za wakati huu, na za baadaye. Unapofanya kazi ya Bwana, Yeye atakusaidia. Wewe ni mmoja wa roho Zake jasiri zaidi. ●

Kielelezo na Jared Matthews