2020
Vijana
Aprili 2020


Vijana

Picha
Photo of Mikayla J from Fiji

Picha na Leslie Nilsson

Mimi ni mwongofu kwa Kanisa. Mojawapo ya vitu ambavyo vilinivutia mwanzo ilikuwa shughuli za vijana. Hata sasa mimi bado nafurahia kutumia wakati pamoja na marafiki kutoka Kanisani ambao hushiriki burudani nzuri, ya aina ya kuinua. Mimi hufurahia hasa kutembelea Hekalu la Suva Fiji pamoja nao kila wiki.

Fiji kuna ushawishi mkubwa kutoka kwa makundi ya rika moja. Maduka huwa hayaulizi kitambulisho wakati wote ili kununua pombe, sigara, na vitu kama hivyo. Watoto huvinunua wakati wote. Inaweza kuwa vigumu kuchagua mema.

Mojawapo ya vitu ambavyo hunifanya kuwa imara ni ndugu zangu wadogo. Mimi ni mkubwa wao, kwa hivyo mimi huwafikiria kila wakati pale ninapojaribiwa kufanya jambo baya. Sitaki wafanye maamuzi mabaya kwa sababu ya kuona nikifanya kitu kibaya kwanza. Kabla mama yangu hajafariki, aliniomba niahidi kuwatunza ndugu zangu na siku zote kuwajali.

Kufikia sasa mimi ni muumini pekee wa Kanisa miongoni mwa ndugu zangu. Lakini mimi husali kwa niaba yao kila siku. Ninamshukuru Baba wa Mbinguni kwa kuwapa wao siku nyingine ya kuishi, na ninasali kwamba watapokea ufahamu wa injili Yake. Wananipa nguvu.

Mikayla J., miaka 17, Fiji