2020
Pasaka Ina Maana Gani Kwangu Mimi?
Aprili 2020


Njoo, Unifuate: Kitabu cha Mormoni

Pasaka Ina Maana Gani Kwangu Mimi?

Machi 30–Aprili 12Pasaka

Picha
What Does Easter Mean for Me

Siku ya Pasaka tunasherehekea “siku muhimu sana katika historia”1—Ufufuo wa Mwokozi wetu Yesu Kristo. Tukio hili ni kitovu cha mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni.

Katika maisha ya kabla ya dunia, Yesu Kristo alichaguliwa kuwa Mwokozi wetu. Aliahidi kutoa njia ya sisi kusamehewa dhambi zetu na kurudi nyumbani kwetu mbinguni.

Asubuhi hiyo ya Pasaka ya kwanza, Yesu alitimiza ahadi Yake. Alishinda kifo. Kama matokeo, “Yeye ni nuru na uzima wa ulimwengu; ndio, nuru isiyo na mwisho, ambayo haiwezi kutiwa giza; ndio, na pia uzima usio na mwisho, kwamba hakutakuwa tena na kifo” (Mosia 16:9).

Ni baraka gani ambazo Ufufuo unaleta kwako?

Toba

Yesu Kristo anamuuliza kila mmoja wetu, “Je mtarudi kwangu sasa, na kutubu dhambi zenu, na kugeuka ili niwaponye?” Anaahidi, “Yeyote atakayekuja, nitampokea” (3 Nefi 9:13–14). Unahisi vipi unapotubu?

Ufufuo

Kifo hakiepukiki, lakini ushindi wa Mwokozi dhidi ya kifo unahakikisha kwamba sote tutafufuliwa—mwili na roho vikiunganishwa tena katika mwili mkamilifu (ona Alma 11:43). Ni jinsi gani ufahamu wa Ufufuo unakupa tumaini?

Uzima wa Milele

Upatanisho wa Mwokozi unasababisha uzima wa milele, au kuinuliwa kuwezekane. Ili kupokea baraka hii, ni lazima tutii amri. Rais Russell M. Nelson ameiita njia inayoelekea kwenye uzima wa milele “njia ya agano.”2 Ni sharti tufanye nini ili kufuata njia hii inayoelekea kwenye uzima wa milele?

Muhtasari

  1. Dieter F. Urchtdorf, “Tazama Mtu!” Liahona, Mei. 2018, 108.

  2. Russell M. Nelson, “Tunaposonga Mbele Pamoja,” Liahona, Apr. 2018, 7.