Mkutano Mkuu
Kustaajabu juu ya Kristo na Injili Yake
Mkutano mkuu wa Aprili 2022


Kustaajabu juu ya Kristo na Injili Yake

Hebu kumbukumbu ya kile macho yetu yalichoona na mioyo yetu ilichohisi iongeze kustaajabu kwetu kwenye dhabihu ya upatanisho ya Mwokozi.

Ninaye rafiki mwema, mwenye akili sana, profesa wa chuo kikuu aliyestaafu, mtunzi mahiri, na, zaidi ya yote, mfuasi wa Yesu Kristo mwenye msimamo. Ametembelea Ardhi Takatifu mara nyingi sana ili kushiriki katika mikutano, kuendesha ufafiti wa kielimu, na kuongoza matembezi. Kulingana na yeye, kila mara anapozuru ardhi ambapo Yesu alitembea, anastaajabu kwa sababu bila shaka anajifunza jambo jipya, la kushangaza na lenye msukumo kuhusu Mwokozi, huduma Yake ya duniani na ardhi Yake pendwa ya nyumbani. Kustaajabu ambako rafiki yangu anaonesha wakati anapozungumza kuhusu yote anayojifunza kwenye Ardhi Takatifu ni ya kuambukiza, na mshangao huu umekuwa muhimu kwenye mafanikio yake makuu na utafutaji wa elimu kwenye maisha yake.

Niliposikiliza uzoefu wake na kuhisi shauku yake, nimetafakari juu ya maajabu ya kiroho, nikisema hivyo, ambayo tunaweza na tunapaswa kuyahisi kwa ajili ya injili ya Yesu Kristo na tofauti inayoweza kuleta katika ufuasi wetu na katika safari yetu kuelekea uzima wa milele. Maajabu ninayoyazungumzia ni mvuto wa hisia, kustaajabu au kuvutiwa ambavyo ni kawaida kwa wote ambao kwa moyo wote huyakita maisha yao kwa Mwokozi na mafundisho Yake na ambao kwa unyenyekevu hutambua uwepo Wake katika maisha yao. Hisia kama hiyo ya mshangao, ikisukumwa na ushawishi wa Roho Mtakatifu, huchochea shauku ya kuishi mafundisho ya Kristo kwa shangwe.1

Maandiko yana mifano kadhaa ya jinsi mvuto huu unavyoweza kudhihirishwa. Nabii Isaya, kwa mfano, alielezea kina cha shukrani yake kwa Bwana kupitia kushangilia kwake ndani Yake.2 Wale waliomsikia Yesu akihubiri katika sinagogi huko Kapernaumu walishangazwa kwa mafundisho Yake na nguvu ambazo kwazo alifundisha.3 Ilikuwa hisia sawa na hii ambayo ilipenya kila sehemu ya moyo wa Joseph Smith wakati aliposoma katika Biblia sura za mwanzo za Yakobo, zikimwongoza kutafuta hekima ya Mungu.4

Wapendwa akina kaka na dada zangu, wakati kwa hakika tunapostaajabu juu ya Yesu Kristo na injili Yake, tunakuwa na furaha, tunakuwa na shauku zaidi kwa ajili ya kazi ya Mungu na tunatambua mkono wa Bwana katika mambo yote. Kwa nyongeza, usomaji wetu wa maneno ya Mungu unakuwa wenye maana zaidi; sala zetu, zenye kusudio zaidi; kuabudu kwetu, kwenye staha zaidi; huduma yetu kwenye ufalme wa Mungu, yenye bidii zaidi. Mambo haya yote yanachangia kwenye ushawishi wa Roho Mtakatifu kuwa wa mara nyingi zaidi kwenye maisha yetu.5 Hivyo, ushuhuda wetu juu ya Mwokozi na injili Yake utaimarishwa, tutamweka Kristo hai ndani yetu,6 na tutaishi maisha yetu tukiwa “wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; tukifanywa imara kwa imani, … tukizidi kutoa shukrani.”7 Tunapoishi katika njia hii, tunakuwa wastahimilivu zaidi kiroho na tunalindwa dhidi ya kuangukia kwenye mtego wa kutojali kiroho.

Kutojali huko kunatambulishwa na upotevu wa taratibu wa msisimko wetu wa kushiriki kikamilifu kwenye injili ya Bwana. Kwa ujumla kunaanza wakati tunapohisi kwamba tayari tumepokea ufahamu na baraka zote muhimu kwa ajili ya furaha yetu kwenye maisha haya. Ridhaa hii, nikizungumza hivyo, hutufanya tuchukulie zawadi za injili kirahisi rahisi, na kuanzia hapo na kuendelea, tunaingia kwenye hatari ya kupuuzia vyote kujikita kwetu mara kwa mara kwenye mambo ya msingi ya injili ya Yesu Kristo8 na maagano tuliyoyafanya. Kama matokeo, taratibu tunajiweka mbali na Bwana; tukidhoofisha uwezo wetu wa “kumsikiliza Yeye,”9 tukiwa wa kawaida na wasio na hisia kwenye ukuu wa kazi Yake. Shaka kuhusu kweli za ushuhuda wetu ambao tayari tumeupokea inaweza hupenya akili na mioyo yetu, ikitufanya wahanga kwenye majaribu ya adui.10

Mchungaji Aiden Wilson Tozer, mwandishi mashuhuri na Mkristo shujaa, aliandika, “kuridhika ni adui mkubwa wa ukuaji wote wa kiroho.”11 Je, hiki si kile hasa kilichowatokea watu wa Nefi muda mfupi baada ya kuzaliwa kwa Kristo? Walianza “kuendelea kupungukiwa zaidi kwa mshangao katika ishara au maajabu kutoka mbinguni,… [kutoamini] yote ambayo walisikia na kuona.” Na hivyo Shetani “akafunika macho yao na kuwaongoza mbali kuamini kwamba mafundisho ya Kristo yalikuwa ni upumbavu na kitu cha bure.”12

Akina kaka na dada zangu wapendwa, katika upendo Wake mkamilifu na usio na mwisho na akifahamu asili yetu ya ubinadamu,13 Mwokozi ameanzisha njia kwa ajili yetu kuepuka kuangukia kwenye mtego wa kutojali kiroho. Mwaliko wa Mwokozi unatupatia mtazamo mpana, hususan tukizingatia ulimwengu wenye mambo mengi ambamo tunaishi: “Jifunze kwangu, na sikiliza maneno yangu; enenda katika unyenyekevu wa Roho wangu, na utapata amani kwangu.”14 Tunapokubali mwaliko wa Mwokozi, tunaonesha unyenyekevu wetu, hamu yetu ya kufundishika na tumaini letu la kuwa zaidi kama Yeye.15 Mwaliko huu hujumuisha pia kumtumikia Yeye na kuwahudumia watoto wa Mungu “kwa moyo [wetu] wote, uwezo, akili na nguvu.”16 Kwenye kiini cha juhudi yetu kwenye safari hii ni, ndiyo, amri kuu mbili: kumpenda Bwana Mungu wetu na kumpenda jirani yetu kama tunavyojipenda.17

Aina hii ya tabia ni sehemu ya sifa ya Yesu ya kiungu na ilikuwa dhahiri kwenye kila kitu Yeye alichofanya kipindi cha huduma Yake ya duniani.18 Kwa hiyo, wakati kwa makusudi na kwa dhati tunapojizatiti sisi wenyewe kumtazama Yeye na kujifunza kutokana na mfano Wake mkamilifu,19 tunapata kumjua Yeye vyema. Tunakua katika shauku na hamu ya kujumuisha katika maisha yetu kiwango cha juu cha jinsi tunavyopaswa kuishi, mfano tunaopaswa kuweka na amri tunazopaswa kufuata. Tunapokea pia uelewa wa ziada, hekima, sifa ya kiungu na neema kwa Mungu na kwa jirani zetu.20 Ninaweza kuwahakikishia kwamba uwezo wetu wa kuhisi ushawishi na upendo wa Mwokozi utakuzwa katika maisha yetu, ukiongeza imani yetu, hamu yetu ya kutenda kwa haki na msukumo wa kumtumikia Yeye pamoja na wengine.21 Kwa nyongeza, shukrani yetu kwa baraka na changamoto tunazopitia katika maisha haya vitafanywa imara na kuwa sehemu ya kuabudu kwetu kwa dhati.22

Rafiki zangu wapendwa, mambo haya yote huimarisha kustaajabu kwetu kiroho juu ya injili na hutusukuma kutii kwa shangwe maagano tunayofanya na Bwana—hata katikati ya majaribu na changamoto tunazopitia. Naam, kwa matokeo haya kutokea, tunahitaji kujikita sisi wenyewe kwa imani na kusudi halisi kwenye mafundisho ya Mwokozi,23 tukijitahidi kujumuisha sifa Zake kwenye njia yetu ya kuwa.24 Kwa nyongeza, tunahitaji kusogea karibu Naye kupitia toba yetu,25 kutafuta msamaha Wake na nguvu ya ukombozi katika maisha yetu na kutii amri Zake. Bwana mwenyewe aliahidi kwamba Yeye ataongoza mapito yetu ikiwa tutamtumaini kwa mioyo yetu yote, kumkiri Yeye katika njia zetu zote na kutozitegemea akili zetu wenyewe.26

Picha
Mzee Jones pamoja na Wes

Mtu niliyekutana naye karibuni, ambaye jina lake ni Wes, na ambaye anahudhuria mkutano leo, alikubali mwaliko wa Kristo wa kujifunza juu Yake na injili Yake na kuanza kupata uzoefu wa kustaajabia upendo Wake baada ya miaka 27 ya kujiweka kando ya njia ya agano. Aliniambia kwamba siku moja alifikiwa na mmsionari kupitia Facebook, Mzee Jones, ambaye alipangiwa kwa muda kwenye eneo la Wes kabla ya kwenda kwenye misheni yake halisi aliyopangiwa huko Panama. Wakati Mzee Jones alipokutana na wasifu wa Wes, bila kujua kabla kwamba alikuwa tayari muumini wa Kanisa, alihisi mwongozo wa Roho Mtakatifu na alifahamu kwamba alipaswa kuwasiliana na Wes haraka. Kwa haraka alifanyia kazi msukumo huu. Wes alishangazwa kwa mawasiliano haya ya bila kutarajia na alianza kutambua kwamba Bwana alimfahamu licha ya kuwa kwake mbali kutoka kwenye njia ya agano.

Tangu hapo na kuendelea, Wes pamoja na wamisionari walianza kuwasiliana mara kwa mara. Mzee Jones na mwenzake walifanya vitendo vya huduma na kutoa jumbe za kiroho kila wiki ambazo zilimsaidia Wes kupata tena mshangao wake juu ya Mwokozi na injili Yake. Ziliwasha tena miale ya ushuhuda wake juu ya ukweli huu na upendo wa Mwokozi kwa ajili yake. Wes alihisi amani ambayo huja kutoka kwa Mfariji na alipata nguvu aliyohitaji kurejea Kanisani. Aliniambia kwamba uzoefu huu ulimrejesha kiroho na kihisia kwenye maisha na ulimsaidia kuondoa hisia za uchungu zilizojikusanya kwa miaka mingi kwa sababu ya uzoefu mgumu aliokuwa ameupitia.

Kama jinsi rafiki yangu mpendwa profesa aliyetajwa kabla alivyosema, daima kuna kitu cha kupendeza na cha kuvutia cha kujifunza kuhusu Yesu Kristo na injili Yake.27 Bwana ametoa ahadi za kupendeza ambazo zimetolewa kwa wale wote, ikijumuisha sisi, wanaotafuta kujifunza Kwake na kujumuisha maneno Yake kwenye maisha yao. Kwa Henoko Yeye alisema, “Tazama Roho yangu [itakuwa] juu yako, kwa sababu hiyo maneno yako yote nitayahesabia kuwa haki; na milima itakukimbia mbele yako, na mito itageuka kutoka uelekeo wake; nawe utakaa ndani yangu, nami ndani yako.”28 Kupitia mtumishi Wake Mfalme Benjamini, Yeye alitangaza, “Mtaitwa watoto wa Kristo, wanawe, na mabinti zake; kwani tazama, siku hii amewazaa kiroho; kwani mnasema kwamba mioyo yenu inabadilishwa kwa imani katika jina lake; kwa hivyo, amewazaa na mkawa wanawe na mabinti zake.”29

Kwa hiyo, kadiri kwa dhati na daima tunavyojitahidi kujifunza juu ya Mwokozi na kufuata mfano Wake, ninawaahidi, katika jina Lake, kwamba sifa Zake za kiungu zitaandikwa kwenye akili na mioyo yetu,30 kwamba tutakuwa zaidi kama Yeye, na kwamba tutatembea pamoja Naye.31

Wapendwa akina kaka na dada zangu, ninaomba kwamba daima tutasimama katika kumstaajabia Yesu Kristo na upendo Wake kamili, usio na mwisho na mkamilifu. Hebu kumbukumbu ya kile macho yetu yalichoona na mioyo yetu ilichohisi iongeze kustaajabu kwetu kwenye dhabihu ya upatanisho ya Mwokozi, ambayo inaweza kutuponya majeraha yetu ya kiroho na kihisia na kutusaidia kusonga karibu Naye. Na tustaajabu kwa ahadi kuu ambazo Baba anazo mikononi Mwake na ambazo ameziandaa kwa wale walio waaminifu:

“Ufalme ni wenu na baraka zake ni zenu na utajiri wa milele ni wenu.

Na yule apokeaye vitu kwa shukrani atatukuzwa.”32

Yesu ndiye Mkombozi wa ulimwengu na hili ni Kanisa Lake. Ninatoa ushahidi wa kweli hizi katika jina lenye msukumo wa kustaajabisha, takatifu na tukufu la Mwokozi wetu Yesu Kristo, amina.