Mkutano Mkuu
Kila Mmoja Wetu Ana Hadithi
Mkutano mkuu wa Aprili 2022


Kila Mmoja Wetu Ana Hadithi

Tafadhali njoo upate familia yako, vizazi vyako vyote, na kuwalete nyumbani.

Marafiki, akina kaka na akina dada, kila mmoja wetu ana hadithi. Tunapogundua hadithi yetu, tunaunganika, ni wa, na tunakuwa.

Jina langu ni Gerrit Walter Gong. Gerrit ni jina la Kidachi, Walter (jina la baba yangu) ni la Kimarekani, na Gong bila shaka ni la Kichina.

Wataalamu wanakadiria baadhi ya watu bilioni 70–110 wameishi duniani. Labda ni mmoja tu ndiye anayeitwa Gerrit Walter Gong.

Kila mmoja wetu ana hadithi. Ninapenda “mvua usoni mwangu [na] upepo mwanana ukipita.”1 Mimi uwayawaya-legelege pamoja na pengwini katika Antartica. Ninawafadhili yatima katika Guatamala, watoto wa mtaani katika Kambodia, wanawake wa Kimaasai katika Mara ya Afrika picha zao wenyewe za kwanza.

Ninasubiri hospitalini wakati kila mtoto wetu anapozaliwa—wakati mmoja daktari aliniomba nisaidie.

Ninamwamini Mungu. Mimi ninaamini “[sisi] tupo, kwamba [sisi] tungeweza kuwa na shangwe,”2 kwamba kuna nyakati na misimu kwa kila kitu chini ya mbingu.3

Je, unajua hadithi yako? Jina lako linamaanisha nini? Idadi ya watu ulimwenguni iliongezeka kutoka bilioni 1.1 katika mwaka wa 1820 hadi kukaribia bilioni 7.8 katika mwaka wa 2020.4 Mwaka wa 1820 huonekana kuwa wakati wa mabadiliko katika historia. Wengi waliozaliwa baada ya mwaka wa 1820 wana kumbukumbu na rekodi hai za kutambua vizazi kadhaa vya familia. Je, unaweza kufikiria kumbukumbu nzuri, maalumu ukiwa na babu au bibi au wanafamilia mwingine?

Bila kujali idadi jumla ya watu ambao wameishi duniani, ina mipaka, inahesabika, mtu mmoja kwa wakati. Wewe na mimi, kila mmoja ana maana.

Na tafadhali fikria hili: kama tunawajua au hatuwajui, kila mmoja amezaliwa na mama na baba. Na kila mama na baba amezaliwa na mama na baba.5 Kwa ukoo wa kuzaliwa au kupangwa utoto, sisi hatimaye wote tunaunganika katika familia ya Mungu na familia ya binadamu.

Aliyezaliwa 837 BK., babu yangu mkuu wa 30, Dragon Gong wa Kwanza, alianzisha kijiji cha familia yetu katika Uchina kusini. Mara ya kwanza kutembelea kijiji cha Gong, watu walisema, “Wenhan huilaile” (“Gerrit amerudi”).

Katika upande wa mama yangu, mti wetu wa familia unajumuisha maelfu ya majina, na zaidi ya kugunduliwa.6 Sisi, kila mmoja wetu ana wanafamilia zaidi ambao wanaweza kuungana nao. Kama unafikiria shangazi yako mkuu ameshakamilisha nasaba yako, tafadhali watafute binamu zako na binamu wa binamu. Unganisha kumbukumbu yako hai ya majina na bilioni 10 za majina yaliyo katika FamilySearch sasa katika kusanyiko lake la mtandaoni na watu bilioni 1.3 katika Mti wa Familia.7

Picha
Mti hai ukiwa na mizizi na matawi

Waombe marafiki au familia kuchora mti hai. Kama Rais Russell M. Nelson anavyofundisha, miti hai ina mizizi na matawi.8 Hata ikiwa wewe uko katika kizazi chako cha kwanza au cha kumi, unganisha jana kwa ajili ya kesho. Unganisha mizizi na matawi katika mti wa familia yako hai.9

Swali “Unatokea wapi? Huuliza uzao, mahali pa kuzaliwa, nchi ya nyumbani au nyumbani. Ulimwenguni, asilimia 25 yetu tunarudi nyuma hadi nyumbani kwetu Uchina, asilimia 23 India, asilimia 17 Asia ya Pasifiki, asilimia 18 Uropa, asilimia 10 Afrika na asilimia 7 Amerika.10

Swali “Unatokea wapi?” pia hutualika kugundua utambulisho wetu wa kiungu na madhumuni ya kiroho katika maisha.

Kila mmoja wetu ana hadithi.

Familia ninayoijua waliunganisha vizazi vitano vya familia wakati walitembelea nyumba yao ya zamani katika Winnipeg, Kanada. Huko Babu alimwambia wajukuu wanaume kuhusu siku wamisionari wawili (yeye aliwaita malaika kutoka mbinguni) walileta injili ya Yesu Kristo ya urejesho, ikabadilisha familia yao milele.

Mama ninayemjua aliwaalika watoto wake na binamu zao kumuuliza bibi yao mkuu kuhusu uzoefu wake wa utotoni. Matukio na masomo ya maisha ya Bibi Mkuu sasa ni kitabu tunu cha familia kinachounganisha vizazi.

Mvulana ninayemjua anatengeneza “shajara ya Baba.” Miaka iliyopita, gari lilimgonga na kumuua baba yake. Sasa, ili kumjua baba yake, huyu mvulana jasiri anahifadhi kumbukumbu za utotoni na hadithi kutoka kwa familia na marafiki.

Nilipouliza pale maana ya maisha hutoka, watu wengi wanasema familia kwanza.11 Hii hujumuisha familia iliyo hai na iliyopita awali. Bila shaka, tunapokufa, hatuachi kuwepo. Tunaendelea kuishi kwenye upande mwingine wa pazia.

Bado wako hai kabisa, mababu zetu wana haki ya kukumbukwa.12 Tunakumbuka jadi yetu kupitia historia simulizi, kumbukumbu ya ukoo na hadithi za familia, kumbukizi au sehemu za ukumbusho, na sherehe za picha, chakula, au vitu vinavyotukumbusha wapendwa wetu.

Fikiria pale unapoishi—si inapendeza sana jinsi nchi yako na jamii yako uwakumbuka na kuwaheshimu wahenga, familia, na wengine ambao walitumikia na kutoa dhabihu. Kwa mfano, katika ukumbusho wa mavuno ya majira ya majani kupuputika katika Molton Kusini, Devonshire, England, Dada Gong nami tulipenda kupata kanisa dogo na jamii pale vizazi vya familia ya Bawden iliishi. Tunawaheshimu mababu zetu kwa kufungua mbingu kupitia kazi ya hekaluni na historia ya familia13 na kwa kuwa kiungo cha weko14 katika nyororo ya vizazi vyetu.15

Katika kizazi cha “Najichagua mimi,” jamii zinafaidika wakati vizazi vinaunganika katika njia za maana. Tunahitaji mizizi ili kuwa na mabawa—mahusiano halisi, huduma ya maana, maisha zaidi ya uzuri bandia unaopita wa mtandao wa kijamii.

Kuunganika na mababu zetu kunaweza kubadilisha maisha yetu katika njia ya kushangaza. Kutokana na majaribu na mafanikio yao, tunapata imani na nguvu.16 Kutokana na upendo na dhabihu yao, tunajifunza kusamehe na kusonga mbele. Watoto wetu wanakuwa wakakamavu. Tunapata ulinzi na nguvu. Miunganiko na mababu huongeza ukaribu wa familia, shukrani, miujiza. Miunganiko kama hii inaweza kuleta msaada kutoka upande mwingine wa pazia.

Kama vile tu shangwe huja katika familia, vile vile huzuni. Hakuna mtu aliye kamili, wala familia yoyote. Wakati wale ambao wanapaswa kutupenda, kutulea, na kutulinda wanashindwa kufanya hivyo, tunahisi kutelekezwa, kuaibika, kuumia. Familia inaweza kuwa ganda tupu. Hali, kwa msaada wa mbinguni, tunaweza kuja kuelewa familia zetu na kufanya amani kila mmoja na mwingine.17

Wakati mwingine sharti lisiloyumba la kudumisha mahusiano ya familia hutusaidia kutekeleza vitu vigumu. Katika hali zingine, jamii huwa familia. Msichana wa ajabu ambaye familia yake ilikuwa inasumbuka walihama kila mara walipata familia ya Kanisa popote alipokuwa na kumlea na kumpa makazi. Mpangilio wa jenetiki na familia ushawishi lakini hauamui sisi ni kina nani.

Mungu anataka familia zetu kuwa na furaha na kuwa za milele. Milele ni muda mrefu sana kama tunafanyiana kukosa furaha. Furaha ni fupi sana kama mahusiano tunayoenzi yanaisha na maisha haya. Kupitia maagano matakatifu, Yesu Kristo anatoa upendo Wake, nguvu, na neema inaweza kutubadilisha18 na huponya mahusiano yetu. Huduma ya kujitolea ya hekalu kwa ajili ya wapendwa wetu hufanya upatanisho wa Mwokozi wetu kuwa halisi kwa ajili yao na sisi. Tukitakaswa, tunaweza kurudi nyumbani kwenye uwepo wa Mungu kama familia zilizounganishwa milele.19

Kila moja ya hadithi zetu ni safari bado inayoendelea, tunapogundua, kutengeneza, na kuwa na uwezekano unaopita kufikirika.

Nabii Joseph Smith alisema: “Yawezekana kwa wengine ikaonekana ni mafundisho mazito sana ambayo tunayazungumzia—uwezo ambao huandika au hufunga duniani na kufungwa mbinguni.”20 Ujamaa tunaotengeneza hapa unaweza kuwepo pamoja na utukufu milele hapa.21 Hakika, “sisi pasipo wao hatuwezi kukamilika; wala wao pasipo sisi hawawezi kukamilika,” hiyo ni “muungano wote mzima na ulio mkamilifu.”22

Je, Tunaweza kufanya nini sasa?

Kwanza, fikiria picha yako ikiakisiwa huko na kule kati ya vioo viwili vya umilele. Katika mwelekeo mmoja, jione mwenyewe kama binti, binti mjukuu, binti kitukuu; katika upande mwingine, tabasamu mwenyewe kama shangazi, mama, bibi. Jinsi gani wakati unapita upesi! Kila wakati na wajibu, tazama ni nani aliye pamoja nawe. Kusanya picha zao na hadithi zao; utengeneze kumbukumbu halisi. Andika majina yao, uzoefu wao, tarehe muhimu. Wao ni familia yako—familia uliyonayo na familia unayotaka.

Unapofanya ibada za hekaluni kwa ajili ya wanafamilia, roho wa Eliya, onyesho la Roho Mtakatifu akitoa ushahidi wa asili ya kiungu ya familia,23 itafuma mioyo ya baba zenu, mama zenu, na watoto pamoja kwa upendo.24

Pili, acha tukio la historia ya familia kuwa kwa kusudi na kwa hiari. Mpigie simu bibi yako. Tazama kwa makini katika macho ya huyo mtoto mchanga. Tenga muda—gundua umilele—katika kila hatua ya safari yako. Jifunze na ukiri kwa shukrani na uaminifu urithi wa familia yako. Sherehekea na kuwa chanya na, inapohitajika, kwa unyenyekevu fanya kila kitu kinachowezekana usilete kilicho hasi. Acha mambo mema yaanze nawe.

Tatu, tembelea FamilySearch.org. Pakua app za vyombo tamba zinazopatikana. Ni za bure na zinafurahisha. Gundua, unganika, kuwa wa. Ona jinsi unavyohusiana na watu chumbani, jinsi ilivyo rahisi na inavyoridhisha kuongeza majina kwenye mti wa familia iliyo hai, kupata na kubariki mizizi yako na matawi yako.

Nne, saidia kuunganisha familia milele. Kumbuka demografia za mbinguni. Kuna wengi zaidi kwenye upande mwingine wa pazia kuliko upande huu. Kadri mahekalu zaidi yanapokuja karibu nasi tafadhali toa fursa kwa wale wanasubiri kupokea ibada za hekaluni.

Ahadi ya Pasaka na daima ipo pale, katika na kupitia Yesu Kristo, tunaweza kuwa hadithi zetu bora na familia zetu zinaweza kuwa na furaha na kuwa za milele. Katika vizazi vyote, Yesu Kristo anawaponya waliovunjika moyo, kuwakomboa wafungwa, kuwaacha huru waliovilia.25 Agano la Mungu na kila mmoja wetu26 hujumuisha kujua roho yetu na mwili wetu utaunganika tena katika ufufuko na mahusiano yetu ya thamani zaidi yanaweza kuendelea kupita kifo kwa ujalivu wa shangwe.27

Kila mmoja wetu ana hadithi. Je, unaweza kugundua yako? Njoo upate sauti yako, wimbo wako, uwiano wako Naye. Hili ndilo kusudi hasa la kile Mungu aliumba mbingu na dunia na kuona kwamba vilikuwa vizuri.28

Sifu mpango wa furaha wa Mungu, Upatanisho wa Yesu Kristo, urejesho endelevu katika injili Yake na Kanisa Lake. Tafadhali njoo upate familia yako, vizazi vyako vyote, na kuwalete nyumbani. Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. “My Heavenly Father Loves Me,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 228–29.

  2. 2 Nefi 2:25.

  3. Ona Mhubiri 3:1.

  4. Based on United Nations Secretariat, The World at Six Billion (1999), 5, table 1; “World Population by Year,” Worldometer, worldometers.info.

  5. Wengi wamebarikiwa kuwa na wazazi ambao hawakuwazaa wao, bado wameunganika kama familia kupitia kamba za upendo na kupangwa na maagano matakatifu ya kuunganishwa.

  6. Natoa shukrani kwa wale ambao wanaasisi njia za kupanga idadi kubwa na majina ya familia katika miti ya familia.

  7. Katika mwaka wa 2021, majina milioni 99 yaliongezwa katika miti ya familia ya uma. Na karibuni, kufanya kidigitali kwa kanda milioni 2.4 za filamu zilizo na takribani majina bilioni 37 kulimalizika (baadhi ni za kurudufiwa). Rekodi hizi za majina ya watu binafsi zinaweza sasa kuandaliwa kupekuliwa, kupatikana, na kuongezwa kwenye mti wa familia ya binadamu.

  8. Ona Russell M. Nelson, “Roots and Branches,” Ensign, May 2004, 27–29.

  9. Bila shaka, tunapogundua na kujenga mti wetu wa familia, tafadhali dumisha asilimia 100 ya heshima kwa ajili ya usiri na ushiriki wa kujitolea wa wanafamilia, wanaishi na wafu.

  10. David Quimette extrapolated these numbers, based on Angus Maddison, The World Economy: A Millennial Perspective (2001), 241, table B-10.

  11. Ona Laura Silver and others, “What Makes Life Meaningful? Views from 17 Advanced Economies,” Pew Research Center, Nov. 18, 2021, pewresearch.org.

  12. 1 Nefi 9:5; 1 Nefi 19:3; Maneno ya Mormoni 1:6–7; na Alma 37:2 huzungumzia kuweka kumbukumbu na kukumbuka “kwa kusudi lenye hekima,” ikijumuisha kubariki vizazi vijavyo.

  13. Ona Russell M. Nelson and Wendy W. Nelson, “Open the Heavens through Temple and Family History Work,” Ensign, Oct. 2017, 34–39; Liahona, Oct. 2017, 14–19; ona pia “RootsTech Family Discovery Day—Opening Session 2017” (video), ChurchofJesusChrist.org.

  14. Ona Mafundisho na Maagano 128:18.

  15. Ona Gordon B. Hinckley, “Keep the Chain Unbroken” (Brigham Young University devotional, Nov. 30, 1999), speeches.byu.edu. Rais Hinckley pia alinukuliwa katika David A. Bednar, “A Welding Link” (worldwide devotional for young adults, Sept. 10, 2017), broadcasts.ChurchofJesusChrist.org.

  16. Kwa mfano, katika familia yetu, Henry Bawden, ktoka Devonshire, England, alimuoa Sarah Howard, ambaye alihama pamoja na familia baada ya kujiunga na Kanisa. Sarah akiwa St. Louis kama msichana, baba yake, mama yake, na ndugu zake watano walikufa. Henry na Sarah walikuwa na watoto 10. Sara pia aliwalea watoto sita wa mke wa kwanza wa Henry, Ann Ireland, baada ya yeye kufa. Sarah pia alikuwa mama kwa wajukuu wa kike wadogo wawili baada ya mkaza mwana wa (Sarah) kufa. Licha ya changamoto nyingi za maisha, Sarah alikuwa mchamgamfu, mwenye upendo, mwenye huruma, na bila shaka mchapakazi. Yeye alijulikana kama “Bibi Mdogo.”

  17. Vigumu kama ingekuwa, tunapojisamehe wenyewe na mmoja na mwingine kwa msaada wa Kristo, tunakuwa “watoto wa Mungu” (Mathayo 5:9).

  18. Ona, kwa mfano, Mosia 3:19.

  19. Ona “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” ChurchofJesusChrist.org.

  20. Mafundisho na Maagano 128:9.

  21. Ona Mafundisho na Maagano 130:2.

  22. Mafundisho na Maagano 128:18.

  23. Russell M. Nelson, “A New Harvest Time,” Ensign, May 1998, 34; ona pia Russell M. Nelson and Wendy W. Nelson, “Open the Heavens through Temple and Family History Work,” 16–18.

  24. Ona Mosia 18:21.

  25. Ona Luka 4:18.

  26. Niliambiwa neno la Kiebrania kwa familia—mishpachah—hutoka kwenye neno lenye mzizi la Kiebrania (shaphahh) kumaanisha “kuunganisha au funga pamoja.” Kila nafasi ndani ya familia imesanifiwa kuimarisha kamba za familia.

  27. Ona Mafundisho na Maagano 88:15–16, 34; 93:33; 138:17.

  28. Ona Mwanzo 1:4, 31.