Mkutano Mkuu
Ujumbe wa Utambulisho
Mkutano mkuu wa Aprili 2022


Ujumbe wa Utambulisho

Tunawaheshimu mabinti za Mungu katika kikao hiki cha kipekee kwa kujikita katika dukuduku zao na zile za vikundi vyao.

Tunaponza kikao hiki ambacho si cha kawaida cha Wanawake cha mkutano mkuu, nina furahi kutoa ujumbe huu wa Utambulisho kutoka kwa Urais wa Kwanza.

Vikao vyetu vya Jumamosi vina historia ya azma tofauti na umati tofauti. Jioni hii tunaongeza kwenye historia hiyo tunapojiingiza kwenye azma na utaratibu mpya kwa ajili ya wakati ujao. Injili ya Yesu Kristo haibadiliki. Mafundisho ya Injili hayabadiliki. Maagano yetu binafsi hayabadiliki. Lakini katika miaka mingi, mikutano tunayoifanya kuwasilisha jumbe zetu inabadilika na kuna uwezekano wa kuendelea kubadilika kadiri ya miaka iendavyo.

Kwa sasa, mkutano huu wa Jumamosi jioni ni sehemu ya mkutano mkuu, si kikao cha kikundi chochote. Kama ilivyo kwa vikao vyote vya mkutano mkuu, upangaji, wazungumzaji, na muziki ni jukumu la Urais wa Kwanza.

Tumemuomba Rais Jean B. Bingham, rais wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, kuongoza kikao hiki. Vikao vijavyo vya Jumamosi jioni vinaweza kuongozwa na mmoja wa Maofisa Wakuu wengine wa Kanisa, kama vile washiriki wa urais wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, Wasichana, na Msingi, waliopewa jukumu na Urais wa Kwanza.

Jioni hii, kikao hiki cha Jumamosi cha mkutano mkuu kitajikita kwenye dukuduku za Wanawake watakatifu wa Siku za mwisho. Hii itajumuisha mafundisho ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za mwisho, sera za Kanisa ambazo ni hususan kwa wanawake, na majukumu ya jumla na kazi za vikundi ambavyo vinajumuisha wanawake na wasichama wa Kanisa. Ingawa kwa kudhamiria matangazo yanarushwa kwa mikusanyiko yote ulimwenguni kama ilivyo kwa vikao vyote vya mkutano mkuu, mkusanyiko ulioalikwa kwenye Kituo cha Mikutano kwa ajili ya kikao hiki ni wanawake na wasichana wa miaka 12 na zaidi. Tumewajumuisha baadhi ya viongozi wa ukuhani wanao simamia vikundi vinavyoshiriki.

Tunacho kianzisha hapa ni kulingana na nyenzo za kimawasiliano zipatikanazo sasa kwa ajili ya uongozi wa Kanisa la ulimwenguni kote la Bwana na uumini. Mafundisho ya injili ya Yesu Kristo ni kwa ajili ya wote, hivyo hii ni sababu yetu kuu na ukubwa wa uenezaji. Tunawaheshimu mabinti wa Mungu katika kikao hiki cha kipekee kwa kujikita katika dukuduku zao na zile za vikundi vyao.

Tuna shukrani kwamba teknolojia ya urushaji matangazo sasa inawapa viongozi wa Kanisa uwezo wa kuendesha mafunzo ya kina kwa kuhutubia mikusanyiko maalumu katika eneo. Pia tunatambua ukweli kwamba fursa za usafiri kwa sasa zinaongezeka. Hiyo huturuhusu kuwapeleka viongozi wa Kanisa kuendesha mafunzo ya uongozi yanayohitajika mara kwa mara moja kwa moja katika eneo husika.

Hii ni kazi ya Bwana Yesu Kristo. Sisi ni watumishi wake, tunaoelekezwa na Roho Wake Mtakatifu. Tunatoa baraka za Bwana wetu juu ya viongozi wa vikundi hivi na juu ya wanawake na wasichana waaminifu wanaomtumikia Bwana katika vikundi hivi na katika maisha yao binafsi, katika jina la Yesu Kristo, amina. Katika Jina la Yesu Kristo, amina.