Mkutano Mkuu
Video: “Nyinyi Ndio Wanawake Aliowaona”
Mkutano mkuu wa Aprili 2022


Video: “Nyinyi Ndio Wanawake Aliowaona”

Mnamo 1979 Rais Spencer W. Kimball alikuwa hospitalini na alimwomba mkewe, Camilla, kusoma hotuba yake kwenye mkutano mkuu wa wanawake.

Dada Camilla Kimball: “Mengi ya ukuaji mkubwa unaokuja kwa Kanisa katika siku za mwisho utakuja kwa sababu wengi wa wanawake wema wa ulimwengu (ambao mara nyingi ndani yao kuna hisia ya ndani ya kiroho) watavutwa Kanisani kwa idadi kubwa. Hii itatokea kwa kiasi kwamba wanawake wa Kanisa wataonyesha uadilifu na ufasaha katika maisha yao na kwa kiasi kwamba wanawake wa Kanisa wanaonekana wa kipekee na tofauti—katika njia za furaha—tofauti na wanawake wa ulimwengu.”1

Raisi Russell M. Nelson: “Dada zangu wapendwa, ninyi ambao ni washirika wetu muhimu wakati wa tukio hili la mwisho, siku ambayo Rais Kimball aliitabiri ni leo. Nyinyi ndiyo wanawake aliowaona! Maadili yenu, nuru, upendo, maarifa, ujasiri, tabia, imani na maisha ya haki vitawavuta wanawake wema wa ulimwengu, pamoja na familia zao, kuja Kanisani kwa wingi wa kipekee!

“Sisi … tunahitaji nguvu yenu, uongofu wenu, kusadiki kwenu, uwezo wenu wa kuongoza, busara yenu na sauti zenu. Ufalme wa Mungu si kamili na hauwezi kukamilika bila wanawake wanaofanya maagano matakatifu na kisha kuyashika, wanawake wanaoweza kuongea kwa uwezo na mamlaka ya Mungu! …

“… Bila kujali wito wako, hali yako yoyote ile, tunahitaji maoni yako, umaizi wako na msukumo wako. Tunawataka mseme bila woga na kwa uwazi katika mabaraza ya kata na vigingi. Tunamtaka kila dada aliyeolewa kuzungumza kama ‘mchangiaji na mwenza kamili’ pale unapoungana na mumeo katika kuongoza familia yenu. Mlioolewa au waseja, ninyi akina dada mna uwezo anuai na wa kipekee wa kuchakata ambayo mmepokea kama vipawa kutoka kwa Mungu. Sisi akina kaka hatuwezi kunakili ushawishi wenu wa kipekee.

“Tunajua kwamba kitendo cha kutamatisha uumbaji wote kilikuwa ni uumbaji wa mwanamke! Tunahitaji uwezo wenu! …

“… Ninawashukuru, dada zangu wapendwa, na kuwabariki kupanda hadi kimo chenu kamili, kutimiza kipimo cha uumbaji wenu, tunapotembea bega kwa bega katika kazi hii takatifu. Kwa pamoja tutasaidia kuuandaa ulimwengu kwa Ujio wa Pili wa Bwana.”2

Muhtasari

  1. Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Spencer W. Kimball (2006), 222–23.

  2. Russell M. Nelson, “A Plea to My Sisters,” Ensign or Liahona, Nov. 2015, 96, 97.